Tuesday, November 8, 2011

Obama na Sarkozy watiwa wasiwasi na kauli za Benjamin Netanyahu.

Aliyekuwa bingwa wa ngumi wa uzito wa juu wa dunia afariki dunia.

Philadelphia, Marekani - 08/11/2011. Aliye kuwa bingwa wa ngumi za uzito wa juu dunia amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani ya ini.
Joe Frazier 67 aliyejulikana kama "Smokin Joe" ambaye aligundulika kuwa na ugonjwa wa saratani ya ini na kulazwa hospital kwa matibabu. Joe the Smokin ambaye alikuwa bingwa wa ngumi za uzito wa juu mwaka 1970 hadi 1973.
Bingwa mwenzake wa dunia kwa muda wote Mohamed Ali alisema " dunia imempoteza bingwa na mpiganaji ambaye hatatokea kama yeye."
Kwani niaba ya launite.blogspot.com Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina.
Obama na Sarkozy watiwa wasiwasi na kauli za Benjamin Netanyahu.
Paris, Ufaransa - 08/11/2011. Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amemwita waziri mkuu wa Izrael Benjamin Netanyahu ya kuwa ni "mwongo" wakati alipo kutana na rais wa Marekani Baraka Obama.
Rais Sarkozy alisikika alisema "siwezi hata kumwelewa na nimechoka naye kwani ni mwongo."
Naye rasi wa Marekani Baraka Obama alisikika akisema "wewe umechoka naye, je mimi mwenzako karibu kila siku na husika naye kwa njia moja au nyingine."
Kauli za viongozi hao zilisikika wakati walipo kutana kabla ya kuanza mkutano wa wakuu wa nchi tajiri G20 uliyo fanyika nchini Ufaransa ili kujadili hali ya uchumi wa dunia ambao unayumba.
Mwana wa Mfalme wa Uingereza atembelea Tanzania.
Dar es Salaam, Tanzania - 08/11/2011. Mwana wa Malkia wa Uingereza na mkwe wamefanya ziara nchini Tanzania ikiwa ni moja ya nchini ambazo walipewa mwaliko na serikali ya nchi hiyo.
Prinsi Charles na mkewe Kamilla katika ziara hiyo wamekutana na rais wa Jakaya Kikwete pia na viongozi mbalimbali wa nchi ya Tanzania na kujadili ni kwa jinsi gani uhusiano uliopo katia ya Tanzania na Uingereza unaweza kudumishwa kwa ukaribu zaidi.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete alisema "Tanzania na Uingereza tunashirikiana katika nyanja zote za kiuchumi na kijamii na ziara hii ya mwana wa Malkia wa Uingereza inaonyesha uhusiano uliopo kati ya kati yetu ni mzuri na utaendelea kudumishwa."
Mwana wa Malkia Prinsi Charles na mkewe Kamilla watakuwa Tanzania kwa muda wa siku tatu.

No comments: