Kiongozi wa Korea ya Kaskazini ampa madaraka ya chama mtoto wake.

Kim Jong -Il, alimteaua mtoto wake huyo Kim Jong-Un ambaye inasemekana alipata elimu yake kwenye nchi za Ulaya Magharibi.
Kiongozi huyo Kim Jong-Il ambaye inasadikiwa ya kuwa hali yake ya afya inazidi kudholota alifanya uteuzi huo hivi karibuni na kutangaza katika mkutano mkuu wa chama chake uliofanyika jiji Pyongyang.
Picha hapo anaonekana kiongozi mkuu wa Korea ya Kaskazini Kim Jong Il akiongoza mkutano mkuu wa chama uliofanyika hivi karibuni.
Picha ya pili wanaonekana wajumbe walioudhulia mkutano ambapo mtoto wa kiongozi wa Korea ya Kaskazini Kim Jong-Un alikabiziwa uongozi.
Waafisa usalama wagundua mpango na njama za magaidi.

London, Uingereza- 29/09/2010. Maafisa usalama wa nchi za Ulaya wamegundua na njama ambazo zilikuwa zimepangwa na makundi ya kigaidi hivi karibuni.
Kwa mujbu wa habari zilizo patikana zilisema "kundi la wapigana la Pakistan lilikuwa limepanga mashambulizi kwenya miji mikuu ya Ujeruman, Uingereza na Ufaransa na hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na mpango huo."
Habari hizo zinasema kundi hilo lilipanga mashambuliza kama ya le yaliyo fanyika nchini India mwaka 2008 Novermba.
Picha hpo juu wanaonekana polisi wakiwa wana chunga mnara maarufu nchini Ufaransa mara baada ya watu kuamriwa waondoke kutokana na tishio la bomu.
Sheria za jumuia ya Ulaya kupambana na Ufaransa.
Paris, Ufaransa - 29/09/2010. Ofisi ya kamishna wa sheria wa jumuia ya Ulaya imeitaka serikali ya Ufaransa kujibu haraka kwanini ilivuluga sheria za umoja wa Ulaya.
Majibu ya barua hiyo yanatakiwa baada ya serikali ya Ufaransa kuwafukuza watu wa jamii ya Waroma hivi karibuni.
Akisisitiza, kamishna wa sheria wa jumuia ya Ulaya Viviane Reding alisema "Ufarance imevunja sheria ambayo ina mruhusu kila raia wa nchi mwanachama wa jumuia ya Ulaya yupo huru kutembea na kuishi katika nchi wanchama wa jumuia hiy."
Hata hivyo msemaji wa serikali ya Ufaransa Bernard Valero ilisema " serikali ya Ufaransa inafanya hivyo ili kukabiliana na uarifu unaondelea katika jamii nchini humo"
Picha hapo juu anaonekana kamishana wa sheria wa jumuia ya Ulaya Viviane Reding akiongea kuhusu swala la raia wa Ulaya wa jamii ya Waroma.

Brussel, Umoja wa Ulaya - 29/09/2010. Maelfu ya wafanyakazi wamendamani ili kupinga ubanaji wa bajeti za serikali na mpango wa kupunguza matumizi.
Akiongea kwa kama mwakilishi wa jumuia ya wafanyakazi nchini Ufaransa Bernard Thibault alisema "tupo hapa kutoka kila nchi mwanacham wa jumuia ya Ulaya ili kunyesha mshikamano wetu kupinga mpango mzima unaochukuliwa na serikali za umoja huu, kwani utaleta matatizo katika jamii."
Maandamano hayo yamekuja baada ya serikali za jumuia ya Ulaya kungalia upya bajeti zake jambo ambalo sekta za umma huenda zikaathirika kwa kiwango kikubwa.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wafanyakazi jijini Manchester wakiandamana kupinga mpango huo.
No comments:
Post a Comment