Friday, June 29, 2012

Marais wa Somalia wakutana UAE - Dubai.

Mohamed Morsi aapishwa rasmi kuwa rais wa Misri.

Kairo, Misri - 29/06/2012. Aliyekuwa mshindi wa uchaguzi wa Urais nchini Misri atapishwa rasmi kuwa rais wa nchi hiyo kesho Jumamosi.
Rais Mohamed Morsi  akiongea mbele ya watu walio kuja kumsikiliza siku moja kabla ya kuapishwa na kuhaidi ya kuwa ataijenga nchi kwa kufuata misingi ya katiba na kisisitiza ya kuwa "hakuna mwananchi ambaye atakuwa juu ya sheria na sitaogopa mtu isipokuwa Mungu.
"Nitalinda nchi yangu na mkipaka yake na kuhakikisha safari  ya kuwa serikali ya kiraia inafikiwa."
Hotuba ya rais Mohamed Morsi imeonyesha kuwa hali ya jeshi kuchukua madaraka kama ilivyo fikiriwa itakuwa ngumu kwa kiasi kikubwa.

Nchi za jumuiya ya Ulaya zachukua hatua ya mbadala ilikuinua uchumi

Brussels, Ubeligiji - 29/06/2012. Viongozi wa jumuiya ya nchi za Ulaya wamekubaliana kwa pamoja kuinua benki zao kwa kuzipatia fedha ili kusaidi kuinua biashara  na uchumi.
Viongozi hao ambao walichukua karibu usiku mzima nakukubaliana kimsingi ya kuwa ipo haja ya kuinua hali ya mtiririko wa fedha ili kusaidi mwamko wa kiuchumi na kibiashara.
kansela Angela Merkel ambaye nchi yake ilikuwa inaaonekana kama ni kikwazo hapo awali alisema  " Nimeridhika na matokeo ya mkuno huu japo ulichukua muda mferu, lakini matokeo ya mkutano huu ni mazuri kwa nchi zote wanchama wa nchi za jumuiya ya Ulaya."
Makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano huo yameleta matumani makubwa kwa nchi za ispania na Itali nchi ambazo hali zake za kichumi fedha zilikuwa katika hali ya kuyumba.


Kampuni ya Nestle yalaumiwa.

London, Uingereza - 2012. Kampuni inayo shughulikia vyakula ya Nestle imelaumiwa kwa kutofanya uchunguzi mazingira ya kazi ambayo yanahusisha watoto wadogo.
Habari zilizo tolewa hivi karibuni na shirika linalo shughulikia na kusimamia ufanyaji wa kazi na usawa ( Fair  Labor Association - FLA) zimesema, " Nestle hakutilia maanani ni kwa jinsi gani  mazao yanayo uzwa na kuzalishwa na wakulima yana patikana kwa namna gani, kwani kuna ushaidi ya kuwa kuna watoto 1.8 million ambao wanafanyishwa kazi katika uzalishwaji wa mazo ya kampuni ya Nestle,  hasa  mashamba ya kakao yaliyopo Afrika ya Magharibi."
Nestle nikampuni kubwa duniani ambayo inajihusisha  na uzalishaji wa chokoleti duniani
hata hivyo makamu wa rais wa kampuni hiyo Jose Lopez alikanusha kwa kusema " Hatutumi watoto katika uzalishaji na tunapinga kitendo hicho katika nyanja  zetu zote za uzalishaji wa mazao ya Nestle. na huwa tunahakikisha ya kuwa hakuna watoto wanao tumiwa katika uazlishaji hasa katika zao la kakao kama ilivyo ripotiwa. na huu ndiyo msimamo wetu" 

Wafanyazi wa kutoa misaada watekwa nyara nchini Kenya.

Nairobi, Kenya - 29/07/2012. Wafanyakazi wa shrika linalo toa msaada wa kibinadamu wametekwa nyara nchini Kenya katika kambi ya wakimbizi iliyopo Dadaab.
Masemaji wa Polisi nchini Kenya  Philp Ndolo alisema " raia wanne wa kutoka Kanada, Pakistan, Norway na Phillippin walitekwa nyarawakati wakiwa maeneo ya kambi ya wakimbizi ya Dadaab baada ya gari walilikuwa wakisafiria kushambuliwa."
Utekwaji nyara wa wafanyakazi wa mashirika ya kigeni wamekuwa wakifanya kazi za kuhudumia wakimbizi katika eneo hilo kwa mashaka na kusababisha baadhi ya mashika kusimamisha utoaji misaada katika eneo hilo.

Marais wa Somalia wakutana UAE - Dubai.

Dubai, United Arab Emirates - 29/06/2012. Marais wa Somaliland na Somalia wamekutana Dubai kwa mara ya kwanza tangu kuvunjika kwa muungano wa nchi hizo miaka karibuni 20 iliyopita.
Rais Sheikh Sharif Ahmed na Ahmed Silanyo walikutana  kufuatia mkutano wa kwanza  wa wawakilishi wa nchi hizo  uliyofanyika  nchini Uingereza hivi karibuni.
Lengo la kuaza kwa mazungumzo hayo ni kukubaliani nchi hiyo kuwa moja kama Somalia, tangu kujitenga kwa Somaliland 1991, kufuatiqa kuangushwa kwa serikaliaki ya rais Mohmed  Seyyid Bare.
Rais wa Syria ahaidi kutoruhusu nchi nyingine kumwekea msharti.

Damascus, Syria - 29/06/2012. Rais wa Syria amehaidi ya kuwa hataruhusu na kukubali nchi yoyote kuiwekea masharti serikali yake katika harakati za kutaka kuleta amani nchi humo.
rais Bashar al Assad alisema " matatizo yaliopo nchini Syria ni ya wanachiwa Syria na ni ya ndani ya Syria, na  hayahusiani na nchi za kigeni kama nchi hizo zinavyo dai na Wasyria ndiyo watakao maliza  hili suala bila  msukumo au masharti kutoka nchi nyingine."
Bashar al Asssad amefanya mazungumzo hayo kwa mara ya kwanza tangu vurugu na kutokuwepo na amani  nchi Syria kuanza jambo ambalo linaaminika kuipilekea nchi hiyo kuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

No comments: