Thursday, December 20, 2007

Bisheni mtafunguliwa,Tafuteni mtapata,Ombeni mtapewa,"Yathibitishwa na Kaka"

Bisheni mtafunguliwa,Tafuteni mtapata,Ombeni mtapewa,"Yathibitishwa na Kaka".

Geneva, Uswisi - Mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Brazil na AC Milan, Kaka amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa dunia wa mwaka 2007.
Kaka ambaye ameshashinda zawadi ya mchezaji bora wa Ulaya, alichaguliwa kwa kuwapita wapinzani wake Messi wa Argentina na Ronaldo wa Ureno.
Kaka ambaye amekuwa mchezaji bora wa mashindano ya kombe ya klabu bingwa duniani yaliyo fanyika hivi karibuni nchini Japan- Yokohama, na kuingoza timu yeke kushinda kombe hilo kwa kuifunga Boca Junior ya Argentina bao 4 kwa 2.
Akipokea zawadi hii, Kaka alisema ilikuwa akiomba Mungu amtimizie ndoto yake ya kuchezea timu ya Sao Poul na timu ya taifa ya Brazil mechi moja tu, na leo Mungu ameniwezesha kufanikisha haya. Alimalizia kwa kusema Mungu ni Mkubwa na anakupa anavyotaka.
Pichani anaonekana Kaka, akishangilia kuonyesha mikono juu kwa Mola,akiwa ndani ya jezi ya timu yake ya taifa, picha nyingine anaonekana akionyesha mikono juu kumshukuru Mungu baada ya kufanya mavitus yake.
Chini wanaoneka wachezaji bora wa dunia msimu wa mwaka 2006 na msimu wa 2007, wakishangilia na kupongezana baada ya timu yao ya taifa ya Brazil kushinda moja ya mechi walizo cheza hivi karibuni.
Sheri ya mkumba na kumpitia kijukuu cha waziri mkuu wa Uingereza.
Sydney,Australia - Kijukuu wa aliyekuwa waziri mku wa Uingereza wa kwanza baada ya vita nya pili vya dunia, na aliyeiongoza Uingereza katika vita hivyo bwana Winston Churchill, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kukamatwa na madawa ya kulevya.
Kijukuu huyu kwa jina Nicholas Jake Barton mwenye miaka 34 , alikutwa na madawa haya ya kulevya aina ya Ekstasi kama vidonge 250,000, zenye thamani ya $USdolla 8.9 million.
Kijukuu huyu alikili makosa na kupata hukumu hii hivi karibuni na huenda akafikiriwa kutoka baada ya kukaa jela miezi 20, kwa mujibu wa jaji Colin Charteri.
Pichani hapo juu, anekana waziri mkuu wa zamani bwana Winston Churchill enzi hizo alipo kuwa kama waziri mkuu.
Mama asilia achukiapo huwa anamadhara makubwa kwa jamii."Wahenga walisema"
Wellington, New Zealand - Tetemeko la ardhi lenye nguvu kiasi cha magnitude 6.8, limetokea ufukweni mwa masharikia km 50 ya mji wa Gisborne.
Hata hivyo tetemeko hilo halikupoteza maisha ya watu wala kuleta ajaili kwa watu, bali vitu vingi vimehaibika.
Wati huu huo, nchini Uturuki kumetokea tetemeko la ardhi lenye nguvu kiasi cha magnitude 5.3, kwenye mji wa Bala ulipo km 70 ya Ankara.
Hata hivyo hakuna huaribifu mkubwa uliotokea, kulingana na tetemeko la ardhi, lililo tokea mwaka 1999 ambapo watu wasio pungua 18,000 walipoteza maisha yao.
Pichani wanaonekana polisi wakisaidia kutoa vitu kwenye nyumba moja baada ya kukumbwa na tetemeko hili.
Picha nyingine anaonekana mwana mama, akiangalia kwa uchungu, jinsi gani tetemeko lilivyo haribu makazi yake.
Tulishirikiana na mashushu waserikali kupata habari nyeti wapi walipo.
Ankara,Uturuki- Msemaji mmoja wa Serikali ya Uturuki, amesema kuingia kwao nchin Iraki, na kupiga mabomo maaeno yanayo shukiwa ni ya PKK, ilikuja baada ya kupata usaidizi kutoka kwa mashushu wa Amerika.
Akithibitisha haya msemaji mmoja wa serikali ya Amerika Dana Perino, alikubali ya kuwa Amerika ina huusiano wa kishushu na Uturuki.
Hapo juu zinaonekana ndege za jeshi la Uturuki, zikiwa hewani kwenye anga la Iraki, baada ya kumaliza kufanya mavitus yake.
Picha nyingine wanaonekana wanajeshi wa Uturuki wakiwa wanaangalia nini kitacheza au kutikisika na kitendo kitakacho fuata ni kukiondoa.