Sunday, December 2, 2007

Hatuwezi kutoka, hali siyo nzuri kiusalama, Serikali ya Ethiopia.

Wana nyota na wasanii, huwa na furaha wakitarajiwa kuwa wazazi.

Hollywood,Amerika - Katika harakati za kurajiwa kuwa wazazi, wanamitindo, wananyota, wakimuziki, sinema wa dunia hasa waishio Hollwood,huwa na raha hasa ikifikia kipindi cha kukaribia kuitwa baba au mama.
Hivi karibuni, mmoja ya wananyota wa kisanii duniani Christine Aguilera, alipiga picha kuonyesha jinsi gani mimba yake anavyo hifurahia, na kutarajia kuwa mama.
Akiongea, mmoja ya wasemaji wa bi Christine, alisema ya kuwa kila wakati msanii huyu hujihisi raha anapo shika tumbo lake.
Pichani anaonekana bi Christine, akiwa amepiga picha, kuonyesha tumbo lake jinsi lilivyo, na picha nyingine akiwa amevalia mavazi ya kiujauzito.
Kucheza mpira ugenini si kigezo cha kushindwa kuwakilisha taifa langu.
London,Uingereza - Mwana soka maarufu na kepteini wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza David Beckham, amesema yakuwa kucheza kwake mpira nchini Amerika, akutamzuia kuichezea nchi yake ikiwa ahitajika.
Beckham, aliyasema haya, alipo kuwa akiongea na mmoja ya wandishi wa habari, wakati wa kuangalia mradi wake wa kuinua vipaji vya wanasoka wajao nchini Uingereza.
Beckham, alisisitiza ya kuwa atakuwa anajiweka fiti kimpira, mpaka hapo wakati mwili utakapo kataa msukusuko.
Hopo juu anaonekana David Beckham, akijiandaa kuingia uwanjani kuisaidi, timu yake ya taifa, wakati wa mpambano na Kroatia.
Kuvunjika kwa makubaliano, Chavez afunga Ubalozi.
Bogota, Kolombia - Rais wa Venezuela, bwana Hugu Chavez, amekatisha mahusiaano ya kidiplomasia na serikali ya Kolombia kwa kumwita nyumbani balozi wa Venezuela aliyekuwepo nchini Kolombia.
Hali ya kutokuelewana kwa nchi hizi mbili, kumekuja baada ya serikali ya Kolombia, kuvunja makubaliano yaliyokuwepo hapo awali, yakuwa rais Chavez angesaidia kuachiliwa kwa mateka waliokamatwa na wapinzani wa serikali ya Kolombia naangekuwa msuruhishi wa wa ugomvi uliopo kati ya serikali ya Bogota na serikali ya rais Chavez.
Kufuatia hailia hii, wapinzani wa serikali ya Kolombia, walisema kuvunjika kwa mkataba huu, ndiyo ulikuwa chanzo cha matumaini ya kuachiwa mateka waliochini ya himaya yao.
Pichani hapo juu, ni picha ya rais Hugo Chavez, akionyesha ishara ya ushindi.Picha nyingine chini ni picha za mateka ambao bado hali zao hazijulikani mpaka sasa.
Hawakuja kuleta amani, bali wapo kwa manufaa yao "Wapinzani".
Darfur, Sudani - Wapinzani wa serikali ya Sudani, wamewataka wanajeshi wa Kichina wapatao 135 kuondoka nchini Sudani.
Kundi hilo la wanajeshi mafundi kutokea nchini China, kujiunga katika harakati za kuleta amani nchni Sudani.
Lakini msemaji wa wapinzani wa serikali ya Sudani, alisema jechi la China halina nia ya kuleta amani, bali wapo nchini Sudani kwaajili ya kwa kutaka kuchukua mali na kulinda maslai yao. Msemaji huyu wa wapinzani, aliagizia serikali ya China kuacha kuisaidia serikali ya Sudani.
Pichani wanaonekana wanajesi wa China wakiingia ndani ya ndege, tayari kuelekea Darfur.
Imani ya dini yoyote si ya kuchezea, Mwingereza aonja joto ya jiwe.
Karthoum, Sudani- Mwalimu mmoja bi Gillian Gibbons mwenye miaka 54, ambaye alikuwa anafundisha shule moja, nchini Sudani, amkutwa na kosa kwa kuita tokoroshi, jina Muhammad.
Kuokana na kosa hilo, bi Gillian, amehukumia kwenda jela kwa muda wa siku 15, na baada ya kumaliza adhabu hii atarudishwa kwao Uingereza.
Kuhukumiwa kwa bi Gillian Gibbons, kumeleta kwa kiasi fulani utata wa kidiplomasia kati ya serikali ya Uingereza na serikali ya Sudani.
Pichani ni picha za maaskari wakiwazuia waandishi wa habari, kuingia kotini ili kusikia hukumu ya bi Gillians Gibbons, na picha ya chini yake ni pcha ya bi, Gilliana Gibbons.
Hatuwezi kutoka, hali siyo nzuri kiusamala,"Serikali ya Ethiopia"
Adis Ababa, Ethiopia - Waziri mkuu wa Ethiopia, Meles Zanawi, amekubali ya kuwa itakuwa vigumu kwa jeshi la Ethiopia kujitoa kwenye mgogoro wa Somalia.
Akiongea, waziri Zanawi, alisema ya kuwa alitarajia kuyatoa majeshi ya Ethiopia mwishoni mwaka, lakini kutokana na hali ilivyo sasa nchini Somalia itakuwa ni vigumu, kwani kundi la Waislamu wenye siasa kali bado kungolewa na jeshi la kulinda amani bado kuwasili.
Waziri Zanawi,aliongeza kwa kusema ya kuwa pia kutokuwepo na serikali ya kudumu chini Somalia,kumemfanya aangalie upya hali hii.
Pichani hapo juu, wananekana wanajeshi wa Ethiopia wakiwa wanakula doria miaatani Mogadishu.
Nchi wanachama za Afrika ya mashariki kufaidika kibiashara na mikataba mipya?
Arusha,Tanzania - Nchi wana chama shirikisho la Afrika ya mashariki,(EAC) East Africa Communite, zimekubalina kimsingi kufanya biashara na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya ( EU) European Union.
Nchi hizo za shirikosho Afrika ya Mashariki, ambazo ni Burundi, Rwanda, Tanzania, Uganda na Kenya, zimetiliana mkataba huu na Umoja wa Ulaya ili kubadulisha uli mkataba wa mwanzo amabo unakabila kuisha mwisho wa mwezi wa desemba.
Makubaliano haya ua EU na EAC,bado yanatizamwa kiundani na nchi nyingine za Afrika ya magharibi, karibiani na Pasifiki.
Wasemaji wa mashirikisho haya, wamesema mkataba huu utazipa nafasi bidhaa za pande zote mbili kuuzwa bila vipingamizi.
Hapo juu, wanaonekana wafanyakazi wa moja ya nchi wanachama wa Afrika ya mashariki wa kiwa katika uzalisaji wa bidha zao, ambazo muda huenda zikaanza kuuzwa kwenye nchi za EU.
Magwanda basi kwa. Gen Musharaff, awa raia na tayari kuongoza nchi kama rais.
Karachi,Pakistani - Rais, Gen Pervez Musharaff, amejiudhuru rasmi kama mwanajeshi wa jeshi la Pakistani, baada ya kutumia jeshi la Pakistani, zaidi ya miongo ninne.
Gen, Musharaff, alisifia jeshi la Pakistani kwa kuwa, mtetezi, mkombozi, wa kudumisha demokrasi ambayo ni ilikuwa inafaa kwa wananchi wa Pakistani.
Katika hutuba hiyo ya kuaga jeshi, aliwaonya wale wote, ambao wataleta matata nchi hawataachiwa kufanya hivyo.
Gen,Musharaff, alisema ya kuwa kunawatu, amabo wamepotea, na hawajui umuhimu wa jeshi la Pakistani,na jinsi gani limejenga na kuendeleza nchi ya Pakistani.
Pichani hapo juu, anaonekana.Gen, Pervez Musharaf alipo kuwa akikagua gwaride la kumuaaga kama mwanajeshi, na picha nyingine, anaonekana Gen Musharaff,akipiga saluti kwa wanajeshi kwa mara ya mwisho kama kamanda wao mkuu.
Mwaenda kinyume na maadili ya vita,kiongozi wa Al-qaeda.
Mashariki ya Kati - Kiongozi wakundi la Al-qaeda, Osama Bin Laden,siku ya alkhamisi, ameoneka tena katika mitandao na luninga tofauti za duniani, kwa kusema ya kuwa jeshi la NATO, kuondoka nchini Afghanistani.
Bi Laden, aliendelea kusema ya kuwa, vita ya vinavyo endelea huku Afganistani, vinakiuka maadili ya vita.
Bin Laden, alisema ya vita hivi, vinaendeshwa kinyume, kwani mpaka sasa,NOTO wamekuwa wakiua na kushambulia maeneo ya ambayo, huleta maafa makubwa kwa watoto na wanawake.
Osama, alisisitiza inafikia hata kshambulia sehemu za sherehe, kwa kutumia jina la kupigana na kundi la Al quada, na hivyo nikinyume cha maadili ya vita, kwani wanawake na watoto, ina julkana wazi sio wapiganaji wa vita.
Kokana na msemaji wa vita dhidi ya Alqaeda, amesema ya kuwa, ujumbe huu, wa bwana Osama , unaashiria kitisho kwa jamii.
Pichani hapo juu, ni picha ya kiongozi wa kundi la Alqaeda, bwana Osama Bin Laden, alipokuwa anaonekana kwenye luninga na mitandao tofauti.

No comments: