Thursday, March 10, 2011

Dalai Lama kuachia madaraka hivi karibuni.

Dalai Lama kuachia madaraka hivi karibuni. Dharamshala,India - 10/03/2011.Kiongozi wa kiimani ambaye ni mzaliwa wa himaya za Tibeti ametangaza atajiudhulu maswala yote ya kisiasa.

Dalai Lama, ambaye amekuwa kiongozi wa wananchi wa Himaya za Tibeti alitangaza habari hizo kwa kusema" nafikili umefika wakati wa kumchagua kiongozi mwingine atakaye waongoza wana Tibeti na umefika wakati wa kutoa nafasi hiyo."
Dalai Lama ambaye anaishi ugenini nchini India baada ya kukumbi kutoka himaya za Tibet baada ya mapinduzi kushindwa zidi ya serikali ya China mnamo miaka ya mwisho ya hamsini.
Ufansa yaitambua serikali ya wapinzani wa Muammar Gaddafi.
Paris, Ufaransa - 10/03/2011. Serikali ya Ufaransa imekuwa nchi ya kwanza kuitambua serikali ya upinzani inayo mpinga kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.
Akiongea mbele ya ujumbe na viongozi wa upinzani rais wa Ufaransa Nicolas Sozy alisema " tunaelewa umuhimu wa kuwaunga mkono watu wa Libya."
Uamuzi huo wa Ufaansa umekuja baada ya Amerika, na washiriki wake kutaka kuwepo na uzuizi wa anga ili kumdhibiti kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi kutumia anga katika mashambulizi zidi ya wapinzani wa serikali.

No comments: