Monday, November 1, 2010

Wabrazil wamchagua rais mwanamama kuingoza nchi yao

Wabrazil wamchagua rais mwanamama kuiongoza nchi yao

Rio De Janeiro, Brazil - 01/11/2010. Wananchi wa Brazil wamemchagua kwa mara ya kwanza rais mwanamama kuiongoza nchi yao.
Dilma Vana Rousseff, 62, alitangazwa kuwa mshindi kwa kupata asilimia kura 55.5% kwa kumshinda mpinzani wake Jose Serra aliyepata asilimia 44.5 za kura zpte zilizo pigwa.
Akiongea mara baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Brazili, Rousseff alisema "kama nilivyo haidi nitatekeleza yale yote na hasa kupigana na ufukara na umasikini na kuakikisha nchi yetu inakuwa kimaendeleo."
Dilma Rousseff, anatarajiwa kuapishwa kuwa rais mapema mwaka 2011, na kuchukua madaraka ya rais wa sasa Luiz Inacio Lula da Silva.
Picha hapo juu ni ya bendera ya Brazil nchi ambayo kwa mara ya kwanza imemchagua rais mwanamke kuiongoza nvhi hiyo.
Picha ya pili anaonekana kulia Dilma Vana Rousseff, akiwa na wadau wakipata ghahawa wake wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais hivi karibuni.
Mizigo yote kufanyiwa ukaguzi wa hali ya juu.
Sanaa, Yemen - 01/11/2010. Serikali za nchi tofauti duniani zimeanza kufikiria njia mpya ya kukabiliana na mbinu za makundi ya kigaidi kwa kuangalia mbinu gani watatumia kuimarisha ukaguzi wa mizigo katika viwanja vyote vya kimataifa.
Uamuzi huo wa kuongea usalama na ukaguzi wa mizigo, umekuja baada ya kundi la kigaidi chini uongozi wa Alqaeda waliweza kupitisha mizigo ambayo ilikuwa imebeba mabomu ambayo yangetumika kulipua na kuaribu maeneo yaliyo kusudiwa na kundi hilo.
Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa shirika la ndege la Ryanair alisema " kufuatia hali ya tukio lililo tokea Yemen litasababisha hali ambayo wasafiri watabidi waizoee, hii ni kwa ajili ya usalama wa abiria na jamii kwa jumla."
Picha hapo juu zinaonekana baadhi ya ndege za kubebea mizizigo zikiwa zimepaki tayari kwa kubeba mizigo ambayo kuanzia sasa mizigo yote itafanyiwa ukaguzi wa hali ya juu.

No comments: