Wednesday, December 19, 2007

Uchaguzi wa mtu bora duniani kwa mwaka 2007 waangukia kwa rais Putini.

Makipa wa ligi ya Brazil, kuanza kuonja Joto ya jiwe" Mguu ulioshiba warudi tena"
Rio De Jeneiro, Brazil - mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na Inter Milan ya Itali Adriano, maeamisha makazi ya kimpira kwa muda na kauanza kuchezea timu ya Sao Poul iliyopo nchini Brazil.
Adrianao mwanye miaka 25, ambaye alikuwa na matatizo ya kifamilia, hasa baada ya kuondokewa na baba yake mzazi, aliye aga dunia miezi michache iliyopita, na kumfananya awe na wakati mgumu saana, alisema mshauri wake.
Kujiunga kwake na timu ya Sao Poul, kumekuja baada ya mshambuliaji huyu mwenye mashuti makubwa na makali, kuwa fiti kwa kila hali kimwili na kiakili pia.
Pichani hapo juu anaonekana Adriano alipo kuwa kipenzi cha timu ya Inter Milan enzi zake, na picha nyingine anaonekana Adriana akituliza kabumbu kwenye friji tayari kufanaya mavitus.
Kapello kukonga mioyo ya wapenda soka wa Uingereza?"Au tatizo siyo Kocha"
London, Uingereza - Baada ya muda kupita hatimaye chama cha mpira cha Uingereza kimategua kitendawili kilicho kuwa kimetegwa kwa wapenzi wa soka wa Uingereza kwa ujumla duniani kote.
Kitendawili hicho kiliteguliwa baada ya chama hicho kumpta kocha atakaye fundisha timu hiyo ya taifa ya Uingereza bwana Fabiano Kapello.
Kocha,Kapello amabaye amesha wahi kuzifundisha timu za Itali na Uispania na kushinda makombe chini ya Uongozi wake anatarajiwa kukonga na kuleta neema ya ushindi nchini Uingereza.
Hata hivyo wataalamu wa soka, wanasema kocha Kapello, ambaye ataanza kazi rasmi mwezi wa januari 7, kwa mkataba wa miaka minne bwana bwana Kapello amejipatia kitita cha $US million 12
Pichani anaoneka kocha Kapello akiwa ndani ya jezi rasmi ya mazoezi ya timu ta taifa ya Uingereza.
Shark's aomba kuachana na mkewe kotini, hakuna tena ukweli wa ndoa.
Miami,Amerika - Mchezaji maarufu duniani wa mpira wa vikapu Shaqquille O'Neil, amerudi tena kwa kuisaidia timu yake kushinda hivi karibu kwenye mashindano ya mpira wa vikapu yanayo endelea.
Shark's kama anavyo julikana kwa wapenzi wake, ameonekana amepunguza kilo kidogo, na hii ianatokana baada ya bwana O'Neil kudai kuachana na mkewe.
Shark's,amesema nataka kuachana namkewe kwani hakuna tena ukweli wa ndani na uaminifu tena, hasa katika njia za kipato.
Shark's,ambaye anawatoto sita amesema huwa anapata muda wa kwenda kuwasalimia watoto, ambao wanaishi na mama yao bi Shaunie.
Pichani anaoneka Shark's akiwa na furaha enzi hizo kabla ya kutangaza kuachana na mkewe, na picha chini anaonekana Shark's akiwa kazini kutafuta kuongezea kipato kwa ajili ya famialia.
Bi Lily Allen, nyota ya muziki kupata mwana,huenda kuacha kuimba mapema.
Holly Wood, Amerika - Mwana muzuki Lily Alen mwenye miaka 22 ,anaaminika ya kuwa ni mja mzito.
Habari hizi zimepatikana kutoka kwa watu wake wakaribu, Lily anasemekana kuwa amekuwa anaonekana mcheza sinema maarufu bwana Ed Simon, na inaaminika huenda wakaa pamoja siku za mbeleni.
Hali hii ya uja uzito imemfanya kusimamisha pirika zote za kimziki mpaka hapo atakapo jifungua, pia inasemekana huenda akaacha kuimba akiwa na miaka 25. Pichani anaonekana bi Lily akionyesha jinsi gani alivyo umbwa na kuumbika mbele ya waandishi wa mitindo, na picha nyingine anaonekana bi,Lily akiingia kwenya moja ya maonyesho ya ulimbwende hivi karibuni
Mali ya asili iliyopo nchini kuwa balaa kwa kizazi,wakulia vita na kuzaliwa wakati wa vita.
Kinshasa, DRC - Vita vinavyo piganwa nchini Kongo DR, vinasemaekana vimefika hali mbaya na jumuia ya kimataifa bado kuamua ni jinsi gani itamaliza vita hivi.
Kutokana na msemaji wa shirika moja la kuhudumi na kutetea haki za binadamau,alisema utajili uliopo nchini humo, umekuwa ndiyo mkosi mkubwa na chanzo cha vita hivyo vilivyo poteza zida ya watu mamillion na wengine kukumbia makazi yao ya hasili na kuishi ugenini.
Akiongezea alisema ya kuwa vita, hivi vimekuwa vikiimaliza nchi ya Kongo DR, kwa malia yake ya asili kuibiwa na kuzwa holera,na vijana wengi kuingizwa katika vita,badala ya kuijenga nchi.
Pichani wanaonekana vijana ambao wangestahili wawe shuleni, wapo wanangojea kwenda kupingana vita ambavyo vilinza wakiwa wadogo ama wengine walikuwa bado kuzaliwa na wajui vita hivi vita kwisha lini.
Uchaguzi wa mtu bora duniani kwa mwaka 2007, waangukia kwa rais Vladimir Putin.
Moscow, Urusi - Rais wa Urusi bwa Vladimir Putini, amchaguliwa na jopo la waandishi wa habari kuwa mtu bora duniani.
Uchaguzi huu hufanyawa na waandishi wa habari kwa kuangalia ni kwa kiasi gani mtu aliye chaguliwa amefanya nini cha maana.
Uchaguzi wa rais Putin, umekuja baada ya kuonekana ya kuwa amekuwa mstari wa mbele kuweka hali ya mambo sawa, hasa kwa kupinga baadhi ya mambo ambayo anaona yataleta msukosuko duniani.
Picha anaonekana rais Putin, akiwa amekaa na sikiliza maelezo kutoka kwa washauri wake, na chini anaonekana rais Vladimir Putin,akijistarehesha kwa kuvua samaki baada ta kazi ngumu za kiofisi.
Ajali ya yaua na kujeruhi mamia, wakati wa sikuku.
Karachi, Pakistani - Treni iendayo kwa kasi, meacha njia na kuuwa watu wasiopungua 41 siku ya jumatano 19/12.
Treni hiyo iliyo kuwa ikisafiri kuelekea mji wa Rahore, ilikuwa imechukua abiria wapatao 1000, wakati ilipo acha reli na kupinduka kilomita 250 miles ( 400km) nje ya jiji la Karachi muda wa saa nane mchana.
Picha hapo juu inaonekana ni kwa kiasi gani treni hii ilivyo haribika baada ya ajli, na picha ya chini anaonekana mmoja ya majerui, akiwasialiana na ndugu zake kwa kutumia simu ya mkono huku akiwa amelala chini karibu na njia ya reli.
Ikuru ya Ufaransa kupata mama hivi karibuni?" Rais wa Ufaransa"
Paris Ufaransa - Wachunguzi wa karibu wa mambo ya kisiasa na familia pamoja na watu wakaribu wa rais wa Ufaransa bwana,Nicolas Sarkozy wamedai huenda akafunga pingu za maisha tena.
Habari hizi zimejiri, baada ya mama wa mpenzi wa mwana mitindo maarufu bi, Marisa Bruni Tendeschi ambaye ni mkazi wa Turin, kupendekeza waoane.Akimalizia kusema mama wa mwana mtindo bi Carla Bruni, alisema simnajua sisi akina mama huwa hataongopi.
Kufuatia habari hizi, inasemekana rais Sarkozy Ameshapendekeza uchumba kuelekea kufunga ndoa kwa bi Carla Bruni.
Rais Sarkozy aliachana na mkewe hivi karibuni baada ya kuishi naye kwa kipindi kisicho pungua miaka kumi na moja.
Kwa mara ya kwanza rais Sarkozy, alionekana na bi Carla Bruni, kwenye maonyesho ya Disney mjini Paris.
Kulia anaoneka rais Nicolas Sarkozy akitabasamu kwa furaha na kushoto anaoneka mama mtarajiwa wa Ikuru ya Ufaransa bi Carla Bruni
Kiongozi atake chguliwa kufuata nyayo za mwanamapinduzi Fidel Castro?
Havana, Cuba - Kiongozi na mwanamapinduzi wa Kuba, rais Fidel Castro ametangaza hivi karibuni anatarajiwa kujiudhuru madaraka yote katika serikali ya Kuba.
Akisoma barua kutoka Ikuru ya Kuba na kwa niaba ya rais Fidel Castro,bwana, Mesa Redonda,alisoma ya kuwa rais Fidel Castro natarajia kujihudhuru na kutoka katika nyanja zote za kisiasa na serikali.
Hata vivyo katika barua hiyo iliyotoka Ikuru, haikuelezea ni lini rais Castro atajiudhuru.
Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanadai huenda, siyo Raul atakaye chukua madaraka haya , bali kuna mwanamapinduzi mwenye damu mpya bwana,Filipe Perez Roque ambaye amekuwa waziri wa mambo ya ndani tangu 1999.
Rais Fidel Castro,amkuwa rais wa Kuba kwa zaidi ya miongo minne, tangu alipongoza mapinduzi ya kuung'oa ubeberu nchini humo.
Picha juu ni bwana Filipe Perez Roque,na picha nyingine anaonekana bwana Raul Castro akisaliamia wana wa Kuba, kabla ya kuhutubia mkutano.
Pichani anaonekana rais Fidel Castro, akiwa katika mavazi ya kiraia wakati wa mazishi ya Papa John Poul II.

No comments: