Sunday, July 8, 2012

George Bush ashiriki ujenzi wa Zahanati nchi Zambia

Roger Federer akata ndoto ya Waingereza.

London, Uingereza - 08/07/2012. Roger Federer amekata ndoto ya Waingereza baada ya kushinda kwa mara ya saba kombe la tenisi la Wimbledon kwa upande wa wanaume.
Roger Feder ameweka kibindoni makombe makubwa 17 (Grand Slam) na kuwa sawa na mchezaji maarufu wa mchezo huo Peter Sampras katika ushindi wa kombe la Wimbledon.
Ushindi huo wa Roger Federer alipata baada ya kumshinda Andy Murry kwa seti 4-6, 7-5, 6-4 jambo ambalo limezima ndoto ya wapenzi wa mchezo wa tenis nchi Uingereza ya kuwa huenda mwaka 2012 ungekuwa wao kwa mchezji  Mwingereza kushinda kombeli hili ambalo kwa mara ya mwisho mchezaji wa Uingereza alishinda mwaka 1936.

George Bush ashiriki ujenzi wa Zahanati nchi Zambia
Lusaka, Zambia- 08/07/2012. Aliyekuwa rais wa Marekani alifanya ziara nchi Zambia na  Botswana ili kuimarisha ufahamu wa ugonjwa wa saratani ( Kansa).
Akiwa nchi Zambia, George Bush, alishiriki katika ujenzi wa  zahanati itakayo toa matibabu ya ugonjwa wa kansa ( saratani) katika mji wa Kabwe na baadaye alizungumza na viongozi wa serikali na viongozi wa maswala ya afya ya Zambia.
George Bush ambaye alisha wahi kufanya ziara barani Afrika, amekuwa akitoa kipao mbele katka harakati za kupambana na magonjwa yanayo tisha ikiwemo ukimwi na malaria katika bara la Afrika tangu alipo kuwa rais wa Marekani na hadi sasa.

Jeshila Bosco Ntaganda lazidi kuteka miji nchi JM-Kongo.


Rutshuru, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo - 08/07/2012. Jeshi la upinzani wa serikali ya JD-Kongo limeteka nyara mjiwa Rutshuru uliyopo km 70 Kusini mwa mji wa Goma baada ya jeshi la serikali kuzidiwa nguvu.
Jeshi hilo la upinzani wa serikali ya Komgo linalo ongozwa na  Generali Bosco Ntaganda,lili chukuwa mji huo muhimu baada ya mapigano makali na jeshi la serikali na baadhi ya wanajeshi wake kukimbilia nchi Uganda.
Wakati huo huo mwanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa mataifa kutoka India aliuwawa katika harakati za jeshi laupinzani wa serikali lilipo fanya mashambuli katika mji wa Bunagana.

Rais wa Misri atengua uamuzi wa jeshi la Misri.

Kairo, Misri - 08/07/2012. Rais wa Misri ametengua uamuzi wa jeshi la nchi hiyo kwa kuamuru baraza la bunge la nchi hiyo kurudi bungeni mara moja na kuanza kazi yake ya bunge.
Rais Mohamed Musri alitoa mri hiyo kwa kuvunja amri ya koti kuu ya nchi yakuwa bunge  lazima lirudi kazini mpaka hapo uchguzi mpya utakapo fanyika.
Amri hiyo ya kuvunjwa kwa bunge nchi Mirsi ilitolewa na jeshi wakati lilipo kuwa limeshikilia madaraka baada ya kuangushwa kwa utawala wa rais Hosni Mubarak.
Kufuatia kuvunjwa kwa amri hiyo na rais Mohamed Musri, wakuu wa jeshi nchi Mosri wameitisha kikao cha dharula ili kujadili uamuzi huo wa rais. 

Rais wa Syria aishutumu Marekani.

Damascus, Syria - 08/07/2012. Rais wa Syria ameishutumu Marakani kwa kusababisha vurugu nchi Syria ambazo zinaleta myumbo wa kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Rais Bashar al Assad akiongea  alisema " Marekani kwa kusaidiana na Katar na Saudi Arabia wana saidia magaidi  ambao ndiyo chanzo cha vurugu nchini Syria.
" Pia majirani zetu Uturuki wanawapa magaidi hawa waliopo Syria kila msaada wanao uhitaji, na kama hali hii ikiendelea basi magaidi watakuwepo na wapo tayari kushirikiana na Marekani.
"Tumekamata wapiganaji wengiwa kundi la Al Qaeda waliotokea nchini Tunisia na Libya na Marakani inahusika pia katika mauaji ya raia wa Syria."
Wakati huohuo jeshi la Syria limeaanza mazoezi ya kijeshi ili kujua kwa kiasi gani jeshi la nchi hiyo lipo tayari  ikiwa vita vikubwa  vitaanza katika nchi hiyo.

1 comment:

Anonymous said...

The firm strange affairs Citizens committee of the U.
S. Congress narrowly voted insist on Lettered the Clandestine convention?
Tagging process kit and caboodle on simple Method acting that involves
of beginning. Advocates of clearer Labels too level to
GET your message more easily. The manufacturers want to that they
can take the outset stairs in reduction exercising weight simply by getting enlightened.


Also visit my blog - custom letterhead printing