Monday, September 6, 2010

Paul Kagame aapishwa kuwa rais wa Rwanda kwa muhula wa pili.

Paul Kagame aapishwa kuwa rais wa Rwanda kwa muhula wa pili. Kigali, Rwanda - 06/09/2010. Wanachi wa Rwanda wameshuhudia kwa mara nyingine tena kuapishwa kwa rais aliyechaguliwa baada ya uchaguzi mkuu kumaliziaka tangu kutokea mauaji ya kimbari mwaka 1994. Paul Kagame 52, ameapishwa kuwa rais wa Rwanda kwa mara ya nyingine tena, baada ya kushsinda uchaguzi mkuu iliyo shirikisha vyama vingi. Akiongea baada ya kuapishwa, rais Paul Kagame, alisema "umefikia wakati wa Afrika kujisimamia wenyewe na hakuna kipya cha kujifunza kutoka nchi za Ulaya." Sherehe hizo ziliuzuliwa na vingozi wa nchi jirani, Afrika na wageni wengine waaalikwa. Pichas hapo juu anaonekana rais Paul Kagame akiapa kuwa rais wa Rwanda kwa mara ya pili.

Amani kati ya Waizrael na Wapalestina mjadala tata.
Tel-Aviv, Izrael - 06/09/2010. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Izrael, Avigdor Lieberman, amesema mazungumzo na makubaliano ya kuleta amani kati ya Waizrael na Wapalestina yatachukua miaka au kufikia kizazi kijacho.
Avigdor Lieberman alisema "siamini ya kuwa makubaliano ya amani na Wapalestina yanawezekana kwa sasa na yatachukua miaka na hata kufukia kizazi kijacho."
Maoni hayo ya waziri wa mamba oa nje wa Izrael, yamekuja wakati viongozi wa Palestina na Izrael chini ya usimamizi wa serikali ya Amerika wanakutana ilikutafuta mbini mbadala za kuleta amani kati ya majirani hao.
Picha hapo juu anaonekana waziri wa mambo ya nchi za nje wa Izrael Vigdor Lieberman, ambaye amesema swala la amani halita fikiwa kwa sasa.
Waziri mkuu wa Lebanon akili kufanya makosa.
Beiruti, Lebanon - 06/09/2010. Waziri mkuu wa Lebanon amesema "kuishutumu Syria kuhusika na kifo cha marehemu baba yake Rafik al Hariri, aliyefariki kwa mlipuko wa bomu mwka 2005 kuliletwa na mivutano ya kisiasa."
Saad al Hariri,aliyasema hayo wakati alipo kuwa anaongea na mwandishi wa habari wa Asharq-Awsat lenye makao yake jijini London.
Tangu kifo cha Rafikia al Hariri, Syria imekuwa ikilaumiwa na kushutumiwa kwa kuhusika na kifo chake.
Picha hapo juu waneonekana waziri mkuu wa Lebanon, Saad al Hariri akiongea ana rais wa Syria Bashar al Assad wakati walipo kutana.

No comments: