Mahujaji wafanya Hija ya kila mwaka.

Makka, Saudi Arabia - 07/11/2011. Mamilion ya waumini wa dini ya Kiislaam duniani wamefanya Hijja ikiwa ni nguzo mojawapo ya dini ya Kiisalaam.
Mahujaji hao ambao hukutana kila mwaka, ili kutubu dhambi zao na kuomba msamaha kwa Mungu ili wasamehewe yale waliyo yafanya kutokana na udhaifu wa kibinadamu huku wakisema Rabeka Alhaahaa Rabeka Alhaahaa.
Waziri mkuu wa Ugiriki aachia madaraka ya kuongoza nchi.

Athens, Ugiriki - 07/11/2011. Waziri mkuu wa Ugiriki amejiudhulu uongozi wa nchi hiyo na kutoa nafasi ya kuundwa serikali ya muungano itakayo ongoza kutatua uchumi wa nchi hiyo.
George Papandreou alisema alitangaza kujihudhulu baada ya kukutana na rais wa Ugiriki Karolos Papoulias ili mkuzungumzia hali halisi nini kinatakiwa ili kuinua uchumi wa nchi hiyo.
Kufuatia kujiudhulu huko serikali ya muungano itaundwa na inatarajiwa kutangazwa siku ya Jumanne.
Rusia yaonya mashambulizi zidi ya Iran


Moscow, Urusi, 07/11/2011. Waziri wa mambo nje wa Urusi, ameonya ya kuwa kitendo cha kutaka kuishambulia Iran kitaleta madhara makubwa na kufanya eneo zima la Mashariki ya Kati kuwa na vurugu kubwa.
Waziri Sergei Lavrov alisema " swala la nyuklia la nchi ya Iran lazima litatuliwe kwa mazungumzo ya kidiplomasia na siyo kwa ushambulizi wa mabomu."
Waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Urusi aliya sema hayo baada ya rais wa Izrael Shimon Perez kusema "mashambulizi zidi ya Iran yanaweza kutokea."
Mvutano huu wa swala la Iran na nyuklia, umekuwa zaidi huku shirika la kimataifa linalo shughulikia maswala ya kinyuklia kukaribia kutoa ripoti yake kuhusu mradi mzima wa kinyuklia wa Iran.
Hata hivyo Iran, imekuwa ikidai ya kuwa mpango wake wa kinyuklia ni kwa ajili ya kuendeleza maswala ya utafiti na sayansi na kusema ya kuwa pindipo itakapo shambuliwa basi haita kaaa kimya itafanya mashambulizi pia.
Polisi wapambana na waandamanaji jiji Monrovia Liberia
Monrovia, Liberia - 07/11.2011. Jiji la Monrovia nchini Liberia limekumbwa na machafuko baaday police kupambana na waandamanaji wanaounga chama cha upinzani kinacho ongozwa na Winton Tubman.
Maandamano hayo yamefanyika ili kupinga ya kuwa uchaguzi unaotaka kufanyika utakuwa si wa haki na wanaupinga.
Kwa mujibu wa mashaidi "polisi walitumia siraha na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine kujeruhiwa wakati wa maandamano hayo."
Hata hivyo mwakilishi wa umoja wa mataifa aliyepo nchini Liberia Yasmin Bouziane alipo ulizwa kuhusu matukio ya mauaji akukana wala kukubali.
Liberia nchi ambayo ilikuwa na machafuko na mauaji miaka michache iliyo pita, imekuwa na mvutano wa kisiasa ambao umeibuka hivi karibuni kati ya chama cha kisiasa kinacho ongozwa na Bi Ellen Johnson Sirleaf na vile vya wapinzani tangu uchaguzi wa kwanza wa mwaka 2003.
No comments:
Post a Comment