Tuesday, July 3, 2012

Uchunguzi wa kifo cha Yasir Arafat watoa majibu nusu.

Uchunguzi wa kifo cha Yasir Arafat watoa majibu nusu.

Paris, Ufaransa - 03/07/2012. Uchunguzi wa kisayansi uliyofanywa kuhusu kifo cha aliyekuwa kiongozi na rais wa Wapalestina umetoa majibu nusu tangu kuanza kwa uchunguzi huo.
Rais Yasir Arafat ambaye alifariki dunia nchini Ufaransa ambapo alipelekwa kwa ajili yamatibabu baada ya kuugua wakati akiwa amefungiwa  kutoka katika mji wa Ramallah na serikali Izrael.
Dr Francois Bochud ambaye ni mtaalamu wa Radiophysique iliyopo nchini Switzerland alisema " naweza kusema tumekuta aina ya gesi inayo julikana kama polonium-210 ambayo inaweza kuwa chanzo ca kifo chake na tunaweza kupata jibu sahihi ikiwa baadhi ya viungo vya marehemu Yasir Arafat vitapatikana kwa  uchunguzi zaidi."
Uchunguzi wa kifo cha Yasir Arafat ulikuja baada ya mkewe Suha Arafat  kuruhusu uchunguzi kuendelea na kutoa ruhusa ya kuwa mwili wa Yasir Araf ufukuliwe kwa uchunguzi zaidi  na kuiomba serikali ya Wapalestina kushirikiana naye.

Iran yadia kupata ufahamu wa ndege ya Marekani waliyo iteka.

Tehran, Iran - 07/03/2012.  Jeshi la Iran limedai ya kuwa limepata uwezo wa kuisoma ndege inayo endeshwa kwa kutumia mtandao (Drone) ambao utasaidi jeshi hilo kiutaalamu.
Brigadia Generali Amir -Ali Hajizadeh aliema " ndege ya Marekani RQ - 170 ambayo tumeikamata itasaidia saana kwani tulicopata ni kitu ambacho maadui zatu hawakuta tukijue."
Maelezo hayo ya mkuu huyo wa jeshi la Iran yamekuja wakati jeshi la nchi hiyo likuwa katika mazoezi ya kijeshi ambayo yameanza hivi karibuni.

Ofisi na nyumba za Nikolas Sarkozy za vamiwa na polisi.

Paris, Ufaransa - 03/07/2012. Ofisi na nyumba anayoishi aliyekuwa rais wa Ufaransa Nikolas Sarkozy zimevamiwa na polisi katika haraki za kufanya uchunguzi zidi ya rais huyo wakati wa kampeni za uchaguzi.
Polisi hao ambao waliaandamana na wapelelezi waiiingia katika ofisi hizo na nyumbani kwa rais huyo na kuchukua baadhi ya mafaili na vitu vingine ambavyo vinashukiwa kuhusika katika uchunguzi huo.
Hata hivyo Nikolas Sarkozy amekanusha kuhusuka na tuhuma hizo na wala hakuhusika.
Uchnguzi huo umekuja ikiwa ni katika harakati za kutafuta ukweli kama kuna kitendo cha rushwa kilitendeka wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2007.


No comments: