Thursday, September 23, 2010

Baraka Obama asisitiza ushirikiano kutatua mgogoro wa Mashariki ya Kati.

Baraka Obama asisitiza ushirikiano kutatua mgogoro wa Mashariki ya Kati.

New York, Amerika- 23/09/2010. Rais wa Amerika amezitaka jumuia za kimataifa kushirikiana ili kuleta amani kati ya Waisrael na Wapalestina.
Rais Baraka Obama aliyasema hayo mbele ya viongozi na wakuu wanchi walioudhulia kikao cha 65 cha umoja wa Mataifa "yakuwa kama tukishirikiana kwa pamoja katika kutatua mgogoro kati ya Wapalestina na Waizrael, basi kwenye mkutano mwingine wa umoja wa mataifa 2011 tutakuwa na mwanacham mpya wa umoja wa mataifa ambayo itakuwa Palestina."
Vilevile rais Obama, alisema mlango uko wazi kwa mazungumzo na Iran ikiwa nchi hiyo itaonyesha nia".
Picha hapo juu wanaonekana viongozi wakimsikiliza katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon akiwakaribisha kabla ya kuanza kikao cha 65 cha umoja wa Mataifa.
Picha ya pili anaonekana rais wa Amerika Baraka Obama akisisitiza baadhi ya mipango wakati alipo akihutubia viongozi kwenywe mkutano wa 65 wa Umoja wa Mataifa.
Rais wa Iran ashambulia sera za kibepari.
UN,New-York - 23/09/2010. Rais wa Iran imeitaka dunia kutangaza mwaka 2011 kuwa mwaka wa kuhangamiza na kuharibu siraha zote za mabomu ya kinyuklia kote duniani.
Rais Mahmoud Ahmadinejad alisema ya kuwa "dunia haitakuwa na usalama ikiwa siriha za nyuklia hazita agamizwa kwani zinakwenda kinyume na maadili ya Mitume ambao walikuja kutangaza amani na upendo"
Kwa kuongeza, rais Ahmadnejad alitaka "heshima lazima iwepo katika dini zote na vitabu ambavyo vinatumika katika kufundishia imani ya kumwamini Mungu" Rais Ahmadinejad, alisema ya kuwa" mashambulizi ya Septemba 11 yalikuwa ni mipango ya ambayo ilipangwa kuhujumu uchumi wa Amerika ili kusaidia mbinu za mabepari"
Picha hapo juu anaonekana rais wa Iran, akihutubia kwenye mkutano wa 65 wa Umoja wa mataifa jijini New York.

No comments: