Ufaransa na Ujerumani kudumisha ushirikiano zaidi.
Berlin, Ujerumani 12/03/09. Kansella wa Ujerumani, Angela Merkel, amempongeza rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, kwa uamuzi wa nchi yake kurudi kikamilifu katika jumuia ya ulinzi ya NATO.
Kansella,Angela Merkel, aliyasema haya, wakati alipo kutana na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, ambaye yupo ziarani nchini Ujerumani,ili kujadili ni jinsi gani nchi hizi mbili zitashirikiana zaidi.
Picha hapo juu wanaonekana rais, wa Ufaransa,Nicolas Sarkozy, akikaribishwa mjini Berlini na Kansella, Angela Merkel mapema leo.
Madaktari na muuguzi watekwa nyara Darfur.
Darfur, Sudan-12/03/09.Waanyakazi watatu wa shirika la madakitari wa sio na mipaka wametekwa nyara na watu wasiojulikana.
Wafanyakazi hao wanao tokea, Kanada na Itali, waliingiliwa katika ofisi zao zilizopo,Saraf Umra na kuchukuliwa kwa nguvu huku mitutu ya bunduki ikiwa nyuma yao.
Kuafuatia hali ya usalama kuwa mbaya katika eneo hilo la Darfur, shirika hilo limeamua kuamishia ofisi zake mjini Kartoum.
Picha hpo juu, linaonekna moja ya gari, lililo kuwa likitumiwa na ma wafanyakazi hao waliotekwa nyara mapema leo.


No comments:
Post a Comment