Saturday, July 21, 2012

Mkuu wa polisi wa Afrika ya Kusini kutolewa jela.

Mkuu wa polisi wa Afrika ya Kusini kutolewa jela.


Johannesburg, Africa ya Kusini - 21/07/2012. Aliyeuwa mkuu wa polisi nchini Afrika ya Kusini na ambaye anatumikia kifungo, anatarajiwa kutolewa hivi karibuni kutoka jela.

Waziri wa magereza wa Afrika ya Kusini Sibusiso Ndebele alisema "Jack Selebi ataachiwa kutaokana na kuwa na matatizo ya figo na mtatizo mengine ya kiafya.
Jackie Selebi 62 alihukumiwa kwenda jela baada ya kukutwa na hatia ya kuopea rushwa mwaka 2010 nakuhumiwa kifungo cha jela miaka 15.
Mahakama ya kimataifa yataka rais wa zamani wa Chad akamatwe.

Brussells, Ubeligiji -21/07/2012. Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia makosa ya ukiukwaji wahaki za binadamu ya Ubeligiji, imetaka aliyekuwa rais wa Chad akamatwe ili ajibu mashitaka ya kukiuka haki za binadamu.
Hissene Habre ambaye alikuwa rais waChad, anashitakiwa kwa makosa ya kukiuka haki za binadamu wakati wa utawala wake katika ya miaka ya 1982 - 1990.
Kesi zidi ya Hissene Hebre ilifunguliwa na raia wa Ubeligiji mwenye asili ya Chad kwa madai ya kuwa wakati wa utawala wa  Hissene Hebre watu wapatao 40,000 waliteswa na hata wengine kupoteza maisha.
Hissene Hebre yupo ukimbizini nchi Senegal ambako alikimbilia baada ya utawala wake kuondolewa.
Izrael ya ombeleza vifo vya watu walo fariki na mlipuko wa basi

Burgas, Bulgaria - 21/07/2012. Polisi nchini Bulgaria bado wanatafuta muhusika katika tukio la kulipua basi lililo kuwa limewabeba abiria wa Kiizrael.
Akiongea na waandishi wa habari, waziri wa mambo ya ndani wa  Bulgaria Tsvetan Tsvetanov alisema "hadi sasa tumetambua ya kuwa aliyelipua basi hakuwa raia wa Kibulgaria na uchunguzi bado unaendelea."
Jiji la Burgas lilikumbwa na mshituko mkubwa baada ya basi lililo beba abiria wa Kiizrael kulipuka na kusababisha vifo na majeruhi walokuwa katika matembezi jiji humo.
Kufuatia mlipuko huo serikali ya Izrael imezilaumu Iran na washiki wake kwa kuhusika na mlipuko huo, jambo ambalo Iran imekanusha.

1 comment:

commpi tubruk said...

Nice posting.
Visit http://eka-ebong.blogspot.com
Ok mister