Saturday, July 7, 2012

Afghanistan kuwa mwanachama huria wa NATO.

Serena Williams ashinda Wimbledon kwa mara ya Tano.

London, Uingereza - 07/07/2012. Serena Willliams ameshinda tena kwa mara ya tano kombe la mashindano ya tennis ya Wimbledon.
Serena alimshinda Agnieszka  Rwadwanska kwa 6-1, 5-7, 6-2 na katika mchezo ambao ulikuwa wa vuta ni kuvute.
Ushindi huu Serena Williams wa mara ya tano katika kombe la tennis la Wimbledon  umekamilisha hatua ambayo dada yake Venus alisha wahi kushinda kombe hilo.
Serena Williams ameshinda kombe hilo mwaka 2002,2003,2009, 2010, 2012  na kuwa mmoja ya wacheza tennis kwa upande wa wanawake kushinda kombe tennis la Wimbledon  hilo mara nyingi

Rais wa Afrika ya Kusini achorwa magazetini na sehemu za siri.

Johannesburg, Afrika ya Kusini - 07/07/2012.  Chama tawala nchi Afrika ya Kusini kimelaani kitendo cha mchoraji wa vikatuni wa gazeti la Gurdian na Mail wa Afrika ya Kusini kumchora rais wa nchi hiyo na kuonyesha sehemu zake za siri.
Jonathan Shapiro alichora kikatuni ambacho kinamwonesha rais Jacob Zuma sehemu zake za siri, jambo ambalo limepingwa vikali na serikali ya Afrika ya Kusini.
Kuchorwa huku kwa rais Jacob Zuma kumekuja baada ya siku za nyuma baada ya msaani mmoja kuandaa maonyesho ya sanaa za uchoraji ambapo zilikuwepo picha za zinazo onyesha sehemu za siri  za rais Jacob Zuma.

Jeshi la Iran la tangaza kugundua miali siraha.

Tehran, Iran - 07/07/2012. Jeshi la Iran limetangaza ya kuwa limetengeneza miali siraha ambayo inaweza kuongoza mitambo yake ya kivita.
Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia General Ahmad Vahidi akiongea na waandishi wa habari alsema " miaali siraha ambayo tumeitengeneza itatusaidia katika kutuongoza kujua adui yupo wapi,kuongoza katika kushambulia siraha ya angani na siraha za aina nyingine.
"Miali siraha hii ni ya kisasa na inauwezo mkubwa na kwa jina ni Dehlavieh na itasaidia katika kuimarisha ulinzi wetu.
Kitendo cha Iran kutangaza kugundua miali siraha hii kumekuja siku chache baada ya jeshi la nchi hii kufanya mazoezi ya kijeshi na kurusha makombora katika harakati za kujua uwezo wa jeshi na nguvu za jeshi hilo.  

Tumbaku bado haijafa thamani yake nchi Marekani.

Kentuck, Marekani - 07/07/2012. Ukulima wa zao la tumbaku umeongezeka nchi Marekani kufuatia mahitaji makubwa ya uvutaji wa sigara.
Katika mji wa Kentuck, wakulima wa mashamba hayo wamekuwa wakiongeza ukulima huo, baada ya faida kuonekana kutokana na mahitaji ya sigara kuongezeka katika bara la Afrika na  Asia.
Hata hivyo wakati mahitaji ya uvutaji wa sigara yakiongezeka katika nchi za Afrika na Asia, barani Ulaya na Marekani uvutajiwa wa sigara umekuwa ukipigwa vita na vyama, mashirika yasiyo ya kiserikali na serikali zenyewe ili kuweza kupunguza vifo vinavyo sababishwa na uvutajiwa wa sigara.

Walibya wapiga kura ya vyama vingi kwa mara ya kwanza.

Tripol, Libya - 07/07/2012. Wanachi wa Libya wamepiga kura kwa mara ya kwanza katika uchaguzi uliyo husisha vyama vingi tangu kuangushwa kwa utawala wa Muammar Gaddafi.
Zaidi ya watu million 2 walijiandikisha kupiga kura ili kuwachagua wabunge 200 ambao wata unda bunge ambalo litakuwa naserikali ambayo itachukua madaraka kutoka katika serikali ya mpito.
Walibya ambao wamepiga kura kuwachagua wabunge wao nakimekuwa ni kitendo ambacho hakijawahi kufanyika zaidi ya miaka 40 iliyo pita tangu Muaamar Gaddafi achukue madaraka.

Afghanistan kuwa mwanachama huria wa NATO.

Kabul, Afghanistan - 07/07/2012. Afghanistan inatarajiwa kuwa mwanachama huria wa nchi za NATO.
Maelezo hayo yalitokewa na waziri wa mambo ya nje ya nchi wa Marekani baada ya kukutana na rais wa Afghanistan.
Hillary Clinton akiongea na waandishi wa habari alisema " uamuzi wa kuikaribisha Afghanistani katika NATO ni moja ya majukumu ya kudumisha uhusiano wa muda mrefu ambao utasaidia katika kujenga serikali ya mpito kuelekea kujenga demokrasi ya kweli na serikali imara ya  Waafghanistan."
Maelezo hayo ya waziri wa mabo ya nje wa Marekani Bi Hillary Clinton yamekuja wakati Marekani na washiriki wake katika NATO wakiwa katika harakati za kuondoz majeshi yao nchi Afghaniztani ifikapo mwaka 2014.
Nchi nyingine ambazo ni wanachama huria wa  NATO ni Pakistan, Izrael, Misri, Japan, Jodan, Korea ya Kusini, Australia na New Zealand

No comments: