Sunday, December 2, 2007

Harakati za uchaguzi wa bi Hillary Clinton zapata msukosuko.

Maendeleo ya China yazidi kutikisa dunia, na mlembo wa dunia je?

Beijing, China- Mwana dada kutoka china Zhang Zilin, amshinda kwa kuwa mwanadada mrembo kulikoni wote dunia.
Mashindano hayo ambayo yaliwashilisha warembo kutoka mataifa yote duniani dada Zhang alishinda kwa uzuri na kila aina.
Zhang Zilin mwenye miaka 23, na urefu wa mita 1.cm 82,alikuwa kivutio cha wengi duniani kote kwa waliokuwa kwenye ukumbi wa maonyesho hayo na wale tuliokuwa tunaamgalia mashindano haya ya ulimbwende kupitia luninga.
Washindi wa wengine ni waliomfuati kwa uzuri dada Zhang, dada kutoka Angola ,na Mexico.
Pichani anaonekana dada wa urembo duniani Zhang Zilin, akiwa ametoa pose yaaina yake kuwaelezea ya kuwa hakushinda kwa bahati, bali yeye ni mzuri, picha nyingine chini anaonekana mwana dada Zhang Zilin, alipopiga picha ya pamoja na washindi wa pili na watatu kwa uzuri duniani.
Mwana wa Kibrazil Kakaa, akamata zawadi nyingine ya dhahabu.
Paris, Ufaransa - Mwanasoka na mtaalamu wa kutikisa nyavu za kila timu pinzani, wa timu ya Kaka ameshinda tena kuwa mcheza bora wa Ulaya, kwa kushinda kwa kura nyingi kuwapita wanasoka wenzake na hivyo kuzawadiwa mpira (soka) Ballon d' Or - wa dhahabu, mjini Paris.
Kakaa ambaye akishirikiana na wachezaji wenzake wa AC Milan, kushinda kombe la klabu bingwa la Ulaya msimu wa mwaka 2006-2007.
Wachezaji wengine ambao waliokuwa wakigombania zawadi hii, ni Ronaldo wa timu ya Man Unite na Leon Messi wa timu ya Barca ya Uispania, ambao walishika nafasi za pili na tatu.
Pichani anaonekana akibusu mpira wa dhahabu aliyo zawadia, picha nyingine anaonekana bwana Kaka akimnyanyasa mchezaji wa timu pinzani katika moja ya mashindano ya kombe la Ulaya yanayo endelea, na picha nyingine anaonekana bingwa Kakaa akishangilia kwa kuinua mikono juu baada ya kutikisa nyavu za timu pinzani.
Moto wa soka waanza kuchemka kwenye roho za wapenzi barani Ulaya.
Zurich - Switzerland- Chama cha mpira cha shirikisho la Ulaya, kimemaliza kupanga makundi ya timu za taifa, ambazo zitapambana kugombea ubingwa wa kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2008 ambayo yata fanyika katika nchi jirani tofauti, Switzerland na Austria.
Kundi ambalo watafiti wa soka, wanahisi kuna makundi mawili ambayo yataleta upinzani mkubwa kisoka, wakati timu za taifa zitakapo pambana
Wengi wanahisi kundi B ambalo linajumuisha, Germani,Kroatia,Austria na Poland, litakuwa kundi la kufatilia kimakini, hasa kwa kuzingatia historia za nchi hizi, zinavyo karibiana.
Hata vivyo, kundi C, ndilo litakuwa jicho la wana soka na wapenzi wa soka, hasa kwa kukutanisha, timu za taifa kama Italy na Fransa ambazo kati yake zilisha kuwa mabingwa wa dunia, Holland na Romania ambazo zinawachezaji wnaocheza timu kubwa duniani, na wengi ya wachezaji wao wa uzoefu wa kucheza soka kimataifa.
Hivi ndivyo makundi yalivyo
Kundi A - Switzerland, Czech Republic, Ureno, na Uturuki.
Kundi B - Austria, Croatia, Ujerumani na Poland.
Kundi C - Holland, Italy,Romania,na Ufaransa.
Kundi D - Ugiriki, Swedeni, Uispania na Russia.
Pichani ni alama ya chama cha shirikisho la soka la Ulaya, na picha nyingine hapo juu ni picha za wachezaji wa Ufaransa, Italy na Uholanzi.
Harakati za uchaguzi wa bi Hillary Clinton,zapata msukosuko.
New Hampshire, Amerika - Raia mmoja wa Amerika, ambaye aliingia kwenye ofisi za mgombea uchaguzi wa urais kupitia chama cha demokrasi, bi Hillary Clinton, amedai ya kuwa anamatatizo ya akili toka kipindi alicho lawitiwa na mchungaji wa kanisa.
Bwana huyo kwa jina Leeland Eilsenberg, aliingia ofisini kwa seneta Hillary Clinton, ambamo kulikuwa na watu watano na kudai ya kuwa na bomu ambalo ameijizungushia kwenye kifua chake.
Hata hivyo baadaye ilikuja julikana yakuwa alikuwa amejifunga maboksi tu.
Kizaaza hicho kilichukuwa muda wa masaa zaidi ya manne, kabla ya kukamatwa kwa bwana Leeland Elsenberg.
Pichani anaonekana,bi Hillary Clinton , akiwahutubia wanachi wakati wakampeni zake, na chini ni picha ya bwana Leeland Elsenberg, ambaye alitaka kutia doa kampeni za bi Hillary Clinton.
Tishio jingine la kupoteza maisha laingia mashariki wa Uganda.
Kampala, Uganda - Ofisi ya wizara ya afya nchni Uganda, ipo mbioni, kupambana na ugonjwa wa EBOLA, ambao umesha ua watu wapatao 18 hadi sasa.
Kutoka na kuwepo kwa ugonjwa huu, serilikali ya Uganda imeweka vizuizi vyakuingia maeneo aliyo kumbwa na ugonjwa ambao umetanda eneo la Bundibugyo magharibi ya Uganda.
Vugu vuvu la kuwepo kwa ugonjwa huu, ulianza mwanzoni mwa septemba, lakini ilichukua muda kujulikana, mpaka ugonjwa huu ulipo wakumba wafanyakazi na wauguzi wa maeneo hayo.
Kihistoria ugonjwa wa EBOLA, huwa unapoteza maisha ya watu kwa 90% baada ya kuingiwa na virusi hivi. Pichani hapo juu, ni wagonjwa wa EBOLA, wakiwa katika maibabu, na chini ni picha ya virus ya EBOLA.
Lazima tujitahidi kumshinda adui huyu anaye hatarisha maisha ya watu wote"Hasa vijana".
Johannesburg,Afrika ya Kusini- Rais wa zamani wa Afrika ya kusini na mpigania haki za binadamu, bwana Nelson Mandela, amesema alishindwa kulishuhurika vizuri tatizo la kupambana na ugonjwa wa ukimwi kikamilifu wakati wa urais wake.
Akiwahutubia mamia ya watu waliohudhulia siku ya ukimwi duniani, ambayo hufanywa kila desembe 1 ya kila mwaka, amezitaka serikali kulitilia mkazo kwa kuchangia pesa ili kupamabana na tatizo hili la ugonjwa wa ukimwi.
Wakati wa hadhimisho hilo, amabalo lili hudhuliwa na wanamuziki mbalimbali waliovalia nguo zenye namba 46664, ambayo ilikuwa namba ya bwana Mandela alipo kuwa kifungoni huku katika kisiwa cha Roben, kilichopo bahari ya Atlantiki karibu na mji wa Cape Town.
Hapo juu pichani anaoneka rais wa zamani wa Afrika ya Kusini bwana Nelson Mandela akihtubia mamia mjini Johannesburg kwenye uwanja wa Els Park.
Vladimir Putini, na United Russia washinda tena uchaguzi"Nguvu zaongezeka".
Moscow, Urussi- Chama cha United Russia, kinacho ongozwa na rais Vladimir Putin, kimeshinda uchaguzi ulio fanyaka siku ya jumapili 2/2/207.
Chama cha United Rassia, kimeshinda kura kwa asimilimia 61% za kura zilizo pigwa.
Kutokana na matokeo haya chama Unied Russia, kinachoongozwa na bwana Putin, kimejipatia viti vipatavyo 306 kati ya 450 kweye bunge la nchi hiyo (DUMA).
Pichani anaonekana, rais Putin akiwapungia watu walio kuja kupiga kura, baada ya rais Putin kumaliza kupiga kura yake.
Panapo jitihada, kujituma na kutumia maarifu, mabadiliko hutokea."Malawi"
Lilongwe, Malawi - Baada ya kipindi kisicho pungua miaaka kadhaa, nchi ya Malawi ilikuwa nimoja ya nchi, ambayo ilikuwa inelekea kwenye janga la kuwa na njaa kubwa kusini mwa bara la Afrika kwa kushindwa kulisha wananchi wake wapatao million 13, lakini janga hili limeelekea kupungua.
Hali hii imejionyesha baada ya Malawi kuanza kuuza mazao waliyo yapata nchi za jirani, kama Zimbabwe, na hali ya utapia mlo kuanza kupngua kwa kiasi kikubwa.
Akiongea, kusisitizia mabadiliko ya kilimo nchni Malawi, msemaji mmoja wa shirika la kusaidia watoto UNICEF, amesema hivi sasa, misaada ya vyakula iliyotolewa na shirika hilo, haitatumika kwa sasa, bali wataipeleka nchini Uganda ili isaidie watoto wa nchi hiyo.
Pichani, wanaonekena wananchi wa Malawi wakipokea misaada, kipindi nchi ya Malawi ilipo kuwa na hali mbaya kilishe.

Uchaguzi wa Amerika, umaharufu kutumika kuongezae kura.
Chicago, Amerika - Bi, Oprah Winfrey, ambaye ni mmoja ya wanawake matajiri duniani, (mamiloneea), amekubali kushirikiana na mgombea uchaguzi wa rais nchini Amerika, bwana Baraka Obama.
Bi, Oprah, atakuwa na bwana, Baraka Obama mgombea urais kupitia chama cha demokrasi, watakuwa pamoja kwenye kampeni kwenye jimbo la Illinoi.
Wachunguzi wa kisiasa, wamesema ya kuwa kampeni hii, itakuwa ya namnayake.
Pichani hapo juu ni anaonekana bi, Oprah Winfrey's, akiwa pamoja na bwana Baraka Obama na mke wake bi Michelle Obama.
Hata ukiwa ukimbizini, hukumu hutolewa bila kuwepo mtuhumiwa.
Moscow, Urussi - Mmoja wa matajiri wa Kirussi, na mpinzani mkuu wa serikali ya Urussia bwana Boris Berezovsky, amehukumiwa kwenda jela wakati yupo ukimbizini nchini Uingereza.
Bwana, Boris Berezovsky, alikutwa na makosa ya kuhusika nakutaka kufirisi na kutumia pesa za shirika la ndege la Russia Aeroflot, wakati alipokuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo.
Bwana Borezovsky, ambaye alikuwa mmoja wa Kremlin,alikimblia Uingereza,baada yakutofautiana na wanakremlin wenzake.
Akiongeza kwa kusema ya kuwa hukumu hiyo, likuwa ni ya uongo na inamsukumo wa kinamna.

No comments: