Wednesday, December 5, 2007

Niwakati wa kurudisha mapato,ili kujenga jamii"Brad Pitt"

Mashindano ya vilabu bingwa vya Ulaya, rekodi mpya ya wekwa.

Milan,Itali - Mshambuliaji wa timu ya AC Milan na timu ya taifa ya Itali, Phillipe Inzaghi, amevunja rekodi ya kombe la mashindano ya vilabu bingwa vya Ulaya kwa kuwa mfungaji mwenye magoli mengi.
Inzaghi, ambaye emeshatikisa nyavu mara 63 za timu tofauti zinazo na zilizo shiriki katika mashindano haya vilabu vya Ulaya.
"The PIPO" kama anayojuikana kwa washabiki wake,alivunja rekodi hii baada ya kufunga goli la pekee, wakati timu yake AC Milan iliposhinda timu ya Celtic kutoka Scotland kwa bao 1-0.
Mchezaji ambaye alikuwa anashikilia rekodi hii alikuwa mcheza wa timu ya Beyern Munchen na timu ya taifa ya Ujerumani Gerd Muller aliyekuwa amefunga magoli 62, mpaka alipo tundika ndula au daluga zake.
Pichani hapo juu anaonekana "The PIPO" Phillipe Inzaghi akilibilingisha gozi la mnyama, huku mchezaji wa timu pinzani akiangalia kwa kukata tamaa,picha ya chini anaonekana PIPO, akinyoosha kidole baada ya kuvunja rekodi ya magoli kwenye mashindano ya vilabu ya Ulaya.
Nawaombeni radhi wapenzi wangu, kwa yote yaliyo tokea.
London, Uingereza - Mwana muziki, maharufu duniani Robbie Williams,amekubali kulipa fidi baada kwa kampuni moja ijulikanyo kama TAKE THAT.
Robbie, imembidi alipe fidia hii baada ya kushutumu mmoja wa viongozi wa kampuni ya TAKE THAT, bwana Martin Smith, ya kuwa ameiba fedha za kampuni.
Akiongezea kusema, Robbie aliomba adhi kwa wapenzi wake kwa msukosuko huu.
Pichani anaonekana, Robbie Williams akianda kutumbwiza wapenzi wake kaika moja ya mnyesho yake, chini ni picha ya Robbie anaonyesha ulimbwende uliopo kwenye mwili kama kivutio kwa wapenzi wake.
Wa Kuba wa bado wanaimani na kiongozi wao mwana mapinduzi.
Havana, Kuba -Bunge la Kuba limemteua rais Fidel Castro kuwa mgombea pekee katika kiti cha urais.
Rais Fidel Castro, ambaye anaumri wa miaka 81, amekuwa rais wa Kuba kwa muda usio pungua miongo mitano.
Kwa kupendekezwa kwake rais Fidel Castro, kutamwezesha kutawala tena kama rais kwa kipindi kingine, na wachunguzi wa siasa wanadai, huenda akamwachia madaraka mdogo wake Raul Castro.
Hapo juu anaonekana, rais Fidel Castro akimwonyesha muda walio wasili hayati baba mtakatifu John Poul IIalipo wasili kiwanja cha ndege. Chini anaoneka rais Castro akiongea kwenye simu baada ya kupata nafu baada ya kufanyiwa upauaji.
Niwakati wa kurudisha mapato ili kujenga kwa jamii,"Brad Pitt".
New Orleans, Amerika - Mcheza sinema maharufu duniani Brad Pitt mwenye miaka 43, ametoa kiasi cha US $ 5 millioni kwa ajili ya kujnga nyumba za kuishi watu waliokumbwa na mafuriko mwaka 2005 katika mji wa New Orleans.
Akiongea hivi karibuni Brad, alisema ya kuwa mradi huu ni kwa ajili ya kurudisha upya sura ya mji wa New Orleans, ambao ulikumbwa na mafuriko yaliyo sababisha uharibifu mkubwa kwa jamii.
Nyunba hizo zitajengwa katika mazingira ya kisasa, bila kuleta matatizo hali ya ubinjani,bali zitasaidia kuboresha hali ya hewa. Alimalizia kwa kusema Bad.
Brad na mpenzi wake Angelina Jolie, wanamakazi ndani ya mji wa New Orleans kwenye eneo lijulikanalo kama French Quater. Pichani anaonekana Brad Pitt, akiongea na viongozi wa ngazi za juu nchini Amerika,picha iliyopo katikati ni picha ya nyumba mpya ambazo zitajengwa, na picha ya mwisho ni picha ya baba mwenye familia Bred na mpenzi wake Angelina wakiwa wana kula hewa.
Mbona mumetusahau, mateka wa walalamika chini ya mtutu.
London.Uingereza - Raia mmoja anaye aminika ni mwingreza, ameonekan katika luninga na mitandao.
Raia huyu ambaye inasadikiwa alitekwa mapema mwaka huu 2007, wakati alipo kuwa kikazi nchini Iraq, alionekana na kusikika kuiomba Uingereza itoe majeshi yake nchini Iraq.
Wateka nyara hawa wameipa Uingereza siku kumi, kutimiza masharti haya.
Raia huyu, alionekana akiongea huku mitutu ya bunduki ikiwa mgomgoni mwake,na kudai yakuwa wamesha kuwa nchni ya ya mateka kwa siku zipatazo 173, inaonekana ya kuwa tumesahaulika.
Inaamika ya kuwa ya kuwa wameshikiliwa na Islamic Shiite Resistance of Iraq.
Pichani anonka mateka huyu, akiongea kupia mitandao na luninga.
Hatuna mchezo wa upeleleza kutumia mtandao" Quin"
Bejing, China - Serikali ya china, iekanusha vikali ya kuwa inafanya upelelezi kwenye makampuni ya kibiashara na mabenki kwa kutumia mtandao.
Akiongea haya siku ya jumanne wiki hii,msemaji wa ofisi ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uchina Quin Gang, amesema hii siyo kweli na na serikali ya China haiwezi kufanya kitendo kama hiki.
Shutuma hizi za China kuchunguza serikali nyingine kwa kutumia njia za mtandao, zilishawahi kutolewa na serikali ya Amerika,serikali ya Uingereza na Ujerumani.
Hapo juu ni bendera ya China ,a chini ni bendera ya Uingereza.
Dunia ya pumua kwa kiasi fulani,Irani haina nia mbaya"Rais wa Iran"
Teheran,Iran - Rais wa Iran, bwna Mahmoud Ahmadinejad, amesema ya kuwa ripoti ambayo imetolewa na wachunguzi wa usalama wa Amerika (NIE) National Intelligence Estimate, ambayo imeripoti ya kuwa Irani haina mpango wa kutengenza bomu la nyuklia, na shutuma zote zilizo tolewa ya kuwa serikali ya Iran, ina endelea kutengeneza bomu la nyuklia ni pigo kwa wale wote waliojenga hoja hii ya kuichafua Iran.
Akiongea kupitia luninga a taifa, rais Mahmoud Ahmadinejad, alisema vitisho vyote vilivyo tolewa, vimeonyesha ya kuwa Iran haina nia mbaya.
Kwa kusitiza habari hizi, mkurugenzi mkuu wa maswala ya nyuklia Mohamed ElBaradei, amesema, ripoti hii ya NEI(Wachunguzi wa Usalama wa Amerika), imeipa unafuu, ripoti yake kwani hazina tofauti.
Pichani hapo juu anaonekana rais wa Iran, bwana Mahmoud Amadinejad, akionyesha kidole huu kuashiria ushindi, napicha nyigine anaonekana rais wa Amerika bwana George Bush,akiwa wanongea na wandishi wa habari, baada ya ripoti kuhuru Irani kutolea na NIE.
Hali ya Somalia yazidi kuwa kitendawili, serikali ya Ethiopia mambo ni magumu.
Adis Ababa, Ethioopia - Serikali ya waziri mkuu wa Ethiponia Meles Zanawi, ameomba nchi za jumuia ya kimataifa, kuanza kusaidia harakati za kuleta amani nchni Somalia.
Mwito huu unakuja, baada ya serikali ya Ethiopia kutangaza ya kuwa itakuwa vigumu kutoka kwenye mapambano ya vita vya wenye kwa wenyee vilivyopo nchini Somalia, ambapo majeshi ya Ethopia ya na saidiana na majeshi ya serikali ya mpito ya Somalia, kupambana na kundi la wapinzani wa Serikali ya Somalia inayoongozwa bwana Abdullahi Yusuf.
Wakati huo huo, rais wa serikali ya mpito ya Somalia amewasili nchini Uingerza kwa matibabu zaidi, inamini ya kuwa bwana Abdillahi Yusuf, amepatwa na hali ya mchoko kiafya.
Pichani hapo juu ni picha ya waziri mkuu wa Ethiopia bwana Meles Zanawi, na picha nyingine ni picha ya wasichana wa Kisomalia wakiandamana kudai wapatiwe haki zao, hata kama wapo kwenye kambi za wakimbizi.

No comments: