Thursday, May 26, 2011

Hatimaye Ratko Mladic akamatwa.

Belgradi, Serbia- 26/05/2011. Serikali ya Serbia imetangaza kukumatwa kwa aliyekuwa mkuu wa jeshi Bosnia Serbi ambaye anakabiliwa na mashitaka ya mauaji wakati wa vita vilivyo tokea mwaka 1992-95. Generali Ratko Mladic ambaye alikuwa natafutwa ili ajibu amshitaka dhidi yake, alipotea mara baada ya kesi dhidi yake kufunguliwa na mahakama ya kimataifa. Akitangaza kuhusu kukumatwa huko, rais wa Serbia Boris Tadic alisema "kwaniaba ya wanchi wa Serbia napenda kuwatangazia ya kuwa Ratko Mladic amekamatwa, na kuanzia sasa tunafungua kitabu kipya ambacho kitatuwezesha kusamehena na kukubaliana kuishi pamoja." "Na tunahaidi wale wote wafanyao mabaya lazima watajibu mashitaka"alimalizia kwa kusema haya rais wa Serbia Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema "Ratko Mladic hakuwa na matata au kuleta kipingamizi wakati wakukamatwa kwake na inasemekana anamatatizo katika moja ya mkono wake."

No comments: