Sunday, March 22, 2009

China kujiandaa kushindana na nguvu za kiaanga.

Mchezaji wa mpira wa miguu apigwa risasi kiwanjani.

Baghdad,Irak-22/03/09.Polisi nchini Irak wamesema mmoja ya mchezaji wa mpira wa miguu, alipigwa risasi ya kichwa na kufa hapo hapo wakati alipo kuwa anaijiandaa kupiga mpira wa adhabu ndogo.
Msemaji wa polisi, Mej,Muthanna Kharid, alisema mchezaji huyo wa timu ya Buhairat, alipigwa risasi na moja ya mshabiki wa timu pinzani ya Sinjar wakati zikiwa zimesalia dakika chache kabla ya mpira kumalizika.
Katika mechi hiyo timu ya Sinjar, ilikuwa inaongoza kwa goli moja.
Hata hivyo, shabiki huyo alikamatwa na polisi mara moja, alimalizia kusema haya masemaji wa Polisi.
Picha hapo juu, wanaonekana baadhi ya wapenzi wa mpira wa miguu wakishangilia mara baada ya timu yao kushinda kombe la matifa ya Asia wakati walipo rudishwa kushiriki mashindano ya kimataifa.
China kujiandaa kushindana na nguvu za kiaanga.
Beijing, China, 22/03/09.Makubaliano kati ya China na Muungano wa Ulaya, kuhusu ujenzi wa pamoja wa chombo cha kuruka angani Galileo, kutoleta zao mafanikio, yameifanya China kuamua kujenga chombo chakuruka angani peke yake .
Kuamua kwa Chini kuendelea na ujenzi huo, kutaifanya China kuwa na uwezo sawa wakianga na nchi kama Amerika na Urussi.
Kutoleta mafanikio ya kushirikiana kujenga chombo hicho, kumekuja hasa kwa kuzingztia swala la usalama ambalo lililtwa na moja ya nchi mwanachama wa Muungano wa Ulaya.
Picha hapo juu, inaonekana moja ya chombo kinaruka kuelekea ngani , kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano.
Vita vya Gaza vyaleta mjadala katika jamii nchini Israel.
Jerusalem. Israel 22/03/09.Habari zinazo endele kutolewa na baadhi ya askari wa jeshi la Israel, kuhusu hali halisi ya vita kati ya Israel na Palestina, mapema mwisho wa mwaka 2008 hadi mwazo wa mwaka 2009, zinazidi kuleta hali ya wasiwasi na mvutano hivyo na kuleta mjadala mkubwa katika jamimii nzima ya Israel na kuhusu imani na ulinzi wa nchi.
Hii ina kuja baada ya ya baadhi ya watu kujadili kuwepo kwa vita hivi kwani vinakwenda kinyume na matakwa ya kidini,na wengine wana sema hii ni lazima kulinda taifa la Israel,kwani ni taifa teule na ni lazima walilinde kwa hali na mali.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya askari wa Israel wakiwa wamesima kwa pamoja kabla ya kuendelea na mapambano na kundi la Hamas kwenye eneo la ukanda wa Gaza.
Rais wa Sudan ashauriwa kuto kuhudhuria mkutano.
Khartoum,Sudan 22/03/09. Shule moja ya kidini nchini Sudan imemshauri rais wa Sudan,Omar Al bashir , kuto safiri nchini Katar, kuhudhuria mkutano wa nchi wanachama wa jumuia ya nchi za nchi za Kislam unaotarajiwa kuanza 30,03/09.
Shule hiyo Ulema, imesema hatuapendele rai Omar Al Bashir, kwenda huko kwenye mkutano, badala yake aende mwakilishi wake atakaye chaguliwa na serikali..
Hii onyo limetolewa, baada ya mahakama ya ianayo shughulika makosa ya jina na iliyopo nchini Uhollandi, kutowa kibali cha kukamatwa kwa rais huyo wa Sudan, ili ashitakiwe.
Picha hapo juu, anaonekana rais wa Sudan Omar Al Bashir, akishangalia kwa kucheza moja ya ngoma za kiasili za Sudan, wakati alipo tembelea katika jimbo moja nchini Sudan.
Picha ya pili wanaonekana, baaadhi ya wananchi maelfu wamekuja kumlaki, rais Omar Al bashir,alipo kwenda kuwatembele kwenye maeneo yao.

No comments: