Sunday, December 9, 2007

Imani ya dini, biblia, tafsili, na maana, bado kuelewaka ni nani ana haki.

Rambo II, ilikuwa na wakati mgumu kuiandaa, chupu chupuu.

Los Angeles,USA - Bingwa na mchezaji sinema za kikomando, Sylvester Stallone, ametoa siri hivi karibu ya kuwa wakati wa kucheza sinema ya RAMBO, alikuwa na wakati mgumu. "The Rambo" Sylvester Stallone, alisema wakati wana elekea kuanza kupiga sinema ya RAMBO, walionywa ya kuwa wawe waangalifu. Kwani wakati wowote wanaweza kuvamiwa au kukumbwa na vita vya wenye kwa wenyewe kati ya Myanmar ( Burma) na wapinzani wake. Na hasa wakati wanaendelea na kupiga sinema hii "RAMBO II" kulikuwa na mapinduzi ya serikali nchini Thailand, hii pia ilichangia ugumu wa kupigapicha ya sinema hii RAMBO II. Pichani anonekana "Rambo" akiwa kazini enzi hizo alipo kuwa na cheza picha ya the RAMBO II.
Imani ya dini, biblia, tafsili, na maana, bado kuelewaka ni nani ana haki.
California, Amerika - Mvutano wa jinsia na usawa hasa katika kumtumikia Baba Mungu,umekuwa unaleta mvutano na kuumiza vichwa vya waumini wa dini ya kikristu, hasa dhehebu la kiangrikana.
Hivi karibuni mjini California, kanisa limegawanyika kuhusu ni nani mwenye haki kuwa padri, anatakiwa awe mtu wa namna gani.
Swala la usenge limekuwa linatawala na kuumuza vichwa vya waumini wa mji wa California, hivi karibuni wameamua kutengena kati ya wale wanao kubali wasenge wawe mapadri na wasiopenda wasenge wawe mapadri.
Mvutano huu, ulianza mwaka 2003, baada ya asfoku msenge kupitishwa kuongoza kanisa. Pichani wanaonekana maaskofu wanao kubaliana kuwa kundi moja tofauti na wengine.
DRC yatoa onyo, LRA's na bwana, Joseph Kony kuregea kwa mkwara?
Kampala, Uganda - Serikali ya DRC, imemuagiza na kumpa onyo kiongozi wa LRA(Lord Resistance Army), bwana Joseph Kony mwezi mmoja kutoka huko mafichoni karibu na mbuga za Gamba.
Onyo hilo la mwezi linampa nafasi bwana Kony hadi 31 januari 2008.
Kipindi hii alicho pewa bwana Kony, kinakuja baada ya makubaliano yalio wekwa mjini Arusha semtemba 8.
Nguvu nyingine za msukumo huu,unakuja baada ya waziri wa mabo ya nje wa Amerika bi Condoleezza alipo kutana na mawaziri wa DRC, bwana Mbusa Nyamwisi waziri wa mabao ya nje ya DRC na waziri wa mambo ya ndani ya DRC bwana Denis Kalume. Pichani hapo juu ni bwana Joseph Kony enzi zake alipoanza kupamabana na serikali ya Uganda miongo miwili iliyopita. Picha nyingine wanaonekana wanajeshiwa DRC wakila doria kwenye mbuga katika harakati za kuweka mkwara kwa bwana Kony.
Chama kinacho tawala chatakiwa kutoa maelezo kwa chama pinzani" USA"
New York, Amerika - Serikali ya sasa iliyopo madarakani chini ya chama cha (Republican),imekubwa na wakati mgumu saana kutoka kwa wapinzani wa chama cha (Demokrasi) wanaotaka maelezo kwa nini mikanda ya video yenye picha zilirekodiwa wakati wa kuwahoji na watu wanaosadikiwa ni wanachama au washiriki wa Alqueda na wenzake, zili haribiwa na CIA.
Kuhaibiwa kwa mikanda hii, kunazidi kuleta maswali mengi,kwani inaaminika ya kuwa njia zilizo tumika katika kuwahoji watuhumiwa hawa zilikuwa za kutisha, na zingeharibu mambo mengi ya kiusalama.
Hata hivyo rais George Bush, amekuwa akikisisitiza ya kuwa, hawaruhusu ukatili kufanyika wakati wa mahojiano. Pichani ni alama ya CIA, amabyo wafanyakazi wake, wanawakati mgumu wa kujielezea mbele ya Waamerika kuhusu kuharibiwa kwa video.
Ripoti kuhusu Iran na nyuklia,bado kitendawili kwa Waisrael.
Tel Aviv, Israel - Viongozi wa serikali ya Israel, wamesikitishwa na ripoti iliyo tolewa na mashushu wa serikali ya Amerika kuhusu Iran na mpango wa kujenga bomu la nyuklia.
Msemaji wa serikali ya Israel alisema, katika ripoti hii, kuna ripoti ambazo ziliolewa na srikali ya Israel hazikujumuishwa.
Kutokana na ripoti hii, inaelekea ya kuwa mpango wa kuishabulia Iran, hasa kwenye maeneo ya viwanda vya nyuklia, una nafasi finyu.
Ripoti hii inakwenda kinyume na CIA ya Amerika na chombo cha usalama cha Waisrael "MOSSAD" ambazo zilisema Iran itakuwa na nguvu za bomu la nyuklia kufikia mwaka 2009.
Hata hivyo, kiongozi mmoja wazamani wa MOSSAD, bwana Ephraim Halevy, alisisitiza ya kuwa "Bado Iran ina uwezo wa kutengeneza siraha za nyuklia" Pichani ni moja ya maeneo yanayo sadikika ya kuwa ni kitovo cha sayansi ya nyuklia nchini Iran.
Pentagon, vichwa vya zidi kuuma, Urusi ya zidi kutunisha misuli.
Washington, Amerika - Mswada wa kujengwa makombora ya masafa,katika nchi za Poland na Jamuhuri ya Czech bado ni ktendawili hasa baada ya ripoti ya mashushu wa serikali ya Amerika, kusema ya kuwa Iran, ilisha acha mpango wake wa kutengeneza makombora yatakayo tumia nyuklia.
Msemaji mmoja wa Pentagon, aliongeza kwa kusema ya kuwa hali hii, imesababisha uhusiano ulipo kati ya serikali za Amerika na Urusi, kuwa katika hali tete,akiongezea kwa kusema, msemaji huyu alisema ya kuvunjika kwa mkataba uliyowekwa mwaka 1990 kati ya Urusi na NATO kuhusu maswala ya kijeshi, ni ishara nyingine ya utete huu.
Pichani hapo juu ni picha ya moja ya makombora ambayo yalitakiwa kuwekwa nchini Poland na jumuhuri ya Czech,na picha ya chini ni picha ya Pentagon iliyopo nchini Amerika, ndani ya jengo hili vichwa bado vinawauma ni jinsi gani na lini hali ya mvutano itakwisha.
Hali inapo zidi kuwa ngumu, binadamu hukumbaka mbinu za mababu.
Gaza, Paletina - Kutokana na hali ya kuwekewa mbinyo wa kimataifa ukiongoza na srael, wakazi wa mji wa Gaza na vitongoji vyake wamaekuwa na wakati mguu wa kuendesha maisha yao ya kila siku, hasa katika nyanja za usafiri.
Hii hali inawafanya wananchi wa Gaza, kuanza kuishi yale maisha ya mitume kwa kutegemea wanyama kama usafiri.
Mnyama huyu ajulikanaye kama punda kwa sasa bei ya mnyama huyu ajulikanaye kama punda anagharimu kiasi US $ 250 mpaka US $ 400.
Hadi kupataikana kwa habari hizi, mnyama ajulikanaye kama punda amekuwa kipusa.
Kufuatia mnunuzi mmoja wa punda bwana Saber Dabour,alisema ya kuwa wanunuzi wa punda, huwana jua ni punda wa aina gani anawafaa, kwani huwa punda anafunguliwa kinywa na kuangalia meno, na kuwapima nguvu punda kwa kuwajaribisha kuvuta mizigo ya uzito fulani.