Tuesday, March 3, 2009

Ulimwengu wa mchezo wa kriket waingia dao kubwa nchini Pakistan

Mke wa rais afungwa jela miaka mitatu. Lusaka, Zambia - 03/03/09. Mke wa rais wa zamani wa Zambia Frederick Chiluba, amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu na nusu, baada ya kukutwa na hatia ya kupokea pesa kinyume cha sheria. Ka mujibu wa mahakama,Bi Regina Chiluba,alipokea pesa hizo za serikali na kuzitumia kwa kujengea nyumba na kufanyia biashara wakati mume wake alipo kuwa rais. Wakati wa hukumu hiyo, rais huyo wazamani wa Zambia, Frederick Chiluba, alikuwepo mahakani, Hata hivyo rais huyo wa zamani wa Zambia, anakesi inayo mkabili kwa kutumia vibaya pesa za umma wakati akiwa madarakani. Picha hapo juu wanonekna, rais wa zamani wa Zambia, Frederick Chiluba na mkewe bi Regina Chiluba, wakiwa mahakamani siku chache kabla ya hukumu ya kwenda kutumikia kifungo cha miaka kwa miaka mitatu na nusu kwa bi Regina Chiluba kutolewa leo 03/03/09. Ulimwengu wa mchezo wa kriket waingia doa kubwa nchini Pakistan.

Lahore, Pakistan - 03/03/09.Wapakistan sita wamepoteza maisha yao na wachezaji sita wa timu ya Kriket ya Sri Lanka,kujeruhiwa vibaya baada ya watu wasiojulikana kushambulia msafara huo wa wachezaji karibu na uwanja wa Gaddafi, wakati tumu ya Pakistan ikicheza na Sri Lanka.
Mashambulizi hayo yaliyo fanywa kwa kutumia bunduki na pia kulipatikana bomu la kutupa kwa mkono ambalo halikulipuka.
Salman Taseer, mkuu wa jimbo la Punjab, alisema mashambulizi hayo yanafanana kama yale yaliyo tokea jijini Mumbai.
Picha ya hapo juu wanaonekana, polisi wa kiangalia kwa makini, kwenye kiti cha gari la polisi, ambalo lilishambuliwa wakati likisindikiza msafara wa wachezaji wa kriket wa timu ya Sri Lanka.
Picha pili hapo juu, wanaonekana kwa mbali baadhi ya watu wakiwa wameshilikia mitutu(bunduki) kuelekeza eneo la tukio.
Waziri mkuu wa Uingereza afanya ziara rasmi nchini Amerika.
Washington, Amerika - 03/03/09.Waziri mku wa Uingereza , Gordn Brown, amefanya ziara rasmi nchini Amerika, kwa mazungumzo ya kiserikali.
Waziri mkuu, Gordon Brown, amekuwa kiongozi wa kwanza, kufanya ziara nchini Amerika tangu rais, Baraka Obama, kuapishwa kuwa rais wa Amerika.
Ziara hiyo, imefanyika mapema, kabla ya kikao cha wakuu wa nchi 20 , kuudhulia kikao kitakacho fanyika njini London April 2 mwaka huu 2009.
Pichani hapo juu, wanaonekana rais, Baraka Obama na waziri mkuu wa Uingereza, wakisalimiana, mapema baada ya waziri mkuu, Gordon Brown kuwasili nchini Amerika.
Bi, Hillary Clinton, atembelea Izrael kwa mazungumzo.
Jerusalem,Izrael -03/03/09. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika, Bi, Hillary Clinton, amefanya mazungumzo viongozi wa Izrael,na kusisitiza yakuwa Amerika itashirikiana na Izrael kwa kila hali.
Hata hivyo , Bi, Hillary Clinton, alisisitiza ya kuwa swala la kuwepo kwa taifa la Palestina, ni njia moja ambayo Amerika inaliona ndiyo njia pekee ya kutatua mgogoro wa eneo hilo.
Picha hapo juu, anaonekana na mmoja wa viongozi wa Izrael , bwana, Benjamin Tetanyahu, wakati walipo kutana kwa mazungumzo.
Picha ya pili anaonekana rais wa Izrael, Shimon Peres na waziri wa mambo ya nje wa Amerika, Bi, Hillary Clnton kabla ya kuanza mazungumzo.

No comments: