Thursday, May 26, 2011

Viongozi wa nchi za G8 wakutana nchini Ufaransa.

Deauville, Ufransa - 26/05/2011. Viongozi na wakuu wa serikali wa kundi lijulikanalo kama G8 wamekutana nchi Ufaransa ili kujadili hali halisi ya mwenendo wa kiuchumi na kidemokrasia duniani. Wakihutubia nini la kufanya ili kuimarisha uchumi dunia na kuunga mkono mageuzi ya kisiasa duniani, viongozi na wakuu hao wamehaidi kutoa misaada tofauti kwa nchi tofauti kwa kuzingatia hali halisi za nchi hizo na kuhaidi kushirikiana kiuchumi kwa karibu. Vile vile viongozi hao walijadiliana kuhusu machafuko na vita vinavyoendela Libya jambo ambalo linapingwa na baadhi ya viongozi wanao udhuria mkutano huo wa G8 na mageuzi ya nayo endelea katika nchi za Kiarabu.

No comments: