Wednesday, July 25, 2012

Wananchi Ghana waanza maombelezi baada ya kifo cha rais.

Wananchi  Ghana waanza maombelezi baada ya kifo cha rais.


Akkra, Ghana - 25/07/2012. Wananchi na wakazi waishio nchi Ghana, wameanza maombelezi bada ya rais wa nchi hiyo kufariki baada ya kuugua kwa  muda fupi.
Hayati rais John Atta Mills 68 ambaye alichaguliwa kuwa rais wa Ghana kwa kumshinda mpinzani wake Nana Akufo-Addo kwa kiasi kidogo cha kura mwaka 2008.
Kufuatia kifo cha rais Attap-Mill, makamu wake wa urais John Dramani Mahama ameapishwa kuwa rais wa Ghana kuanzia sasa mpaka hapo uchaguzi wa rais mpya utakapo anza mwisho wa mwaka huu.

Kesi zidi ya makamu wa rais wa Irak yaharishwa.

Baghdad, Irak 25/07/2012. Kesi inayo mkabili makamu wa rais wa Irak na ambaye yupo ukimbizi nchi Uturuki imeharishwa.
Kesi hiyo ambayo inamkabili aliyekuwa makamu wa rais  Tariq al-Hashimi ilihairishwa baaada ya rais wa Irak Jalala Talabani kukataliwa kutoa ushahidi mbele ya mahakama.
Makamu wa rais Hashimi anakabiliwa na kesi ya kuhusika katika mauaji na mateso ambayo amekanusha.

Nchi zajumuiya ya  Ulaya hakuna mafikiano juu ya Hezbollah

Brussels, Ubeligiji - 25/07/2012. Jumuiya ya nchi za Ulaya imelikataa ombi la Izrael la kutak kundi la Hezbollah llilipo Lebanoni kuingizwa katika makundi yanayo husika na ugaidi.
Waziri wa mambo ya nje ya nchi wa Cyprus Erato Kozakou-Marcoullis ambaye nchi yake ndiyo inayoshikilia urais wa nchi za jumiya ya ulaya alisema "kwa sasa hakuna makubaliano ya kuliunganisha kundi la Hezbollah kama kundi la kigaidi."
Waziri Kozakou-Marcoullis aliyasema hayo baada ya Izrael kuzitaka nchi za jumuiya ya Ulaya kuliunganisha kundi la Hezbollah kuwa moja ya makundi ya kigaidi.
Izrael imeilaumu kundi la Hezbollah kwa kuhusika na bomu lililo lipuliwa nchini Bulgaria na kusabababisha vifo vya raia wa Izrael na wengine kujeruhiwa wakati wakiwa matembezini nchi humo.

1 comment:

Anonymous said...

zama topic za bongomovie tunapata wap.nina maoni