Tuesday, July 3, 2012

Rais wa Syria hatuta jenga huhasama na Uturuki kamwe.

Iran yazidi kujimarisha kijeshi.

Tehran, Iran - 03/07/2012. Jeshi la mapinduzi la Iran lmeanza mazoezi yake ya kijeshi siku chache kabla ya kuanza rasmi ka vikwazo kwa mafuta ya Iran katika nchi za jumuiya ya nchi za Ulaya.
Katika mzoezzi hayo jeshi la Iran limejaribu siraha zinazo julikana kam ShababMeteor) 1,2,3, Khalij Fars (Persian Gulf), Tondar(Lightning), Fateh (Victor),  Zelzal (Quake) na Qiam(Uprising).
Mazoezi hayo yaklijeshi ya Iran, yanafuati yale yaliyofanywa  mwezi wa Februari ambayo yalijlikana kama Val Farj.
Iran imekuwa ikivutana na nchi za Ulaya gharibi na Marekani kuhusu mradi wake wa kuendeleza nguvu za kinyuklia jambo ambalo hadi sasa halijapagtiwa ufumbuzi.

Kashfa zasabisha mkuu wa beni ya Barclays kujiudhulu uongozi wake.

London, Uingereza - 03/07/2012. Mkuu wa benki kubwa ya tatu nchi Uingereza Barclays, amejiudhulu uongozi wake kufuatia kashfa za benki hiyo kukiuka maadili ya kibenki.
Mkuu huyo Bob Diiamond imembidi ajiuzuru uongozi wake baada ya banki ya Barclays kukutwa na hatia ya kuwalipisha riba wateja wake kinyume na maadili ya kibenki jambo ambalo limeleta msituko mkubwa katika jamiii nzima ya mfumo wa benki unavyo endeshwa nchini Uingeereza.
Kujiudhulu huko kwa mkuu huyo waa benki kumekuja bada ya waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kusema" nitaunda tume kupitia bunge ili kuchunguza uarifi huu uliyo tokea katika benki, kwa watu wanataka kujua ukweli na lazima tujifunze hali hi isije klutokea tena."

Rais wa Syria hatuta jenga huhasama na Uturuki kamwe.

Damascus, Syria - 03/07/2012. Rais wa Syria amesikitishwa na kitendo cha kuangushwa ndege ya jeshi la Uturuki wakati ilipo ingia anga za Syria.
Rais Bashar Al Assad alisema " tulijua ni ndege ya Uturuki baada ya kuiangusha, na naomba nieleweke kama tungejua ni ndege ya kijeshi ya Uturuki tusinge iangusha kamwe.
"Na hatutaruhusu uhasama kujengeka kati yetu na Uturuki kwani watu wapande zote mbili wataathirika kijamii na kiuchumi, na sisi hatutaweka jeshi letu karibu na mpaka na Uturuki japo serikali ya waziri mkuu Tayyip Erdogan imeweka jeshi lake mpakani na Syria."
Kuongea kwa rais Bashar al Asssad, kuhusu kuangushwa kwa ndege ya kijeshi ya Uturuki, huku hali kati ya nchi hizo mbili zikiwa katika utata.


Kampuni ya madawa ya Uingereza yapigwa faini.

Massachusetts, Marekani - 03/07/2012. Kampuni ya madawa ya Uingereza imepigwa faini baada ya kujulikana  kuepuka kwa makusudi kutoa maelezo ya dawa zake kwa watumiaji nchini Mareakani.
GlaxoSmithKline, imekubali kulipa kiasa cha dola za Kimarekani $3billion, baada ya kukutwa  na hatia na mahakama iliyopo Massachusetts.
Mwanasheria mwandamizi  wa serikali James M Cole alisema " hatutakubali wala kuachia afya za watu kuchezewa au kufanyiwa mchezo wa kirushwa,na kuanzia sasa hii ni onyo kwa makampuni mengine ya madawa."
Faini hiyo imekuja baada ya dawa zilizo tolewa na GlaxoSmithKline kwa ajili ya watu waliochini ya miaka 18 na kutumiwa kwa wagonjwa waliozidi umri wa miaka 18.


No comments: