Sunday, March 8, 2009

Dunia ina siku 100 kabla ya kuangamia "Mwana wa Malkia".

Wacko Jacko kupanda jukwaani tena kufanya vitu vyake.

London Uingereza - 08/03/09.Bingwa wa muziki wa Pop duniani Michel Jackson, ametangaza ya kuwa atafaya onyesho lake la mwisho la kimziki nchini Uingereza wakati wa kipindi cha baridi kuisha barani Ulaya (Summer time).
Akiongea hayoa mbela ya wapenzi wake wa muziki, Michel Jackson, malisema ataimba nyimbo ambazo wapenzi wake wanazipenda na roho za wapenzi zitakongwa hadi mwisho wa onyesho hilo.
Kwa mujibu wa mtayarishaji wa onyesho hilo, Rob Hallet,alisema tiketi zitauzwa kwa kwa bei ambayo kila mpenzi wa Michael ataweza kununua.
Alisisitiza kwa kusema tiketi zitaanzia paudi 50 hadi Paundi 75.
Picha hapo juu anaonekana, bingwa wa muziki wa Pop, Michael Jackson akifanya vitu vyake katika muziki wa Thriller, muziki ambao ulimletea sifa kubwa ulimwenguni.
Picha ya pili, naonekana bingwa wa muziki wa Pop, Maichael Jackson akiwaaga wapenzi kwa kuwaonyesha vidole viliwili, mara baada ya kutangaza uamuzi wake wa kufanya onyesho la mwisho mjini London Uingereza, wakati wa kipindi cha jua.(Summer time) mwaka huu 2009.
Dunia ina siku 100,kabla ya kuangamia." Mwana wa Malkia
London, Uingereza - 08/03/09. Mwana wa Malkia Elizabeth wa Uingereza, Prinsi Charles, atauhutubia viongozi na wafanya biashara jijini Rio de Jeneiro nchini Brazil wiki ijayo.
Katika mkutano huo, Prinsi Charles, atawaelezea viongozi hao na wafanya biashara ya kuwa tunazo siki chache kuikomboa dunia katika janga la ukame, na uaharibifu wa mazingira.
Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya ufalme, Prinsi Charles atasisitiza saana kufanya kila njia kuikomboa dunia, kwai kwa mtazamo wake tunazo kama siki 100, kabla ya mazingira ya dunia kuaribika.
Akiwa ziaran katika nchi za Amerika ya Kusini, atatembela nchi za Chile,Equado na kisiwa cha Galapogos.
Picha hapo juu ni ya Prinsi Charles, ambaye anatatarajiwa kuwaomba viongozi wa duinia kuikomboa dunia, ambayo mazingira yake yapo hatarini.
Morocco ya vunja uhusiano na Iran"Imani ya Madhehebu yaleta mgogoro".
Rabat,Morocco - 08/03/09. Serikali ya Morocco imefunga uhusiano wa kibalozi na serikali ya Iran, kwa kile kinacho daiwa na serikali ya Morocco, ya kuwa serikali ya Iran, kuingilia maswala ya ndani ya nchi.
Kwa mujibu wa msema wa wizara ya mabo ya nje wa Morocco alisema, uhusiano na Iran, umevujwa tangu ijumaa 06/03/09.
Uhusiano wa Morocco na Iran umekuwa wakaeribu saana tangu mwanzo wa miaka ya 1990.Hadi hivi karibuni, baada ya yakuonekana ya kuwa kuana njama za kuendeleza wa Uislaaam wa Kishia nchini Morocoo, nchi ambapo nchini Morocco waumini waliowengi ni wa Waislaaam wa Suni.
Picha hapo juu ni ya bendera ya Iran, nchi ambayo ina waumini wengi Waislaam Washia.
Picha ya pili, ni bendera ya Morocco, nchi ambayo ina waumuni wengi Waislaam Suni.
Ajali ya waziri mkuu wa Zimbabwe ni ajali kama ajali nyingine."Ubalozi wa sema"
Harare,Zimbabwe - 08/03/09.Ajali ya gari iliyokuwa imembeba waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai, kugongwa na lori la mizigo la USAIDA (United State Agency For International Development), haikuwa ajali ya kupangwa, ilikuwa ajali ya kama ajali nyingine zinavyotokea.
Kwa mujibu wa ofosi za ubalozi wa Uingereza, mjini Harare, zinasema lori hilo la mizigo, lilikuwa ni moja ya malori ya nayo tumiwa na serikali ya Uingereza kwa kushirikiana na serikali ya Amerika katika kutoa msaada kwa jamii.
Ajali hiyo ambayo ilitokea siku ya ijumaa, ilisababisha kifo cha mke wa waziri mkuu bi Suzan Tsvangirai, na waziri mkuu Morgan Tsvangirai na dereva wa gari hilo kupata majera kiasi.
Picha hapo juu, linaonekna gari lilolo mbeba, waziri mkuu wa Zimbabwe,likiwa libebinuka matairi juu,mara baada ya kupata ajali ya kugongwa na lori.
Picha ya pili, ni marehemu Bi Suzan Tsvangirai,amabye alipoteza maisha katika ajali ya gari, baada ya kugongwa na roli la USAID.
Picha ya tatu wanaonekana, waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai akicheza ngoma za asili na mkewe marehemu bi, Suzani wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe.
Picha ya tatu, anaokana rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, akiongea na waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, wakati alipo kwenda kumtembelea hospitali.
Amerika na Talibani kukaa meza moja.
Washington,Amerika - 08/03/09. Serikali ya Amerika huenda ikaanza kuongea na baadhi ya viongozi wa kundi la Taliban, ambao wanamwelekeo wa kati.
Akiyaongea hayo rais , Baraka Obama, aliyasema hayo, kabla ya makamu wa rais wa Amerika , Joe Biden, kuanza ziara ya katika bara la Ulaya, ili kukutana na viongozi kujadili hali ya Afghanistan.
Wakati huo huo, ofisi za ilikulu ya Amerika, zimesema, rais Baraka Obama, huenda akafanya ziara ya kiserikali nchini Uturuki mnamo mwezi wa nne mwaka huu 2009.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Amerika, Baraka Obama, akiongea hivi karibuni na waandishi wa kuhusu hali msimamo wa serikali yake hasa katika maswala yanoyo sera za kigeni.
Picha ya pili wanonekana wapiganaji wa jeshi la Amerika wakiwa wamepumzika, huku wakijipoza kwa sigara, baada ya ya kazi ngumu ya kupambana na kundi la Taliban nchi Afghanistan.

No comments: