Thursday, July 5, 2012

Urusi yakanusha kuwa rais wa Syria kuchukua ukibizi.

Ligi kuu ya Uingereza kuanza kutumia teknolojia ya goli line.

London, Uingereza - 05/07/2012. Shirikisho la Soka Duaniani FFA limekubaliana kwa pamoja yakuwa teknolojia inayo julikana kama Hawk eye ya kutumia mtandao katika kuhakikisha mpira umevuka mstari wa goli inatumika.
 Kufuatia uamuzi huo wa FIFA, chama cha mpira nchi Uingereza kimeamua kuanzia msimu wa ligi wa mwaka 2012/13 teknologia hiyo itaanza kutumika.
Uamuzi wa kutumia teknolojia hiyo umekuja baada yamechi kati ya Uingereza na Ukraine kuleta matata ya umuzi wakati Ukraine ilipo pata goli lakini waamuzi wa mechi hiyo hawakona kama goli lilikuwa limeingia.

Urusi yakanusha kuwa rais wa Syria kuchukua ukibizi.

Moscow, Urusi - 05/07/2012. Serikali ya Urusi imekanusha uvumi iliyokuwa umevuma ya kuwa rais wa Syria  Bashar al Assad anampango wa kuchukua ukimbizi nchini humo.
Waziri wa mambo y kigeni wa Urusi Sergei Lavrov alisema " hakuna kitu kama hicho na wanaovumisha habari hizo wana njama zao binafsi na inaelekea wanaupungufu wa uelewa wa hali halisi."
Uvumi huo ya kuwa Urusi inampango wa kumpa rais wa Syria ukimbizi umekuja baada ya China na Urusi kuwa kinara katika kutetea serikali ya rais Bashar al - Assad ambayo inapingwa na nchi za Ulaya Magharibi na Marekani.

Wikileaks yachapisha habari za siri za Syria na washiriki wake.

London, Uingereza - 05/07/2012. Wikileaks imetoa mafaili yenye habari za nchi ya Syria na jinsi ilivyo jihusisha na nchi nyingine kisiasa, kiuchumi na kibiashara tangu mwaka 2006 hadi 2012.
Msemaji wa Wikileaks Sarah Harrison akiwakilisha maelezo ya Julian Assange aliseme " maelezo yaliyopo kwenye mafaili hayo yataleta aibu kwa serikali ya Syria na wale wanaojiita wapinzani wa Syria.
"Na itasaidia kuelewe ni kwa kiasi gani ukweli uliyopo na  ni kwanini vita vimetokea nchi Syria.
Wikileaks imelipa jina tukio hil kama " The Syria Files" na kudai ya kuwa kuna mafaili  zaidi ambayo yatafuta ikiwa ni mpango wake wakuchapisha habari hizo ambao ulianza 2010.

No comments: