Sunday, March 29, 2009

Rasi wa Brazil,azilaumu nchi tajiri kwa mporomoko wa uchumi.

Rais wa Brazil, azilaumu nchi tajiri kwa mporomoko wa uchumi.

Sao Paulo,Brazil -28/03/09. Rais wa Brazil, Lula da Silva, amezilaumu nchi za tajiri duniani kwa kuleta hali mbaya ya kiuchumi, wakati alipo kutana na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown, ambaye yupo nchi Brazili kwa ziara ya kiserikali.
Rais Lula da Silva, alisema yakuwa wazungu wenye macho ya bluu, ndiyo wakulaumiwa, kwa kusababisha mporomoko wa uchumi, kwani hakuna, watu weusi wala waindi ambao wameleta maafa haya ya kiuchumi duniani, na hivyo nchi masikini zisilazimishwe kulipa hasara iliyo sababishwa na watu hawa wenye machoi ya bluu.
Rais, Lula, aliongezea kwa kusema ya kuwa, mporomoko wa uchumi duniani, umeweka wazi ni jinsi gani baadhi ya watu wanavyo fikiria wao ni bora na kumbe sivyo.
Hata hivyo waziri wa Uingereza, Gordo Brown, alisema hivi sasa ni wakati wa kushirikiana kutafuta njia ya kutatua matatizo haya ya kiuchumi.
Picha hapo juu, anaonekana, rais wa Brazil, Lula da Silva, akiongea na wandishi wa habari, mara baada ya mkutano na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown.
Picha ya pili, anaonekna waziri mkuu wa Uingereza, akimwangalia kwa makini, rais wa Brazili, wakati akiongea kuhusu hali halisi, kwa nini uchumi umeporomoka.
Urussi kushirikiana na NATO kuijenga Afghanistan.
Moscow, Urussi-28/03/09.Serikali ya Urussi, imesema ipo ytayari kushirikiana na NATO,ili kuijenga Afghanistan.
Akisema hayo , waziri wa mambo ya nje wa Urussi,Sergei Lavrov,alisema haya wakati wa mkutano unaozungumzia hali halisi ya Afghanistan, uliofanyikia Mocsow, na kusema ya kuwa serikali ya Urussi inatizama kiundani ni jinsi gani itashirikiana na NATO, ili kuijenga upya Afghanistan.
Picha hapo juu ni baadhi ya wanchi wa Afghanistan, wakiwa katika moja ya shamba lao wakiangalia matunda, ambayo huwa wanauza na kupata kipato cha kila siku, lakini kutokana na zao hili, ndimo madawa ya kulevya hutengenezwa, na jumuia ya kimataifa imekuwa inatafuta njia mpya ya kuijenga kiuchumi Afghanistan, ili wananchi wasitegemee zao hili.
Jacob Zuma,azilaumu nchi za Magharibi.
Johannesburg,Afrika ya Kusini-28/03/09.Mwenyekiti wa chama tawala cha Afrika ya Kusini Jacob Zuma, amezilaumu nchi za Magharibi, kwa kushindwa kuisaidia Zimbabwe., kwa kudai ya kuwa ni njia moja wapo ya kushinikiza rais wa Zimbabwe ili akubaliane na mabadiliko.
Jacob Zuma, alisema hii si sawa , kwani rais Robert Mugabe amekuwa madarakani, kwa kipindi kirefu kama rais wa Zimbabwe, na hivyo sivyo kama wanaovyo ona nchi za Magharibi, bali hali ya wanchi wa Zimbabwe ndito ya muhimu, kwani katika kupiga kura kila mwananchi alipiga kura, na siyo kila mwananchi alipiga kura kwa rais Mugabe au waziri mkuu ,Tsvangirai.
Hata hivyo , Jacob Zuma, alisema kuukubali kushirikiana kwa rais Mugabe na Tsvangirai,ni mwanzo wa mageuzi yatakayo waletea wa Zimbabwe manufaa na Maendeleo.
Picha hapo juu, anaonekna , Jzcob Zuma ,akiwa kavalia vazi la kiasili la Kizulu, wakati wa sherehe za kuazimiasha kumbukumbu ya Mfalme Shaka Zulu.
Picha ya pili ni viongozi wa Zimbabwe, rais Robert Mugabe na waziri mkuu, Morgen Tsvangirai wakipeana mkono mara baada ya kukubaliana kushirikiana kuongoza serikali na wananchi wa Zimbabwe kwa pamoja.
Sudan ya shuku Israel kwa mashambulizi nchini mwake.
Kartoum,Sudan-28/03/09. Serikali ya Sudan,imesema huenda mashambulizi yaliyo fanywa katika eneo moja lililopo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, lilifanywa na Israel na kupoteza maisha ya watu 40.
Mashambulizi hayo yalioyo tokea mapema mwezi wa kwanza na wapili mwaka huu 2009.
Hata hivy msemaji wa serikali ya Sudan, alisema yakuwa mashamulizi hayo mwanzo yalizaniwa yamefanywa na Amerika, lakini , baadaye serikali ya Amerika ilikanusha madai hayo.
Aliendelea kwa kusema, msemaji huyo wa serikali ya Sudan, yakuwa bado wanachunguza kwa makini, lakini huenda mashambuliz haya yalifanywa na Israel,kwani hapo awali Israel ilidai yakuwa kua siraha, zina pitia Sudan kupelekwa Ukanda wa Gaza.
Picha hapo juu, inaonyesha ramani,ni jinsi gani mashambulizi yalivyo vyanywa ikiwa ni Israel iliyafanya.
Picha ya pili ni ya moja ya gari, ambalo lilishamuliwa na makombora ya liyoshambulia eneo lililopo Kaskazini Mashariki mwa Sudan, bilia serikali ya Sudan kufahamishwa.
Japan yawa tayari kuzuia chombo cha anga cha Korea ya Kaskazini.
Tokyo, Japan-28/03/09.Serikali ya Japan, imepitisha amri ya kulitaka jeshi la ulinzi wa anga kujiandaa kuzuia chombo cha anga kitakacho rushwa na Korea ya Kaskazini.
Uamuzi huo umekuja mara baada ya Korea ya Kaskazini kutangaza ina mpango wa kurusha chombo chake angaani kati ya Aprili 4 na 8 mwaka huu 2009.
Uamuzi huu unakuja baaada ya serikali ya Japan, kuona ya kuwa kitendo cha Korea ya Kusini, kutaka kurusha roketi hiyo ni hatari kwa Japan.
Picha hapo juu, inaonekana meli ya kijeshi ya Japan, iliyo na mitambo tayari kuzuia chombo cha anga cha Korea ya Kaskazini.
IAEA-Shirika linalo shughulikia nguvu za nyuklia duniani la vutana kupata kiongozi mpya.
Vienna, Austria - 28/03/09.Shirika la umoja wa Mataifa linalo shughulikia maswala ya nguvu za nyuklia limeshindwa kumpata mkurugenzi wake mkuu, katika uchaguzi uliochukua mzunguko mara tano kwa kipindi cha siku mbili.
Uchaguzi huo unafanyika,ili kumpzta mkurugenzi mpya, atakaye ongoza shirika hilo , baada ya mkurugenzi wa sasa Mohamed El Baredei ambaye anatarajiwa kujiuzuru.
Wagomea waliogombea kuwa wakurugenzi wa shirika hilo,Abdul Samad Minty wa Afrika ya Kusini na Yukiya Amano, hawakuweza kushinda baada ya kushindwa kupata kura zinazo hitajika ili kuwa mkurugenzi wa shirika hilo.
Picha hapo juu, ni ya mkurugenzi wa sasa wa shirika linalo shughulikia nguvu za nyuklia, Mohamed El Baredei,ambaye anatajariwa kujiuzuru kutoka madarakani.

No comments: