Sunday, May 15, 2011

Mkurugenzi wa IMF akabiliwa na shitaka la ubakaji.

Umoja wa mataifa waagiza kutotupa vyakula ovyo. Hong Kong, China - 15/05/2011. Shirika la umoja wa mataifa linalo shughulikia maswala ya kilimo na chakula duniani limeagiza tabia ya kutupoteza au kuharibu vyakula usimamishwe mara moja. Kwa mijibu wa shirika hilo limesema, "nchi tajiri na watu matajiri ndiyo huwa wanatupa au kuharibu vyakula kwa wingi kuliko wale watu masikini na nchi masikini." Kwa kuongea habari hizo zimesisitiza zaidi ya asilimia thelathini, huwa kuharibiwa karibu kila mwaka duniani kutokana na kutokuwa makini. Mkurugenzi wa IMF akabiliwa na shitaka la ubakaji. New York, Amerika - 15/05/2011. Mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la kutathmini maswala ya fedha namisaada ya kifedha -Internaltional Monetary Fund(IFM) amefunguliwa mashitaka. Dominik Strauss Kahn, alikamatwa na polisi baada ya muhudumu mmoja katika hotel aliyo kuwa amefikia kudai yakuwa alisumbiliwa kijinsia na mkurugenzi huyo. Msemaji wa polisi, Ryan Sesa alisema, Dominik Strauss Kahn, amekamatwa na polisi wakati akiwa njiano kuelekea uwanja wandege. Hata hivyo mwansheria wa Dominik Strauss, amesema "mteja wake atakana shitaka hilo." Domink Strauss, ambaye inasemekana alikuwa mmoja ya wale viongozi waliokuwa wamepanga kugombe akiti cha urais wa Ufaransa mwaka 2012 ili kuchuana na rais wa sasa. Marekani ya sema Walibya ndiyo wataamua uongozo wao Washington, Marekani - 15/05/2011. Viongozi wa serikali ya upinzani wa Libya wameondoka kwa shingo upande baada ya selikali ya Amerika kushindwa kuikubali kimsaada wa hali na mali. Kwa mujibu wa habari kutoka ikulu ya Marekani zinasema, "serikali ya Amerika haiwezi kuitambua au kuuutambua uongozi huo, kwani uamuzi huo upo mikononi mwa wanachi wa Libya kuwachagua viongozi wao." Hata hivyo serikali ya Amerika, imesisitiza msimamo wake wake wakuunga mkono wanchi wa Libya katika harakati za kuleta mabadiliko ya kisiasa na demeokrasia. Wakati huo huo wataalamu wa mabo ya kisiasa, kidiplomasia na uchumi, wanasema "vita vinavyo endelea nchini Libya, vinasababishwa na nchi zenye hisa nchini humo, nahasa nia kubwa ni kuhakikisha Urussi na China zisitawale maeneo hayo kiuchumi."

1 comment:

Anonymous said...

ccd