Monday, March 21, 2011

Vladmil Putin alaani mashambulizi zidi ya LIbya.

Vladmil Putin alaani mashambulizi zidi ya Libya. Moscow, Urussi 21/03/2011. Waziri mkuu wa Urussi amezilaumu nchi za magharibi kwa kitendo chake cha kuishambulia Libya.

Vladamil Putin alisema " mashambulizi yanayo endelea nchini Libya ni ya kishetani na Amerika na washiriki wake wanafanya mashambulizi bila hata kufikilia mbele."
Na hii inaashiria ya kuwa lazima tuongeze uwezo wetu wa kijeshi ili kuendana na hali ahalisi."
Wakati huo huo, mtoto wa kiongozi wa Libya Saif al Gaddafi amesema "rais wa Ufaransa Nikolas Sarkozy anatakiwa kurudisha pesa zote ambazo serikali ya Libya ilimsaidia wakati wa kampeni zake za Urais, kwani malipo yake ni kuongoza na kuwa kinara wa kutushambulia kivita na kusahahu misaada yote na tunao ushahidi."
Hata hivyo msemaji wa rais Nikolas Sarkozy amekanusha maelezo hayo yaliyo tolewa na mtoto wa Muammar Gaddafi.

1 comment:

Anonymous said...

For sure american,s and his allied powers are devils they got no right to Libyan people .....African's problems will be solved by african's ourself.what they need is oil weath of Libya ......we african's we are together with Col.Ghadafy and the Libyan people until the end of the world.