Monday, March 30, 2009

Mkutano wa nchi za wanachama wa jumuiya za nchi za Kiaarabu waanza kwa vishindo"Rais wa Sudan audhuria mkutano".

Wapenzi wa soka wapotezamaisha"Fifa yataka maelezo".

Abdjan, Ivory Coast - 30/03/09. Zaidi ya watu 22 wamepoteza maisha baada ya kukanyagana wakati walipotaka kuingia uwanjani kuangalia mpira kati ya timu yao ya taifa na timu ya taifa ya Malawi katika kinyanganyiro cha kugombea nafasi ya kuingia katika fainali ya kombe la dunia litakalo fanyika nchini Afrika ya Kusini mwakani.
Kufuatia mkasa huo,shirikisho la mpira wa miguu duniani,FIFA, limeitaka chama cha mpira cha Ivory Coast, kutoa maelezo kuhusu mkasa huo ambao umesababisha mauaji na majeruhuhi ya watu.
Picha hapo juu ni alama ya shirikisho la mpira wa miguu duniani,ambalo linasimamia michezo yote ya mpira wa miguu duniani na kupanga sheria za mchezo huo.
Picha ya pili wanaonekna polisi wakiwa wamembeba mmoja ya watu alijeruhiwabaada ya kukanyagwa wakati akijaribu kuingia uwanjani kuangaria mechi kati ya timu ya taifa lake na timu ya taifa ya Malawi.
Waziri wa mambo ya ndani aponea chupuchupu.
Mogadishu, Somalia - 30/09/09. Waziri wa mambo ya ndani wa Somalia Abdirahman Ali, amenusurika kupoteza maisha baada ya gari alilo kuwa akisafiria kukanyaga bomu na kulipuka na kupoteaz maisha ya walinzi wake katika kitongoji kimoja katika mji wa Mogadishu.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, jina limehifadhiwa ,alisema inaelekea hili shambulizi lilikuwa limemlenga waziri huyu.
Picha hapo juu, anaonekana mmoja ya wapiganajiwa moja ya kundi linalo pingana na serikali ya Somalia.
Mkutano wa nchi za nchi wanachama wa jumuiya za nchi za Kiaarabu waanza kwa vishindo"Rais wa Sudan audhuria mkutano".
Doha, Katar - 30/03/09. Mkutano mkuu wa kuwakutanisha viongozi na marais wa nchi wanachama wa nchi za Kiaarabu, umeanza rasmi nchini Katar, ili kutafuta ni jinsi gani nchi hizi zita weza kutatua matatizo yanayo zikabili nchi zao.
Katika mkutano huo, ambao umekuwa una malumbano mengi ya kisiasa, hasa baada ya mahakama ya kimataifa inayo shughulikia kesi za uarifu na mauaji iliyipo nchini Uhollanzi kutoa hati ya kukamatwa kwa rais wa Sudan Omar Al bashir, ili ashitakiwe kwa makosa ya jinai.
Wakihutubia mkutano huo kwa nyakati tofauti, viongozi wa Syria na Libya, walisema imekuwa jambo la aibu kwa nchi za Kiaarabu kushindwa kushirikia na baadhi ya nchi wanchama wa nchi hizo kuwa vibaraka wa nchi za Ulaya na Amerika.
Katika mkutano huo, rais wa Misri, hakuudhulia mkutano huo, na kwa mujibu wa chunguzi wa maswala ya kisiasa wanasema hii ni kutokana na hali halisi iliyopo eneo la Mashariki ya Kati.
Picha hapo juu ni ukumbi wa mkutano ambamo viongozi wa nchi za jumuia wanachama wa nchi za Kiaarabu wanakutana.
Picha ya pili anaonekana rais wa Libya, Muammar Ghadaffi, akuongea na viongozi wenzake wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa jumuiya ya nchi Wakiarabu mji Doha.
Picha ya tatu ni rais wa Syria, Bashar al Assad, aliongea na kukumbusha makubaliano ya amani katika eneo la Mashariki ya Kati bado kutimizwa hivyo ni lazima nchi za kiaarabu ziungane kuhakikisha mkataba huo unafikiwa na kukamilishwa.
Picha ya nne, anaonekana rais wa Sudan, Omar al Bashir, akiwasili katika mkutano wa viongozi wa nchi za Kiaarabu unaofanyika nchini Katar Doha.
Chuo cha polisi cha shambuliwa nchini Pakistan.
Rahore,Pakistan - 30/03/09 - Mashambulizi yametokea katika kituo cha kufunzia polisi kilichopo Rahore na kusababisha mauaji na majeruhi ya polisi walio kuwa katika majengo hayo.
Chuo hicho kilikuwa na watu wapatao 800, ambao walikuwa katika chuo hicho kwa ajili ya mfunzo ya polisi.
Hata hivyo kwa msemaji wa serikali na mkuu wa operasheni hiyo Majr General Athar Abbas,alisema makamanda waliweza kuwashinda watu walioteka nyara majengo hayo na baadhi yao walikamatwa na wapo chini ya mikono ya serikali.
Picha hapo juu, wanaonekana na baadhi ya polisi na maafisa usalama wakiwa wamemshikilia mmoja ya mtuhumiwa ambaye anasadikiwa kuwa mmoja ya watu walio leta maafa katika chuo cha mafunzo ya polisi cha Rahore.
Picha ya pili wanaonekana wafanyakazi, zima moto na huduma ya kwanza wakiwa wamembeba mmoja wa watuwalio jeruhiwa wakati wa mashambulizi yaliyo tokea katika chuo cha polisi.
Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari kizimbani nchini Kambodia.
Phnom Penh, Kambodia - 30/03/09.Mahakama ya ualifu wa kivita ya Umoja wa Mataifa iliyopo nchini Kambodia, imeanza kusikiliza kesi ya mauaji ya kimbari yaliyo fanyika mapema miaka ya 1970s, ambapo zaidi ya watu wapatao million 1.7 waliuwawa na baadhi ya viongozi wa kundi la Khmer Rouge.
Majaji watano, wataanza kusikiliza kesi zidi ya aliyekuwa mmoja wa kiongozi, wa kundi la Khmer Rouge, Kaing Guek Eav au kwa jina jingine Duch anashitakiwa kwa kuhusuka na mauaji hayo ya kimbari wakati alipo kuwa mkuu wa jela moja nchini Kambodia.
Kaing Guek Eav au Duch,mwenye miaka 66,anashitakiwa kwa makosa ya kubaka, kuua kwa makusudi,na kutesa watu bila hatia kati ya miaka 1975-1979.
Picha hapo juu, anaonekana, Kaing Guek Eav au Duch, akiwa mahakamani kusikiliza kesi zidi yake zikisomwa.
Picha ya pili anaonekana, Kaing Guek Eavau Duch,akiwa amezungukwa na wanasherika ambao wapo kusikiliza kesi ya mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari zidi ya mteja wao.

No comments: