Friday, December 28, 2007

Bi, Benazir Bhutto, aaga dunia kwa imani aliyokuwa akiitetea

Bi, Benazir Bhutto,aaga dunia kwa imani aliyokuwa akiitetea.

Rawalpindi, Pakistan - Aliyekuwa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan na kiongozi wa chama cha (PPP) Pakistani Peoples Party, bi Benazir Bhutto, amefariki dunia tarehe 27/12/07, kutokana na majeraha ya risasi yaliyo mpata kwenye shingo na begani.
Tukio hili lilitoke wakati bi, Bhutto alipo maliza kuhutubia mkutano wakampeni ya uchaguzim kwenye mji wa Rawalpindi.
Inaaminika bi, Bhutto alikumbwa na janga hili, baada ya mlipuko mkubwa wa bomu kutokea karibu na gari yake aliyokuwemo ndani, nandipo mjitolea muhanga mmoja alipo fyatua risasi na kumpiga bi Bhutto, na yeye mjitolea muhanga kujiua kwa kujilipua na bomu.
Bi, Bhutto alikimbizwa hospitali, lakini titihada za madakitari kuokoa maisha yake hazikifanikiwa.Bi, Bhutto alikuwa kiongozi wa upinzani ambaye alikuwa anatarajiwa yeye na chama chake kushinda kwenye uchaguzi utakaofanyika mapema januari, picha nyingine anaonekan bi, Bhutto akishuka ngazi kutoka jukwaani baada ya kumaliza mkutano
Pichani anaonekana bi,Benazir Bhutto akiwaaga wapenzi na wanachama wake baadaya kumaliza kampeni za uchaguzi.
Hapo kati anaonekana bi, Bhutto akiwa na Malkia Elizabeth wa Uingereza, alipombelea Malkia wakati akiwa kama waziri mkuu wa Pakistani.
Pichani ni Wapenzi na Wanachama wakilia kwa uchungu baada ya kupata habari ya kuwa bi Bhutto ametutoka.
Pichani linaonekana jeneza la bi, Bhutto likipokelewa kutoka hospitali tayari kwa kuelekea nyumbani kwao kwa mazishi.Mola aiweke roho yake peponi "Amin."
Uchaguzi nchini Kenya,demokrasi yatafutwa kwa kila njia."Mungu Ibariki Afrika"
Nairobi, Kenya - Harakati za uchaguzi nchini Kenya zimefika tamati huku wagombea wote wa vyama vilivyo shiriki vikiwa na matumaini makubwa ya kushinda.
Hata hivyo hali ya viti ya ubunge vimekuwa na mageuzi makubwa, kwani kwa asilimia kubwa ,wale wote waliokuwa wapo kwenye serikali ya rais Kibaki wameshindwa kupita tena, na hii ina ashiria ya kuwa hata kama rais Kibaki ata shinda kiti cha urais, basi atakuwa nawakati mgumu kimaamuzi.
Kutokana na wachunguzi wa mambo ya kisiasa, wansema ya kuwa uchaguzi wa Kenya umekuwa na vitisho vingi na vurugu za kila namna kutoka kambi zote za upinzani, nahata kufikia baadhi ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa.
Hadi sasa bado kura zinahesabiwa na wanchi wa Kenya wanasubiri kwa hamu kuona kama kura zao zimelenga walipo chagua.
Pichani anaonekana bwana Laira Oginda, akiwa na wanachama wenzake kuelekea kwenye kampeni za uchaguzi.
Chini inaonyesha jinsi gani, uchaguzi nchini Kenya unavyokuwa wa hatari, mpaka mapanga huhusishwa katika uchaguzi.
Pichani anaonekana mama Yoyo akipiga kura yake, je safari hii watakumbukwa?
Picha chini anaonekana bwana Mwai Kibaki akimsalimia mmoja ya wazee wakati wa kampeni.
Kitendawili cha mafuta, bado kupatiwa jibu na rais mpya wa Nigeria.
Lagos, Nigeria - Kulikuwa na mshtuko mkubwa ndani ya jiji la Lagos, baada ya moto mkubwa ukiambatana na moshi mzito na mweusi, huku kelele za watu zikisikika, karibu na bomba moja la kupitishia mafuta ya aina ya petrol,haya ni maneno ya mmoja ya watu walioshudia tukio hili.
Mlipuko huu ulio chukua upna wa mita zipazo nusu uwanjwa wa mpira, ulijeruhi watu wengi nawengine kupoteza maisha yao baada ya kuungua vibaya na moto huu.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, watu hawa walio ungua na kufariki dunia walikuwa wana chukua mafuta kutoka kwenye bomba hilo, amablo linasadikiwa lilitobolewa kwa makusudi.
Hata hivyo baadhi ya watu walisikika wakisema, hii inatokana na ukame na upungufu wa bidhaa hii,amabyo nchi yao no ya saba dunia katika utoaji wa bidha hii ( mafuta).
Hili sio tukio la kwanza, kwani Wanchi wa Nigeria wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na matukio haya ya kuchukua mafuta kutoka kwenye mabomba yaliyo toboka.
Pichani juu wanaonekana polisi wakiangali magalono amabyo hutumiwa kichukulia mafuta haya,picha nyingine anaonakana rais mstahafu wa Nigeria bwana Obasanjo akishuka kutoka kwenye gali, naambaye alimkabidhi kibarua kizito rais wa sasa wa Nigeria bwana Amuru Yar Adua ambaye picha yake ipo chini ya Obasanjo.
Picha ya mwisho inaonjesha moja ya mitaa, ambapo mafuta yanapo tokea au kuchimbwa, lakini hali ya wazawa bado kitendawili.
Wafaransa waota joto la jiwe la jela ya Afrika"Kazi ngumu Pilato asema"
Ndjamena, Chad - Serikali ya Chad imewahukumu wafaransa sita kwenda jela miaka nane na kazi ngumu , kwa kosa la kukutwa na hatia ya kutaka kusafirisha watoto kinyume cha sheria.
Hukumu hiyo ilitolewa siku ya jumatano zidi ya wafaransa hao, hata hivyo siku ya ijumaa serikali ya Ufaransa imeiomba serikali Chad ya kuwa wafaransa hao waruhusiwe kwenda kutumikia kifungo chao nchini Ufaransa.
Hata hivyo serikali ya Chad bado inafikiria ombi hilo.Tukio hilo la kutaka kusafirishwa kwa watoto hao lilileta mtafaruku mkubwa saana kati ya jamii ya Wafaransa na Wachad. Picha juu anaonekana rais wa Chad, bwana Idriss Deby akiongea na watoto alipo kwenda kuwatembelea.
Picha ya kati anaonekana Eric Breteau, mwanzilishi wa Merikebu ya NOA,akiwa na wafanyakazi wenzake ndani ya lupango nchini Chad.
Picha ya mwisho chini anaonekana mmoja wa watuhumiwa akielekea kwa Pilato kula kigungo.
Ebola kukung'utwa kabisa ifikapo 2008"Wizara ya Afya Uganda"
Kampala, Uganda - Serikali ya Uganda, iko katika hatua za mwisho kupmabana na ugonjwa wa Ebola.
Akiongea hivi karibuni kwa niaba ya wizara ya Afya, bwana Sam Okware, alisema ya kuwa idadi ya watu wenye kukumbwa na virusi hivi, imepungua hasa kwenye maeneo amabyo yalikuwa yamekumbwa na ugonjwa huu.
Hadi hivi sasa hatujapata habari za kifo kuhusiana na ugonjwa huu, bado tunachunguza kwa makini kujua kama kweli tumefanikiwa kukabiliana na ugonjwa huu, hivyo hadi kufikia januari 12, tutapata huhakika kamili , alimalizia kwa kusema haya.
Picha juu ni bendera ya Uganda yenye ngede mzuri, na picha nyingine inaonyesha mandhari ya milima iliyopo sehemu ambazo zilivamiwa na ugonjwa ebola, na wanao taabika hasa ni watoto amabo wanonekana wakingojea jebu kwa kinga.

No comments: