Tuesday, May 17, 2011

Luis Moreno Ocampo ataka Muammar Gaddafi afikishwe mahakamani.

Den Haag, Uhollanzi , 16/05. 2011. Wakili wa mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi zidi ya kukiukwa haki za binadamu, amewaomba majaji wa mahakama hiyo watoe rukhsa ya kukumatwa kwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, mtoto wake wa pili Saif al Islam na mkuu wa usalama wa taifa Abdullah Senussi. Luis Moreno Ocampo, aliyasema haya mbele ya waandishi wa habari, kwa kusema " upo ushaidi wa kutosha ya kuwa haki za binadamu zimekiukwa na serikali ya kiongozi huyo tangu kuanza kwa mvumo wa kutaka aaondoke madarakani." Akiwakilisha na kuonyesha kurasa zipatazo 74 ambazo ameziwakilisha katika mahakama jijini Den haag (Hague), na zimeelezea ushaidi wa kutosha wa kukiukwa kwa haki za binadamu nchi libya na uongozi wa Muammar Gaddafi. Muamar Gaddafi ambaye ametawala Libya zaidi ya miaka 40, amekumbwa na wimbi lililotokea kwemye maoenao ya Afrika ya Kaskazini baada wanachi kutaka demokrasi na mageuzi ya kisiasa. Mkurugenzi mkuu wa IMF akataliwa dhamana na mahakama. New York, Marekani - 16/05/2011. Halimu wa mahakama jijini New York amemkatalia kumpa dhamana mkurungenzi mkuu wa shirika la fedha duniani (IMF) Internaltional Monetary Fund. Mkurugenzi hyo kwa IFM, Dominik Strauss-Kahn, amekataliwa dhamana hiyo na jaji kwa madai huenda akaondoka nchini humo kwa kutumia ndege. Dominik Strauss anakabiliwa na shitaka la kutaka kumbaka mmoja wa mfanyakazi wa hotel aliyo kuwa amelala na anatarajiwa kurudi mahakamani Mei 20.

1 comment:

khodri said...

good post :)

visit my blog ,

http://suasanapekanbaru.blogspot.com/