Mawaziri wa fedha wakutana kujadili hali ya uchumi wa dunia.
London,Uingereza - 15/03/09.Mawaziri wa nchi 20 zenye uchumi mzuri, wamekutana nchini Uingereza li kujadili hali halisi ya kiuchumi na kuhaidi kuokoa dunia na tatatizo ya kifedha.
Kwa mujibu, wamkutano huo,mawaziri hao wameamua kwa pamoja yakuwa watasaidiana kuinua masoko ya dunia li kuepuka zaidi matatizo ya baadaye.
Picha hapo juu wanaonenaka mawaziri wa fedha wa nchi 20, zenye uchumi mzuri walipo kutana mjini London ili kujadili hali halisi ya kiuchumi ya duniani na kutoa uamuzi bora.
Hali ya siasa, nchini Madagasca ni tete"Rais akubali kura za maoni".
Antananarivo, Madagasca - 15/03/09.Rais wa Madagasca, Marc Ravalomanana, ametangaza ya kuwa yuko tayari kuitisha kura ya maoni nchini humo, ili kumaliza mzozo wa kisiasa uliopo nchini humo.
Rais, Marc Ravalomanana, aliyasema hayo mbele ya watu wapatao 5,000,kwenye ikulu ya nchi hiyo.
Hata hivyo , kiongozi wa wa chama cha upinzani nchini humo, Andy Rajoelina,amemtaka rais Marc Ravalomanana, aachie madaraka, kwani amshindwa kuongoza nchi kwa kufuata misingi ya kidemokrasia, na anaongoza nchi kinyume na sheria na kuwa dikteta.
Picha hapo juu wanaonekana,baadhi ya wanajeshi wakiwa katika doria,baada ya kuchukua madaraka ili kutuliza ghasia.
Picha, ya pili anaonekana, rais Marc Ravalomanana, akiwahutubia watu walio kuja kumsikiliza, kuzungumzia swala la kisiasa nchini humo ambalo lipo tete.
Wafanyakazi wa shirika la misaada waachiwa huru.
Darfur,Sudan - 15/03/09.Wafanyakazi wa shirika la madokta wasio na mipaka(MSF) Medicins Sans Frontires, ambao tekwa nyara siku siku ya jumatano, wameachiwa huru.
Wafanyakazi hao wananao tokea nchi za Itali na Kanada waliachiwa jana kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Sudan
Kwa kudhibitisha, maelezo hayo ya seikali ya Sudan, msemaji wa (MSF) linalo tokea nchini Ubeligiji ,Erwin van t'Land, alisema ya kuwa ni kweli wafanyakazi wenzao wamaachiwa huru.
Picha hapo juu, yanaonekana makazi ya wakimbizi wa ndini wa Sudan, ambo ni wanachi wa Sudan, wamekuwa wakiishi katika maeneo hayo, na msaada mkubwa wa matibabu umekuwa ukitolewa na mashirika haya ya kimataifa.
Nawaz Sharif, avunja amri ya kifungo."Aongoza maandamano".


Tehran,Iran - 14/03/09.Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, amesema kuendelea kuwekewa vikwazo kwa nchi yake ni mchezo wa kitoto,kwani hakutazuia nchi kundeleza utaalamu wa kutumia nguvu za nyuklia kwa ajili ya matumizi ya umeme na teknolojia.
Rais, Mahmoud Ahamadinejad, aliyasema hayo wakati walipo kuwa akizindua mtambo mpya wa kutengeneza nguvu za gasi uliopo kusini mwa Pars nchini Iran.
Maelezo haya ya rais wa Iran, yalikuja mara baada ya rais, wa Amerika Baraka Obama, kutangaza ya kuwa Amerika itaiwekea Irana vikwazo zidi kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Irana , Mahmoud Ahmadinejad,akihutubi wakati wa uzinduzi wa mtambo mya wa gasi, kwenye mji wa Pars nchini Iran..
No comments:
Post a Comment