Rais wa pili wa Zambia Fredrick Chiluba afariki dunia.


Lusaka, Zambia 18/06/2011. Aliye kuwa rais wa pili tangu Zambia kupata uhuru na kuchaguliwa kupitia kura zilizo shirikisha vyama vingi nchini humo amefariki dunia.
Fredrick Jacob Titus Chiluba 68, ambaye ametawala Zambia kwa muda wa miaka kumi na kubadilisha muundo mzima wa serikali uliyo kuwa umewekwa na rais wa kwanza wa Zambia Keneth Kaunda.
Akitangaza kufariki kwa Fredrick Chiluba, rais wa sasa wa Zambia Rupiah Banda alisema " aliyekuwa rais wetu Fredrick Chiluba amefariki dunia mapema leo 18/06/2011, na kwaniaba ya serikali napenda kutoa salamu za rambirambi kwa familia, ndugu marafiki na jamaa wote."
Hayati Fredrick Chiluba alisifiwa sana kwa kuleta mageuzi ya kisiasa hasa na nchi za Ulaya Magharibi.
Ujerumani na Ufaransa wakubaliana kuisaidia Ugiriki.

Berlin, Ujerumani - 18/06/2011. Viongozi wa serkali ya Ujerumani na Ufaransa wamekubaliana kwa pamoja kuisaidia Ugiriki kifedha ili kuinua uchumi wa nchi hiyo.
Kansela wa Ujerumani Angel Merkel na rais wa Ufaransa Nicalas Sarkozy walikubaliana bila kipingamizi kuipa Ugiriki kwa kusema " wakati huu ni wakati wakuonyesha ushirikiano wetu."
Kufuatia myumbo wa kiuchumi waziri mkuu wa Ugiriki, alibadilisha baraza la mawaziri ili kuleta msimamo mmoja ndani ya serikali.
Ugiriki ambayo ianayumba kiuchumi,inatakiwa kupewa mkopo wa kiasi cha 12 billioni ili kuinua uchumi wa nchi hiyo.
Marekani na Taliban wakutana kujadili usalama wa Afghanistan


Rais Hamid Karzai alisema " wakuu wa siasa na wakijeshi kutoka serikali ya Marekani wamekuwa wakiongea na viongozi wa kundi la Taliban ."
Hivi karibuni waziri wa ulinzi, Robert Gates alisema " huenda kukawa na amzungumzo na Taliban, ili kuleta suruhisho kupitia siasa."
Mazungumzo hayo na kundi la Taliban yamekuja huku serikali ya Marekani ikiwa inajiandaa kuondoa majeshi yake taratibu, tayari kukabidhi madaraka kwa serikali ya Afghanistan ifikapo mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment