Fidel Castro ataadharisha dunia na nguvu za nyuklia.
Havana, Kuba - 05/09/2010. Rais wa zamani wa Kuba Fidel Castro, ameitaadhalisha dunia kuhusu hali iliyopo ambayo nchini zenye nguvu za kinyuklia zitaendelea kusukumana na Iran basi huenda zikaamua kutumia nguvu za kinyuklia jambo ambalo litahatarisha dunia kwa ujumla.
Fidel Castro 84, akihutubia mbele ya watu wapatao 11,000 alisema " ikiwa Amerika na washirki wake wataendele kuiwekea Iran vikwazo kutokana na nchi ya Iran kutokubaliana na matakwa yao ( Amerika) na washiriki wake kunaleta wakati mgumu na hivyo wakati umefika watu wote duniani washirikiane kuzuia matumizi ya nguvu za kinyuklia yasitumike."
Picha hapo juuanaonekana Fidel Castro akiwasalimia baadhi ya watu waliohudhulia wakati wa hotuba yake.
Sunday, September 5, 2010
Fidel Castro ataadhari dunia na nguvu za kinyuklia.
Bei ya vyakula yaleta mashaka nchini Mozambili.
Mozambiki, Msumbiji - 05/09/2010. Maelfu ya wanachi wa Mozambiki wamepambana na polisi wakati wa maandamano ya kupinga kupanda bei ya vyakula nchini humo.
Kwa mujibu wa msemaji wa shirika la msalaba mwekundu polisi walitumia risasi za mipira na mabomu ya kutoa machozi ili kuwasambaza watu waliokuwa wanaandamana.
Msemaji huyo alisema "kutokana na maandamano hayo viongozi wa serikali wamakuwa wakiwatembelea wananchi na kueleza hali halisi ili kupunguza ghasia."
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya watu wakiwa wapo katika mstari ili kununu chakula.
Ugonjwa wa kipindupindu waleta maafa Afrika ya Kati.
Msemaji wa wizara ya afya ya Chad Mohamat Mamadou alisema "hadi kufikia sasa kuna watu wapato 600 wamepata maradhi hayo ya kipindupindu."
Msemaji huyo wa wizara ya afya ya Chad, alisisitiza kwa kuongeza ya kuwa karibu eneo zima la Afrika ya Kati limekumbwa na ugonjwa huo.
Ugonjwa wa kipindupindu, humsababisha mtu kuarisha na kupungua maji mwilini na hata kusababisha kifo.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wagonjwa wakiwa wamelazwa katika hospitali moja nchni Chad kwa ajili ya kupata matibabu.
Posted by
Kibatala
at
Sunday, September 05, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment