Wednesday, May 25, 2011

Obama na Cameron kupambana na Gaddafi hadi mwisho.

Obama na Cameron kupambana na Gaddafi hadi mwisho.
London, Uingereza - 25/05/2011. Waziri mkuu wa Uingereza na rais wa Amerika wakubaliana kwa pamoja yakuwa wataendelea kusisitiza kwa kila hali ili kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi kutoka madarakani.
Wakiongea pamoja, wakati walipo wakiongea na waandishi wa habari, rais wa AAmerika Baraka Obama na David Cameron, walisema, tunaamini zipo nguvu za kutosha za kuhakisha Muammar Gaddafi anaachia madaraka.
Wakati huo huo serikali ya Afrika ya kusini, imesema inafanya mmpango wa kutaka kuleta amani nchi Libya na kuandaa njia ya kutoka madarakani kwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.
Rais Baraka Obama yupo ziarani katika nchi za Ulaya kwa muda wa siku sita.
Kwa mujibu habari kutoka serikali ya Afrika ya Kusini, zinasema, rais wa Jacob Zuma atatembelea Libya ili kutafuta suruhisho katika nchi hivyo ambao, imekuwa na mapigano kati ya serikali ya Libya na wale wanaoipinga.
Libya imekuwa ikishambuliwa na ndege za majeshi ya NATO, ili kupunguza mashambulizi yanayofanywa na serikali ya Gaddafi zidi ya wapinzani wanaopinga serikali.
Serikali ya India kuimarisha uhusiano na bara la Afrika.
Adis Abeba
, Ethiopia - 25/05/2011. Waziri mkuu wa India amehaidi yakuwa serikali yake itakuwa karibu na Afrika, ili kusaidia kujenga uchumi wa bara zima.
Akiwahutubia katika mkutano ulio wakutanisha viongozi wa Afrika na India, waziri mkuu Manmohan Singh alisema, " kuna mafanikio ya kiuchumi ambayo yanaendelea barakani Afrika, na India itashirikiana kikamilifu na bara la Afrika, kwa kuzingatia India na Afrika kunauhusiano mkubwa kihistoria.
Serikali ya India, imekuwa mbioni kuimarisha uhusiano wake na bara la Afrika kwa kuwekeza zaidi ya $5billion, na hii inaonekana ni katika kukabiliana na mataifa kama China, na Umoja wa nchi za Ulaya ambazo zimekuwa zijaribu kushirikiana na serikali za Afrika.

No comments: