Tuesday, December 18, 2007

Huenda ikawa moja ndoa iliyo kaa muda mfupi katika historia ya Holly Wood.

Dawa za kuzuia kipara za mletea mushkeri nyota ya Brazil ya 1994.

Rio De Jeneiro, Brazil - Mshambuliji hatari wa Vasco Da Gama na aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil pia kuwa mfungaji bora wa mashindano ya kombe la Dunia 1994 yaliofanyika Amerika Romario amefungiwa kucheza mpira kwa muda wa siku 120.
Hukumu hiyo ilitolewa na jopo la majaji wa kwa kushirikiana chama cha soka nchini Brazil, baada ya Romario, kujulikana alitumia madawa ya kuonngeza nguvu mwilini, bila kukusudia.
Romario,alisema madawa haya, aliyanywa ili kusaidia kukuza nywele zake, na anaona matokeo yake yakuwa nywele zake zinazidi kukua tangu kaanza kutumia dawa hizi.
Romario, ambaye alifunga bao la 1000, alidai ya kuwa analaumu haya madawa ya kukuza nywele kwa kumletea haya matukio ambayo siyo mazuri kisoka.
Hata hivyo anatarajiwa kurudi uwanjani tena pindipo kigungo hiki kikiisha aliseama Romario.
Pichani hapo juu anaoneka De Souza Romario, akipokea zawadi ya kuwa mchezaji bora wa timu yake Vasco Dama mwaka huu,chini pichani Romario, akifanya mavitus, kupita kijana na kuonyesha ya kuwa utu uzima huwa dawa.
Picha ya chini, anaonekana Romario na Rivarldo wakishangilia kwa pamoja baada ya De Souza kufunga bao la kuipeleka Brazil Asia kwenye mashindano ya kombe la dunia mwaka 2002, nchini Japan na Korea.
The Prince of Bel air aibuka tena na kitu kipya na mafaranga kemkem.
Holly Wood, Lo Angeles - Mcheza sinema maharufu na mwana vitimbwi duniani, bwana Willy Smith ameweka moja rekodi ya mwezi wa kuminambili (Desember), kutokana na mauzo ya tiketi ya sinema yake mpya ijulikanayo kama The Legend. Sinema hii ambayo imemwingizi kiasi cha millioni 72.6, kuzidi sinema za kwanza alizocheza.
Pichani anaonekana Willy Smith,akiongea na wandishi wa habari ndani ya jiji la Los Angerles, na picha ya katikati anaonekana Willy Smith akionyesha jinsi gani moto unavyo unguza.
Hapo chini anaonekana Willy Smith (Prince), akionyesha kidole kwa wapenzi kuashiria bado nipo na mavitus mengine yanakuja hivi karibuni.
Huenda ikawa moja ndoa iliyo kaa muda mfupi katika histori ya Holly Wood.
Los Angeles, Amerika - Mwana mitindo na msanii bi Pamela Anderson mwenye miaka 40, anakaribia kuachana na mumewe, masanii mwenziwe bwana, Rick Salomonmwenye miaka 38, hivi karibuni. Bwana Rick Solomon, amabye anajulikana kwa umaarufu wa kucheza sile sinema za kufanaya mapenzi duniani.
Wapendanao hawa walifunga ndoa hivi karibuni, na ndoa yao huenda ikawamoja ya ndoa zilizodumu muda mfupi kataiaka historia ya wasanii na wana mitindo.
Kuvunjika kwa ndoa ambayo imedumu kwa muda wa wiki 10 (KUMI). Pichani hapo juu anaonekana bi Pamela Anderson akiwa njiani kwenda kujirusha, na chini anaonekana bi, Pamela Anderson akiwa kazini kutangaza moja ya mitindo ya mavazi ya kina mama.
Makomrade wa ANC, wamchagua Zuma, Mbeki hapata nusu ya kura.
Polokwane, Afrika ya Kusini -Chama tawala cha ANC - African Nationala Congeress, kimemchagua kiongozi mpya wa chama hicho, katika mkutano mkuu wa chama hiki mjini Polokwane.
Kiongozi huyu sio, mwingine ni aliye kuwa makamu wa rais wa Afrika ya Kusini bwana Jacob Zuma, ambaye alimshinda mpinzani wake kwakupata kura 2329,ambaye ndiye rais wa sasa wa Afrika ya Kusini, bwana Thabo Mbeki ambaye alipata kura 1505.
Kuchaguliwa kwa bwana Jacob Zuma, kumeonekana ni ushindi mkubwa kwa wafasi wake, kwakuzingatia ya kuwa bwana Zuma, alifukuzwa kazi na rais Mbeki, kwa kufanya makosa ndani ya serikali, hata hivyo bwana Zuma alikanusha tuhuma hizo.
Hata hivyo mmoja wa msemaji wa chama cha vijana wa ANC,( ANCYL - African National Congress Youth Leauge), alisema ya kuwa, rais Mbeki alichaguliwa na vijana hawa, na ndiyo walio mtoa madaraka ya kuongoza chama, na inaonyesha yakuwa vijana wananguvu.
Pichani hapo juu anaonekana mwenyekiti mpya wa cham tawala ANC bwana Jacob Zuma akiwasalimia wapenzi na wafuasi wake.
Picha chini wanaonekana vijana wa ANC, wakiwa katika harakati za kampeni.
Hopa chini wanaonekana bwana Jacob Zuma, akipiga makofi, mpinzani wake, rais Thabo Mbeki akiangali pembeni nini kinaendelea.
Waingereza walipewa siku 12,atawafukuza kwa kupinga mwelekeo nchi "Iddi Amini Dada".
Kampala, Uganda - Inaaminika siku kama ya leo tarehe 19/12/ ni siku ambayao kwa mara ya kwanza, aliyekuwa rais wa Uganda Gen, Iddi Amini Dada, aliwamuru wafanyakazi wote wenye uraia wa Uingereza kukubaliana na matakwa ya serikali yake na upunguzaji wa mishahara ama amnawapa siku 12 kuishinchini.
Punguzo hilo lili kuwa la asilimia 40%, habari hizi zilimfikia barozi wa Uingereza wakati raisi Aiddi Amini alipo kuwa akiongea na taifa kwa kupitia vyombo vya habari na kuwaomba wafanya biashara wa Uingereza waishio nchini Uganda kuthibitisha mali, vitu na fedha walizo nazo kabla ya mwisho wa mwaka yaani tarehe 31 Desemba.
Rais Iddi Amini, alisema "nafanya hivi kuzuia, isitokee tena kile walicho fanya watu wa jamii ya kihindi na Waisrael kwa kumbia na mali,vitu na fedha wakati walipo ondoka hapa cnhini"
Pichani hapo juu anaonekana Gen Iddi Amini Dada, akiwa ametinga mavazi ya kazi( Kijeshi) tayari kukagua gwaride.
Picha nyingine anaonekana Gen Iddi Amini Dada, akiwa amebebwa na raia wa (Ulaya), wafanyabiashara wakati waufunguzi wa mkutano.
Chini ni picha ya Iddi Amini Dada, ikiwa amevaa nguo za kiraia enzi za uhai wake.
Waislamu watimiza moja ya nguzo za Uislam kwa kuomba na kutubu.
Mlima Arafat, Saudi Arabia - Waislama kote duniani wanaadhimisha sherehe ya siku nya IDD Alfitri.
Sikumoja kabla ya siku yaleo Waislamu waliojaliwa kwenda Kuhiji pale pahali patakatifu kwenye mlima Rahma ambao huko nchini Saudi Arabia.
Kabla ya sikuku ya Idd Alfitri Waislamu waliojaliwa kuhiji huomba Mungu, kutumbu zambi, na kumpiga shetani kwa mawe ili kukamilisha moja ya nguzo kuu za Kiislamu.
Moja ya watu waliokwenda kuhiji mwaka huu ni rais wa Iran, bwana Mahamoud Ahmadinejadalikuwa mmoja wapo wa waumini hawa waliojaliwa kufanya Hija hii. Hspo juu pichani wanaonekana Waislamu wakiwa wanatupa mawe kabla ya kuanza sherehe za Iddi Alfitri.

Sheria za Uingereza zamkatisha safari waziri wa Israel.
Tel Aviv, Israel - Waziri mmoja nchini Israel bwana Avi Dicther, alikatisha ziara yake kutembela Uingereza, baada ya kuoneka ya kuwa huenda akakamatwa na polisi kwa kosa la mauaji na serikali ya Uingereza kushindwa kumuhakikishia kama hatakamatwa na polisi na kushitakiwa na kesi ya mauaji ya aliyekuwa kamanda wa Hamas bwana Sarehe Sheheda na familia, watoto tisa,mke wake na pamoja na walinzi wake
Mauaji haya yalitokea mwaka 2002 julai wakati bomu la tani moja lilipo dondoshwa juu ya nyumba ya bwana Sarehe Sheheda na bwana waziri Dechter alikuwa ndiye mkuu wa kikosi cha Shin Beth Agency ambacho kilipewa kazi ya kumundoa kiongozi huyo wa Hamas.Hapo juu pichani ni waziri Avi Dechter, amabye ame hairisha safari ya kutembelea Uingereza, ili kuhutubia katiaka moja ya vyuo vya nchini Uingereza kuhusu ugaidi.

Kufuatia msemaji wake Barak Sari, bwana Dichter huenda akafunguliwa mashitaka na moja ya makundi fulani yaliyopo nchini UIngereza kwa kosa hilo.Akiongezea sheria za serikali ya UIngereza zinammruhusi mtu yoyote au raia yoyote kumfungulia kesi mtu yoyote awapo nchini humo
Liberia yamkamata aliyekuwa rais wa serikali ya mpito kwa kuhusika na hujuma.
Monrovia, Liberia - Polisi nchin Liberia wamemtia ndani, aliyekuwa rais wa zamani wa Liberia bwana Gyude Bryant, kwa matumizi mabaya ya faraga za serikali wakati wa urais wake.
Kukumatwa kwake kumekuja baada ya bwana Bryant, kushindwa kufika mahakamani kujibu mashitaka yake ya upotevu na matumizi mabaya ya fedha zidi ya millioni moja.
Bwana Gyde Bryant, alikuwa rais wa mpito baada ya vita visivyo pungua mwngo mmoja na nusu kumalizika
Picha hapo juu ni picha ya rais wa zamani wa Liberia bwana Gyude Bryant, picha nyingine anaonekana raia mmoja wa Liberia, akitokea kuvuna zao la mpira, ambalo ni moja ya zao linalo iingizia nchi ya Liberia kipato.
Jueni mambo yenu, Kenya siyo koloni lenu tena"Waziri wa sheria"
Narobi, Kenya - Serikali ya Kenya hivi karibuni, imetoa onyo kwa serikali ya Uingereza kuacha kuingilia mambo ya ndani ya nchi ya Kenya.
Akiongea haya Waziri wa sheria wa Kenya Bi Martha Karua, amesema kitendo cha bunge la Uingereleza kujadili swala la rusha nchini Kenya, ni sawa na kuifanya serikali ya Kenya bado koloni la Uingereza.
Hii imekuja baada ya mmoja ya mbunge na waziri Baroness Vadera kusema ya kuwa, kuna matumaini kidogo ya uchaguzi kuwa wa halali,kwa kuzingatia hali halisi kwa serikali ya Kenya kushindwa kupambana na rushwa nchini humo.
Na kuitaka Uingereza kufuatilia maswala ya rushwa nchini mwake.
Hapo juu ni picha za bwana Kalonzyo Musyoka akiwa katika kampeni za uchaguzi, chini ni rais Mwai Kibaki akisalimiana na wafuasi wake kabal ya kuanza mkutano wa kampeni ya uchaguzi utakaofanyaika mwaka hu desemba 27 mwaka huu 2007.

Aliyesadikiwa kuwa dereva wa Osama kujua hatimayake hivi karibuni.
Washington USA-Serikali ya Amerika inafikiria kiundani ni jinsi gani watakavyo mfungulia mashitaka bwana,Salim Ahamed Hamdani ambaye alikuwa dereva wa bwana Osama BinLaden.
Habari kutoka kwa wachunguzi wa mambo ya kiusalama, wanadai huenda akafungulia kesi kama mfungwa wa kijeshi , nakama atafunguliwa kesi kama mfungwa wa kijeshi, basi itaibidi serikali ya Amerika ifute sheria zote za makubaliano ya Geneva.
Wakati huu vilivile, serikali ya rais Bush, bado inatakiwa kutoa jibu lolililo sahii ni kwanini,CIA waliziharibu picha za video, ambazo zilikuwa na picha zinavyo onyesha ni jinsi gania watu wanaushukiwa kuwa ni wafusi wa kundi la Al Qaeda walivyo kuwa wakifanyiwa, ili kupata habari za kuhusu kundi hili.
Pichani ni picha ya bwana, Salim Ahmed Hamdani, ambaye inasemekana alilkuwa dereva wa bwana Osama, na picha nyingine ni alama ya CIA.
Magharibi ya ya Afrika ndiyo chanzo cha kumiminika madawa ya kulevya Ulaya?
Bissau,Guinea Bissau - Serikali ya Guinea Bissau,imekuwa na wakati mgumu wa kupambana na mmiminiko wa madawa ya kulevya (mihadarati) kwenye mipaka ya nchi yake. Vile vile kutokana na umasikini wa naukwasi wa kipato kwa wananchi ambao hupata kiasi cha nusu $ dola ya Amerika kwa siku,na hii ndiyo chanzo cha kuwa na miminiko huu wa mihadarati nchini humo alisema mmoja bwana Jamel Handem.
Na kutokana na hali ya ukiukwaji wa sheria, inasemekana baadhi ya wafanya biashara
watuhumiwa wamekuwa wakiachiwa na vyombo vya sheria, hata baada ya kukamatwa.
Hata hivyo mmoja wa wananchi wa Guinea Bissau, alisema yakuwa asilimia 95% ya mihadarati hii huishia kupelekwa nchi za Ulaya.
Pichani hapo juu anaonekana akila doria na picha chini mni picha za kina mama wakiwambioni kutafuta mahela, ili kuweza kulisha watoto zao.
Basra ya kabidhiwa kwa wenyewe,Al Qaeda wadai ni ushindi kwao.
Basra, Iraki - Jeshi la Uingereza limekabidhi rasmi madaraka kwa jeshi la Iraki hivi karibuni,sherehe hizo lilifanyika hivi katika jimbo la Basra, baada ya miaka isiyo pungua minne ya jimbo hilo kuwa chini ya jeshi la Uingereza.
Kukabidhiwa kwa madaraka hayo ni moja ya tukio muhimu kwa wananchi wa Iraki alisema mshuri wa maswala ya usalama wa Iraki Dr Mowaffak al - Rubaie.
Uingereza ilikuwa na wanajeshi wasiopungua 4500, nakuanzia hivi sasa watashughulika zaidi na mafunzo ya uundaji wa jeshi la Iraki.
Wakati huo, kiongozi namba mbili wa kundi la Al Qaeda, bwana Ayman al Zawahiri,ambaye ni mzaliwa wa Misri, amesema ya kuwa kuondoka kwa jeshi la Uingereza, ni ushindi kwa wapinza wa serikali ya Iraki, Al Qaeda na wana chama wake.
Pichani hapo juu wanaonekana wanajeshi wa Iraki wakipigakwata kuchukua madaraka kutoka kwa jeshi la Uingereza.
Picha ya kati ni bwana Zawahiri akiongea kuhusu halihalisi ya kutoka kwa majeshi ya Uingereza.
Picha nyingine wanaonekana wanajeshi wa Iraki wakishangilia kwa kutawanya bendera ya nchi yao.

No comments: