Friday, July 13, 2012

Venezuela yapelek mafuta nchi Syria.

Venezuela yapelek mafuta nchi Syria.


Karakas, Venezuela - 13/07/2012.  Serikali ya Venezeula imepeleka mafuta nchini Syria kufuatia viwazo vilivyo wekewa nchi hiyo.
Uamuzi wa serikali ya Venezuela kupeleka mafuta nchini humo umekuja kutokana na uhusiano uliyopo kati ya nchi hizo mbili.
Habari kutoka serikali ya  Venezuela zinasema  "mafuta yatazidi kupelekwa nchini Syri kma kawaida."
Serikali Venezuela imetumia meli zake za kusafirisha mafuta kufuatia mashirika ya meli na bima za nchi za Ulaya na Marekani kukataa kuzidhamini meli za mafuta zinazo peleka mafuta nchi Syria baada ya vikwazo kuwekwa kwa serikali ya rais Bashar al Assad.

Ruksa kutailiwa kufuatia imani za dini nchini Ujerumani.

Berlin, Ujerumani - 13/07/2012.  Kansela wa Ujerumani ameunga mkono jamii za Kiyaudi na za Kiislaamu zinazo taka kitendo cha kutahiriwa kiendelee katika jamii zao.
Mseamji wa Kansela Angela Merkel, Steffen Seibert alisema " kutailiwa kwa watoto wa kiume ni kitendo ambacho kinakwenda sambamba na imani ya dini hizo na hakuna adhabu itakayo tolewa.
"Na ieleweke serikali inaruhusu haki ya kiimani na Wayahudi na Waislaam ni Wajeruamani hivyo wanahaki sawa na Wajerumani wangine."
Kuungwa mkuno huko kwa kitendo cha kutailiwa kumekuja baaada ya dakitari mmoja kutokutwa na hatia ya kusababisha maumvu kwa mtoto aliye mtairi, ambapo idaiwa mtoto huyo alikutwa na matatizo ya kiafya kutokana kutailiwa huko.
Hata hivyo kitendo cha kutailiwa kimekuwa kinaleta mvutano katika jamii nchi Ujerumani huku wengine wakipinga na wengine wakiunga mkono.

Marekani yaongeza nguvu za kijeshi kanda za Ghuba

Washington, Marekani - 13/07/2012.  Serikali ya Marekani kimeongezea siraha na nguvu za kijeshi katika nchi zenye makao yake ya kijeshi zilizopo katika nchi za Ghuba.
Kwa mujibu wa habari zilizo tolewa zinasema " uamuzi wa serikali ya Marekani kuogeza nguvu zake za kijeshi katika eneo hilo jimekuja katika harakati za kutaka kuizuia Iran isiweze kuzuia ghuba ya Hormuz kama ilivyo tangaza hapo awali."
Iran ambayo imewekewa vikwazo na Marekani na nchi washiriki wake ilitangaza hapo awali yakuwa itafunga njia ya Hormuz ambayo inatumika kusafirisha mafuta kutoka katika nchi zilizopo maeneo hayo.

1 comment:

'Zmail said...

This is a well made photo. I am a pro photographer and I salute your talent. My photo blog is alveraphoto.blogspot.com. Enjoy and have a nice day!