Saturday, March 21, 2009

Nchi zaanza kulegeza vukwazo nchini Zimbabwe"Misaada yaanza kutolewa

Nchi zaanza kulegeza vikwazo nchini Zimbabwe."Misaada yaanza kutolewa".

Stockholm, Sweden - 21/03/09.Serikali ya Sweden, imesema itatoa kiasi cha million $ 10.5 kwa serikali ya Zimbabwe, kwa ajili ya kusaidia kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.
Uamuzi huo wa Sweden, kuipatia serikali ya Zimbabwe, pesa umefuatia wa ule wa serikali ya Australia kutoa msaada wa pesa mapema mwamzoni mwa mwezi tatu/2009, baada ya ya kuridhika na hai halisi ya kisiasa inavyo endelea nchini Zimbabwe.
Picha hapo juu, anaonekna rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, akiongea katika moja ya sherehe nchini Zimbabwe, mara baada ya chama chake kukubaliana kufanya kazi kwa pamoja na chama cha upinzani cha MDC, kinacho ongozwa na waziri mkuu Morgan Tsvangirai.
Amerika na Iran bado zawekeana vitendawili.
Tehran,Iran 21/03/09.Kiongozi mkuu wa Iran,Ayatollah Ali Khamenei, amesema yakuwa Iran ipo tayari kushirikiana na Amerika, ikiwa Amerika itabadilisha mwelekeo wake kuhusu Iran.
Kiingozi huyo wa Iran,Ayatollah Ali Khamenei,aliya sema haya wakati alipo kuwa akizungumza mbele ya maelfu ya Wairan waliokusanyika kusherekea siku ya kuanza mwaka mpya wa Iran.
Hatua ya kiongozi wa Iran kuongea hayo , imekuja baada ya rais wa Amerika, Baraka Obama, kuongea swala la Iran wakati alipo kuwa akiongea mbele ya vyombo vya habari mapema wiki hii.
Kwa kipindi kisicho pungua miaka 30, uhusiano kati ya Irana na Amerika, umekuwa siyo mzuri,tangu Iran ilipo wateka nyara baadhi ya wafanyakazi wa kibalozi wa Amerika, walio kuwa nchini Iran, wakati wa mageuzi ya kisiasa ya mwaka 1978.
Picha hapo juu anaonekana rais, wa Amerika Baraka Obama, akiongea wakati alipo kuwa akiongea mbele ya vyombo vya habari.
Picha ya pili,anaonekana kiongozi wa Iran,Ayatollah Ali Khamenei, akiongea wakati wa kuakaribisha mwaka mpya wa Wairan.
Usalama wa waweka amani Darfur mashakani.
Darfur,Sudan 20/03/09. Mmoja ya walizni wa amani kwenye maeneo ya Darfur, amepigwa risasi na kufa wakati wakiwa ulinzi kwenye kwenye maeneo ya Nyala.
Mashambulizi hayo yalitokea wakati watu wapatao wanane, waliojifunika uso, waliwashambula walinzi hao kwa ghafla wakati walipo kua katika doria, alisema msemaji wa (UNMID -UN Afrika Union force ) Kamal Daiki.
Hata hivyo akueleza ni askari huyo ametokea nchi gani.
Picha hapo juu anaokana askari wa UNAMID, akiwa ameshikilia mtutu, huku mbele yake kuna mtoto mdogo wa kike akiwa anamwangalia kwa makini.
Muungano wa nchi za Ulaya kutoa fedha mara dufu.
Prague,Czech -20/03.09.Viongozi wa muungano wa Ulaya, wamekubaliana kwa pamoja kuongeza mara dufu, fedha ili kuinua hali ya kiuchumi inalo likabili bara hili.
Akiongea haya waziri mkuu wa Czech,Mirek Topolanek,ambaye ndiye rais wa sasa wa muungano huu, alisema nchi za muungano wa ulaya zimekubaliana kutoa billion $68, wakati walipo kutana ijumaa ya wiki hii Brussel kuzungumzia hali halisi ya kiuchumi ya nchi za muungano huo.
Picha hapo juu wanaonekna viongozi wa muungano wa Ulaya wakipongezana mara baada ya kumaliza mkutano mjini Brussel siku ya ijumaa 18/03/09.
Baba aliyezaa na mtoto wake ahukumiwa kifungo cha maisha.
Viena,Austria - 20/03/09.Mahakama ya mji wa St Poelten, imemuhukumu kifungo cha maisha Josef Fritzl mwenye miaka 73, kwa kumkuta na hatia ya kumteka nyara, kumfanya mtumwa na kumweka kinyumba mtoto wake wa kike kwa kipindi kisicho pungua miaka 24 na kumzalisha watoto na mmoja ya watoto hao kufa kutokana na kukusa matibabu.
Kitendo hicho cha Josef Fritzl,kiliishangaza na kustua dunia, hasa jamii ya watu wa Ulaya kwani si kitu chakawaida katika jamii, alisema mmoja ya wakazi waliokuwa wakiishi karibu na Josef Fritzl.
Josef Fritzl, alitubu makosa yake mbele ya mahakama, baada ya mtoto wake wa kike kutoa ushaidi mbele ya mahakama,na ndipo kulimfanya akubali makosa, kwani mara ya kwanza alikuwa amekana makosa yake.
Picha hapo juu anaonekana, Josef Fritzl, akisindikizwa na polisi kueleka jela, baada ya kupata hukumu ya ke ya kukua maisha jela.
Picha ya pili, anaonekana mwanasheria wa Josef Fritzl,bwana Rudolf Mayer, akiongea mbela ya waandishi wa habari, mara baada ya kukumu zidi ya mteja wake.

No comments: