Thursday, May 26, 2011

Serikali ya Libya kuitaka Uhispania katafuta njia ya luleta amani.

Madrid, Uhispania - 26/05/2011.Serikali ya Uhispania imepokea maombi kutoka serikali ya Libya ya kutaka kuwepo na mazungumzo ya kusimamisha vita vinavyo endelea nchini Libya. Habari kutoka ofosi ya waziri mkuu wa Uhispania, zinasema " tumepokea mswaada kutoka serikali ya Libya ambao unaomba kuwa na mazungumzo ya kuleta amani nchini Libya." Akiongea mbele ya waandishi wa habari, waziri mkuu wa Libya Al-Baghdadi al Mahmoud "alisema serikali ya ke ingependelea kuanza mazungumzo ya kuleta amani na kusimamisha mashambulizi nchini Libya yanayofanywa na NATO." "Na Muammar Gaddafi bado na atakuwa kiongozi wa LIbya, na kama Gaddafi akiondolewa kwa kutumia nguvu, basi hakutakuwepo na Libya watu wanayo tarajia." Hata hivyo, kundi la upinzani linalo pinga serikali ya Gaddafi, linadai lazima kiongozi huo ataoke madarakani na ndipo amani ipataikane.

No comments: