Uispania yaweka rekodi kwenye mchezo wa soka barani Ulaya.
Kiev, Ukraine - 01/07/2012. Uispania imeshinda kwa mara ya tatu mfululizo ubingwa wa kombe la nchi za Ulaya baada ya kuifunga Itali magoli 4 bila.
Ushindi huo ulikuja baada ya wachezaji wa timu ya Uispania David Silva, Jordi Alba Fernando Torres na Juan Mata kufunga magoli ambayo yalizamisha matumaini ya Itali kuwa mabigwa.
Kocha mkuu wa Itali Cesare Pandelli akiongea baada ya mechi kuisha alisema "tumekunaa na timu yenye kustaili kushinda mechi hii."
Uispaania imekuwa nchi ya kwanza kihistoria kufunga magoli manne katika fainali ya kombe la Ulaya.
Watu wauwawa kanisani nchini Kenya
Geissa, Kenya 01/07/2012. Watu 17 wamepoteza maisha yao baada ya kushabuliwa wakati wakiwa kanisani.
Mashahidi walitoa habari kwa kusema " miili ya watu walio poteza maisha kutokana na mshambuliz hayo ilikutwa ndani ya kanisa na ndani ya kanisa kulikuwa kumetapakaa damu."
Mashambulizi hayo yalitokea katika kanisa wakati watu hao walikuwa wakisali baada ya watu wenye siraha kuingia kanisani humo huku wakiwa wamejifunika nyuso zao na kufanya mashambulizi ambayo yaameleta mshutuko mkuu katika eneo hilo la Gerissa lililopo mpakani na Somalia.
Mashambulizi ya kigaidi nchi Kenya yamekuwa yakitokea tangu serikali ya Kenya ilipoanzisha kampeni ya kupambana na wapiganji wa kundi la Al - Shabab la Somali na kundi hilo kushukiwa kuhusika na mashambulizi yanayo tokea nchini Kenya.
Mpango wa Kofi Annan juu ya Syria wakubalika.
Kofi Annan, ambaye anasimamia upatikanaji wa amani nchi Syria alisema " wakati umefika sasa wa kushirikiana na serikali ya Syria inatakiwa iwajumuishe wapinzani wake katika kuongoza serikali."
Mkutano huo ambao uliudhurriwa na viongozi wa Urusi, Marekani, Uingereza China na wajumbe wa jumuiya ya Ulaya walikubaliana kwa pamoja ya kuwa ufumbuzi wa tatizo la kisiasa nchini Syria ni kuhakikisha ya kuwa serikali ya mpito inaundwa ili kusimamisha vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vinaendelea kwa sasa.
No comments:
Post a Comment