Monday, March 2, 2009

Rais wa Guinea Bissau, auwawa na wanajeshi"Hausishwa na kifo cha mkuu wa Jeshi"

Wafadhili na Wahisani wakutana kuchangisha ili kuijenga upya Ukanda wa Gaza.

Sharm El Sheikh,Misri - 02/03/09.Wafaziri na Wahisani wanakutana nchini Misri, kwa ajili ya mkutano wa kuchangisha pesa za kuijenga upya Ukanda wa Gaza.
Akiongea hayo, rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas,amesema ujenzi wa Ukanda wa Gaza utahitaji zaidi ya $ 5billion.
Akiongea na washiriki, Wahisani na Wafadhili, rais,Mahmoud Abbas,alisema yakuwa Wapalestina wataungana katika kuijenga maeneo yao.
Wahisani na Wafadhili hao, wanaotoka nchi 40, wanakutana mjini Sharm El Sheikh, wamesema pesa zote zitakazo tolewa zisipitie kwenye mikono ya Hamas.
Picha hapo juu, anaonekana waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika, Bi Hillary Clinton, akisalimiana na katibu mkuu wa Muungano wa Ulaya, bwana Javier Salana,wakati alipo wasili mjini Sharm El Shekh.
Picha ya pili ni ya moja ya jengo likiwa limebomolewa vibaya, kutokana na vita vilivyo tokea mwisho wa mwaka 2008 hadi mapema 2009 katikati ya mwezi wa Januari.
Rais wa Malawi, akamatwa na polisi.
Lilongwe, Malawi - 02/02/09. Polisi nchini Malawi, wamemkamata aliyekuwa rais wa nchi hiyo, bwana Bakili Muluzi, kwa kushukiwa kutumia pesa zipatazo million 11, pesa zilizo tolewa na wahisani.
Rais, Bakili Muluzi,ambaye alitawala Malawi tangu mwaka 1994 hadi 2004, analaumiwa kwa kuzitumia pesa hizo kwa matumizi yake binafsi.
Kesi ya mauaji ya, Rafiki Hariri, yafunguliwa nchini Uhollanzi.
The Hague,Uhollanzi - 02/03/09.Umoja wa mataifa, umefungua koti ya kimataifa itakayo shughulika kesi ya mauaji ya aliye kuwa waziri mkuu wa Lebanoni, Rafiki Hariri.
Waziri mkuu, Rafiki Hariri, aliuwawa kwa bomo mnamo tarehe, 14/02/05 na watu wengine 22 walipoteza maisha yao pia.
Kuuwawa kwa bwana , Hariri, kulisabababisha Syria, kujiondoa toka Lebanoni,baada ya kuwepo nchini humo kijeshi kwa miaka mingi.
Picha hapo juu, linaonekana moja ya gari likiwa limeshika moto,baada ya kulipuliwa na bomu, na kutokana na ajari hiyo, waziri mkuu, Rafiki Hariri alipoteza maisha.
Picha ya pili, anaonekana hayati, waziri mkuu wa Lebanoni, enzi za uhai wake.
Rais wa Guinea Bissau,auwawa na wanajeshi "Hausishwa na kifo cha mkuu wa Jeshi".
Bissau, Guine Bissau - 02/03/09. Rais wa Guinea Bissau,Joao Bernardo Vieira,ameuwawa kwa kupigwa risasi wa wanajeshi wakati akiwa nyumbani kwake mapema leo hasubuhi, 02/03/09.
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi, Zamora Induta, alisema mauaji haya yamefanyika na wanajeshi wa karibu wa aliyekuwa mkuu wa majeshi, Generali Tagme Na Waie, aliye uwawa mapema siku ya jumapili, baada ya risasikwa kufyatuliwa na mlipuko wa bomu kutokea karibu na eneo alilo kuwa amekaa.
Hata hivyo, msemaji huyo wa jeshi, alisema yakuwa , rais,ni moja ya watu waliohusika katika mauaji ya Generali,Tagme Na Waie.
Picha hapo juu, ni ya rais wa, Guinea Bissau, Joao Bernardo Vieira,anaonekana enzi za uhai wake, akitoa saluti , wakati jeshi lilipo pita mbele ya katika moja ya sherehe za kitaifa.
Kemikal Ali - (Chemical Ali) ahukumiwa kunyongwa.
Baghdad,Irak-02/03/09.Jaji wa mahakama kuu nchini Irak, Mohammed Al Uraibi, amemuhukumu kunyongwa aliyekuwa aliyekuwa waziri wa ulinzi, wakati wa hayati rais Saddam Hussein, bwana Ali Hassan Al Majid.
Bwana, Ali Al Majid, aliyejulikana kama Kemikal Ali(Chemical Ali),alihukumiwa kunyongwa baada ya hakimu,Mohammed Al Uraibi, kumkuta na hatia ya kuu ruhusu mauaji ya Wairak wa jamii ya Kishia mnamo mwaka 1999.
Picha hapo juu,anaonekana, bwana, Ali Al Majid ( Chemical Ali), akijieleza mbele ya jaji, kabla ya kkuhukumiwa kunyongwa.

No comments: