Tuesday, May 31, 2011

Mshukiwa wa mauaji ya Serbia,Meja Ratko Mladik kupelekwa Uhollanzi.

Mshukiwa wa mauaji ya Serbia, meja Ratko Mladik kupelekwa Uhollanzi.
Belgrade, Serbia - 31/05/2011.Mahakama kuu nchini Serbia imekataaa na kuitupilia mbali rufaa ya mshukiwa na muhusika mkuu wa mauaji ya liyo tokea wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyo tokea miaka ya 1991-95.
Mtuhumiwa huyo Ratko Mladik, ambaye alikuwa mkuu wa majeshi anakabiliwa na mashitaka ya dhidi yake kwa kuhusika na mauaji ambayo yalisababishwa na vita hivyo, wakati yeye akiwa kama mkuu wa majeshi.
Kufuatia kukataliwa rufaa hiyo, mkuu wa majeshi huyo Ratko Mladik, anatarajiwa kupelekwa kwenye mahakama kuu ya kutetea haki za binandamu iliyopo nchini Hollanzi ili kujibu mashitaka yanayo mkabili.
Hata hivyo kabla ya kupelekwa nchini Uhollanzi, Ratko Mladik, aliruhusiwa kutembela kaburi la mwanaye wa kike ambaye alijiua baada ya baba yake kushutumiwa ya kuwa anamehusika katika mauaji.

No comments: