Sunday, May 1, 2011

Papa John Paul afanywa kuwa mteule.

Vatican City,Vatican - 01/05/2011. Kanisa Katoliki limetangaza rasmi yakuwa aliye kuwa Papa John Paul wa Pili amekuwa mteule rasmi. Kufanywa huko kuwa mteule kumekuja baada ya ushahidi kutolewa ya kuwa alikuwa ni mtu wa aina ya pekee. Mmoja ya watu waliotoa ushahidi huo, ni sista wa Marie Simon Pierre ambaye alisema yakuwa "alitibiwa na Papa John Paul kupitia maombi." Sherehe hiyo iliudhuliwa na viongozi wa serikali na wakidini akiwemo rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na mkewe.

1 comment:

Christian Sikapundwa said...

Tunamshukuru Mungu na waumini wa Roman Catholic kwa sala zao,wengine walifunga Novena kwa ajili ya Papa Jhn Paul wa II kuwa mwenye Heri.

Ana haki ya kuwa mwenye Heri kutokana na matendo yake na huduma zake kwa kondoo zake kama mchungaji.

Nakushukuru sana Habari na Matukio kwa kazi nzuri endelea hivyo kucheza na mtandao.