Tuesday, September 14, 2010

Viongozi wa Palestina na wa Izrael wakutana tena

Viongozi wa Iran wakutana na viongozi wa Afrika. Tehran, Iran - 14/09/2010. Rais wa Iran amezitaka nchi za Afrika "kutafuata uhuru kamili iki kuepukana na uchumi tegemezi ambao unakuja kwa masharti. Rais Mahmoud Ahmadinejad aliyaongea hayo wakati alipokuwa akifungua mkutano uanawakutanisha viongozi wa Afrika na wa Iran ili kujadili ushirikiano wa karibu. Picha hapo huu inawaonyesha viongozi wa Afrika wakiwa na rais wa Irani mara wakati wa mkutano.

Viongozi wa Palestina na wa Izrael wakuatana tena.
Sharm el Sheikh. Misri-14/09/2010. Viongozi wa Izrael na Palestina wamekutana leo ili kwa mara ya pili tangu kuanza kwa mazungumzo kujadili swala zima la usalama la eneo hilo.
Viongozi hao, Benjamin Netanyahu Waizrael na Mahmud Abbas wa Wapalestina walikutana wakati serikali ya Amerika ikiwa inasisitiza kuwepo na mazungumzo yatakayo fikia fuaka.
Mazungumzo hayo yalisimamiwa na waziri wa mambo ya nje wa Amerika Bi Hillary Clinton.
Picha hapo juu wanaonekana waziri mkuu wa Izrael Benjamini Netanyahu akipeana mkono na kiongozi wa Wapalestina Mahmud Abbas mara baada ya mkutano.

No comments: