Wednesday, March 30, 2011

Rais wa Syria ahutubia wananchi baada ya maandamano.

Rais wa Syria ahutubia na wanachi baada ya maandamano. Syria, Damascus - 30/03/2011. Rais wa Syria amelihutubia taifa siku kadhaa baada maandamano yaliyo fanyika nchini humo kutaka mageuzi.

Akiongea kupitia runinga na mbele ya bunge rais Bashar al Asad alianza kwa kusemasema " mimi ni Msyria na yoyote ambaye ni Msyria atakuwa anajidai kwa kutembea kifua mbela."
Najua Wasyria walikuwa wanasubiri maoni yangu, lakini ulinibidi nisubiri ili nipate picha kamili na huhakika wa hali halisi ili kuto wapa maadui wa Syria kutokana na hali iliyokuwawakati huo."
Naomba niwaeleze Wasyria wenzangu lazima tuwe na umoja na tutatue tofauti zetu bila magomvi na tuta shinda mbinu zinazo tumiwa na vyombo vya habari ambavyo vinatumika kudanganya dunia kuhusu hali ya nchi yetu."
Rais Al-Asad alikuwa akihutubia ili kuelezea ni kwa jinsi gani uongozi wake unavyo kabiriana na mageuzi yanato likumba bara la Waarabu.

No comments: