Sunday, May 1, 2011

Mashambulizi ya jeshi la NATO laua mtoto wa Gaddafi.

Tripol, Libya- 01/05/2011. Ndege za jeshi la NATO zimeshambulia makazi ya rais wa Libya na maisha ya watu waliokuwepo katika jengo hilo. Kwa mujibu wa msemaji wa serikali Moussa Ibrahim, amesema " Mashambulizi yaliyo fanywa na NATO yameuwa mtot wa mwisho wa kiume Saif al Arab Gaddafi wa Kanali Muammar Gaddafi na wajukuu zake watatu." "Kijana aliye uwawa alikuwa anasoma nchini Ujerumani na hakuwa anahusika na mambo ya kisiasa na hii inaonyesha yakuwa NATO na washiriki wake wanataka kumwua kiongozi wetu. Lakini hata hivyo Koingozi Kanali Muammar Gaddafi yeye na mke wake ni wazima." Mashambulizi dhidi ya serikali ya Libya yalinza li kusinikisha kiongozi wa nchi hiyo kuacha kuwashambulia raia wa Bhengazi na kuachia madaraka ambayo amekuwa akiyashikiria zaidi ya miaka arobaini.

No comments: