Sunday, September 19, 2010

Mzozo wa kidini waleta hali ya wasiwasi Indonesia

Mzozo wa kidini waleta hali ya wasiwasi Indonesia. Jakarta, Indonesia - 19/09/2010. Mamia ya waumini wa dini ya Kikristu wame kiuka amri iliyo wekwa na polisi kuwataka wasiudhulia misa kutokana na sababu za kiusalama. Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa kanisa la Batak Christian Church alisema "tunataka haki ya kuomba Mungu, kwani tukikataliwa tutakuwa tunanyimwa haki zetu." Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu ambao walikusanyika pamoja kumuomba Mola.

Nchi za Sahara ya Kusini mwa Afrika zapambana kikamilifu na ukimwi.

New York, UN - 19/09/2010. Umoja wa Mataifa umetoa ropoti ya kuwa nchi zilizopo kusinu mwa jangwa la Sahaha zimejitahidi kupambana na usaambaa wa ugonjwa wa ukimwi.

Kwamujibu wa hahabiri UN zinasema "uambukizwaji wa ugonjwa huo umepungua kwa asilimia 25 katika nchi ambazo zilikuwa zinaongoza kwa kusambaa kwa ugonjwa huo."

UN ilisisitiza haya ni matokeo ya kampeni na mipango mbinu ambayo imesaidia katika kupunguza uasambaaji wa ugonjwa huo.

Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya watu wakiwa katika kampeni ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi.

No comments: