Monday, December 24, 2007

The, Hugo Chavez, kuwa mkombozi wa watekwa nyara nchini Kolombia?

Kizuri hukumbukwa siku zote, wapenzi kukongwa na kumbukumbu.

Stocklohm, Sweden - Lile kundi maharufu la muziki duniani, hasa katika miaka ya "arobaini saba" the ABBA GROUP, watafungua jumba lao la kumbukumbu mjini Stockholm ufikapo mwaka 2009.
Jumba hilo la kumbukumbu, litakuwa na vyombo vya muziki walivyo tumia enzi zao, nguo na picha mbalimbali walizopiga na washabiki(wapenzi wao) wakati walipo kuwa pamoja na kutikisa roho za walimwengu na kwakukonga mioyo kwa nyimbo zao Fernando, money nakadhalika. Kundi hili la ABBA, lilikuwa ni Bjorn Ulvaeus, Benny Anderson, Agnetha Faltskog na Anni Frid Lyngstad.
Akiongea haya, afisa anaye simamia mradi huu, Ulf Westeman na mkewe bi Ewa Wigenhem Westen, alisema, watu watakao tembelea jumba hili la kumbukumbu za ABBA, wataru kutumia studio kujaribu kumba na kujikumbusha enzi hizo.
Pichani wanaonkana kundi la ABBA, wakiwa wamekula pozi enzi zao, picha nyingine wanaoneka the ABBA, wakiwa na mmoja ya washabiki wao.
Picha ya chini wanoneka the ABBA GROUP wakifanya vitu vyao miaaaaaaka hiiyo ya 47.
Mama Afrika, achaguliwa bila kupingwa, mama bado ni nguzo ya chama."ANC"
Polokwane, Afrika ya Kusini -Mama mwana mapinduzi, mpigania haki za binadamu ,na mmoja wa kiongozi aliyeongoza kupinga ubaguzi wa rangi usidumu milele nchini Afrika ya Kusini bi Winnie Madigizela Mandela, amerudi tena katika ngazi za juu za za uongozi za chama cha ANC, ambacho ndiyo chama tawala nchini Afrika ya Kusini.
Bi, Winnie Madigizela Mandela, alishinda kura zipatazo 2,845 za wanachama waliopiga kura amabo walikuwa 3,603.
Hata hivyo bi Winnie, alisikika tena , baada ya kutaka kusuhurisha mgogoro uliopo katai ya kambi ya rais Thabo Mbeki, mwenyekiti wa sasa wa ANC, bwana Jacob Zuma.
Pichani anaonekana bi Winnie Mandela akihutubia hivi karibuni, na chini nim picha ya bi Winnie enzi hizo za kampeni, kupinga ubaguzi wa rangi.
The Hugo Chavez , kuwa mkombozi wa watekwa nyara nchini Kolombia?
Havana, Kuba - Rais wa Venezuela,bwana Hugo Chavez, ameseama ya kuwa ule mpango wa kusimamia kuachiwa kwa mateka waliotekwa na jeshi la upinzani la Kolombia FARC hutakamilika hivi karibuni.
Akizungumza baada ya kuudhulia mkutano mjini Havana rais Hugo Chavez, alisema mpango huu hupo njiani na karibuni mateka wote wataachiwa.
Aliongeza ya kuwa mpango huu ni mgumu, kwani wapo baadhi ya viongozi wa serikali hapendi kufanikiwa kwa kuachiwa kwao, na wapo vile vile majeshi ya serikali ambayo yapo tayali kuvuruga mpango huu.
Ikiwa mopango huu ukifanikiwa, basi utazidi kuleta kindumbwembwe kati ya serikali ya Kolombia na Venezuela.
Picha hapo juu ni picha ya kuchora ya rais Hugo Chavez na picha ya kati anaonekana rais Hugo Chavez alipo kuwa akuhutubia umoja wa Mataifa hivi karibuni.
Picha ya mwisho anaonekana rais Chavez wakati wa kampeni ya kuhimiza watu wakubaliane na mabadiliko ya kisasa na kiuchumi nchini Venezuela.
Hezbollah kuzuia maoni ya rais Bush?Hali bado ya utata nchini humo.
Beiruti, Lebanon - Kikindi cha Hezbollah, kimepinga kabisa mawazo yaliyo tolewa na rais wa Amerika bwana Georgr Bush.
Hii inakuja baada ya Lebanon, kukaa kwa kipindi kilefu bila kuwa na serikali kamili itakayo kuwa chini ya rais ambaye mpaka sasa hajachaguliwa kutokana na mivutano ya kisisa kati ya makundi yanayo kubalika na Alaya na Amerika na yale yanayo sadikika ya kubalika na Syria.
Akiongea haya, kiongozi msaidizi wa kundi la Hezbollah, Sheikh Naim Kassem, ya kuwa mambo yote yaliyo zungumzwa na rais Bush, hayatakubalika na kutimizwa.
Pichani ni picha ya rais Bush, amabye anatarajiwa kutembela Mashatiki ya kati hivi karibuni.
Hapo juu ni picha ya bendera ya kundi la Hezbollah, ambalo lina nafasi kubwa kinguvu nchini Lebanoni.
Nguvu zaidi kwa jeshi la AU, Somali bado kasheshe kwa wote.
Mogadishu,Somalia - Katika harakati za kuleta amani na utulivu chini Somali,jeshi la AU ( African Union) limepata nguvu, baada ya nchi ya Burundi kutuma wanajeshi wasiopungua 100.
Kuwasili kwa wanajeshi hawa 100 wa Burundi,ambao walikutana na mashambulizi ya vita kati ya jeshi la serikali na wapinzani wa serikali ya Somalia
AU inawanajeshi wasiopungua 1,600 wengi wao ya wanajeshi wanatoka nchini Uganda,hata hivyo Au inatakiwa kuwa na wanajeshi 8,000 ili kukabiliana na hali mbaya iliyopo nchini Somalia.
Pichani anaonekana mmoja ya mwannchi wa Somalia, akiwa hospitali huku hali yake kiafya ikiwa dhofu li hali na huku akiwa na majeraha kungoja matibabu.
Pichanyingine anaonekana askari wa jeshi la AU, akila doria karibu na ufukwe wa pwani wa bahari ya India nchini Somalia.
Irani yawa joto ya jiwe, kwa mashushu wa nje na ndani ya nchi.
Tehrani, Iran - Ufualiaji wa kujua wapi mmoja ya wafanyakazi wa FBI, bwana Robert Levinson, umefika hatua ya kukatisha tamaa.
Akiongea hivi karibuni , mke wa bwana Bob, alisema imekuwa vigumu kujua yupo wapi?Kwani hapa nilipo nina machungu na majonzi.
Bwana Robert Levinson, aingia nchini Irani kibiashara, namara ya mwisho alionekana kwenye maeneo ya Kish Island kwenye Ghuba ya Persia.
Na hivi karibubi serikali ya Irani, ilimfungulia mashitaka aliyekuwa msamaji wa serikali ya Iran kuhusu maswala ya Nuklia, bwana Hossein Moussa, kwa kuwa mpelelezina kutoa habari kwa serikali za nje.
Pichani wanaonekana mke wa bwana Robert Levinson na mtoto wake wakongea na waandishi wa habari hivi karibuni miji Terhani,
Hapo juu ni picha ya bwana Houssen Moussa, amabye inasadikiwa alikuwa mpelelezi wa serikali za nje.
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, awa muumini"Mungu mkubwa"
Vatican City,Vatican - Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza bwana Tony Blair, amebatizwa tena na kuwa muhumini wa jumuia ya kanisa la Katoriki.
Bwana Blair, ambaye alikuwa hapendelei kuongelea hadharani maswala ya imani na dini yake wakati wa uongozi wake wauwaziri mkuu wa Uingereza.
Hata hivyo bwana Blair, amabye alikuwa ni muumini wa kanisa la Uingereza Agrikani.
Bwana Blair na familia yake walikuwa wanonekana manr kwa mara kuhudhulia misa za kanisa la Katoriki.
Akitangaza, mbele ya waumini wengine, Kardinal Cormac Murphy O Connor, ambaye ndiye kiongozi wa Katoriki wa Wales na Uingereza, alisema tunamkaribisha bwana Tony Blair na familia yake katika familia ya Kikataoriki.
Sala pamoja na maombi yetu yapo pamoja na familia yake.
Pichani anaonekanabwana Tony Blair, akiaga wakati alipo kuwa namalizia kipindi chake cha Uwaziri mkuu wa Uingereza.
Picha nyingine anaonekana bwabna Tony Blair, akiwa na Papa Benedict XVI, mapema mwaka huu.
Shutuma za rushwa bado moto, uchaguzi moto,kusafiri marufuku"Uingereza"
London, Uingereza - Serikali ya Uingereza, imeweka vikwazo vya usafiri kwa mawaziri wa serikali ya Kenya ianyaongozwa na rais Mwai Kibaki nawatu wake wote waliopo karibu na uongozi wake kwa tuhuma za rushwa.
Ofisi ya ubalozi wa Uingereza iliyopo nchni Kenya , imeagiza mashirika yote ya ndege ya yaendayo Ulaya kutowachukuwa viongozi hawa, wakiwemo mawaziri watatu na waziri za zamani wa fedha bwana David Mwiraira na bwana Nicholas Biwott.
Hata hivyo serikali ya Uingereza, imesema vikwazo hivi haviingiliani na hali ya uchaguzi utakaofanyika hivi karibuni.
Hata hivyo msemaji wa serikali bwana Alfred Mutua, alikataa kuongele swala hili, alipo ulizwa na wahandishi wa habari.
Pichani anaonekana aliyekuwa waziri wa zamani wa faranga wa Kenya bwana, Davd Mwiraira, ambaye ndege za UK, kawekewa ngumu,
Ndege aina ya Jet kununuliwa, Uganda yawa na jet mbili za rais?
Kampala, Uganda - Serikali ya Uganda imepitisha bajeti ya kununu ndege aina ya jet kwa ajili ya matumizi ya rais.
Akiongea kuhusu swala hili , kiongozi aliyesimamia uamuzi huu bi Mary Karooro Ukurut,alisema ndege hii itagahalimu kiasi US $dolla 48million.
NDege hii aina ya jet ni ya pili kununuliwa na serikali ya Uganda, baada ile ya kwanza iliyo nunuliwa US$35millionmwaka 2000, kwajili ya matumizi ya rais,nawakati huhu serikali ilikuwa inatafuta mikopo kutoka mashirika ya fedha ya kimataifa, hii ilileta mvutano mkubwa .
Hasa baada ya IMF kuuliza ya kuwa,inakuwaje nchi za kimasikini kukua ndenge za gharama, wakati bado zinadai zifutiwe maden?
Hapo juu, anaonekana rais Yoweri Kaguta Musen, akiongea hivi karibuni kwenye moja ya mikutano nchini Uganda.
Picha nyingine inaonekana picha ya jet, ambayo iatanunuliwa na serikali ya Uganda kwa ajili ya matumizi ya rais.

No comments: